top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

ULY CLINIC

18 Septemba 2026, 14:24:24

Ammi visnaga

Asili ya Ammi visnaga ni Afrika Kaskazini na maeneo mengine ya nchi za Mediterania, na kwa sasa mmea huu unazalishwa katika nchi nyingi duniani. Kwa miaka mingi, mmea huu umetumika kutibu maumivu ya figo yanayotokana na mawe na pumu ya kifua kutokana na uwezo wake wa kulegeza misuli.


Sifa za mmea Ammi visnaga

Mmea huu huwa na ladha ya uchungu, lakini una uwezo mkubwa wa kitiba kama kilainisha misuli.


Uwezo wa Ammi visnaga kitiba

Hutibu maumivu ya figo yanayotokana na mawe kwa kulegeza misuli ya mrija wa mkojo unaoitwa yureta, hivyo kufanya mawe yatoke kwa urahisi.


Hutumika kutibu pumu ya kifua. Licha ya kutokuwa na uwezo mkubwa wakati wa mshiko wa pumu, hupunguza vipindi vya kupatwa na pumu.


Hutumika pia kutibu magonjwa mengine kama bronkaitiz, emfizima na dondakoo.


Matumizi ya Ammi visnaga kama dawa

Mmea huu haupaswi kutumika kama dawa bila ushauri wa daktari kwa sababu matumizi ya muda mrefu yanaweza kusababisha kichefuchefu, kipanda uso na kukosa usingizi. Mmea huu hauruhusiwi kutumika katika baadhi ya nchi.


Infusheni ya mmea huu hutumika kupunguza dalili za pumu ya kifua, mawe kwenye figo na bronkaitiz.

Unga wa dawa hii hutumika kutibu anjaina.


Majina mengine ya Ammi visnaga

Ammi visnaga hufahamika kwa majina mengine kama:

  • Dawa asili ya mawe ya figo

  • Dawa asili ya maumivu ya mawe ya figo

  • Dawa asili ya pumu ya kifua

  • Dawa asili ya bronkaitiz

  • Dawa asili ya emfizima

  • Dawa asili ya dondakoo

Namna ya kuandaa aina mbalimbali za dawa kutoka kwenye mmea


Namna ya kuandaa infusheni ya dawa asilia

Infusheni huandaliwa kwa kuzamisha sehemu ya mmea unayotaka kutumia kama dawa kwenye kiasi cha maji yaliyochemka. Baada ya kuzamisha kwenye maji yaliyochemka, maji hayo huchujwa baada ya dakika 15. Dozi ya dawa inayotakiwa kuandaliwa kwa wastani huwa ni gramu 1 kwa kila mililita 10 za maji.


Kuna dawa nyingi asilia ambazo tayari zimetengenezwa na kufungwa kwenye vifungashio vya karatasi, ambapo unaweza kuzitumia kwa urahisi kama majani ya chai ya kuchovywa. Dawa zilizo katika fomu hiyo hupunguza muda wa kuandaa.


Namna ya kuandaa dikokshen ya dawa asilia

Dikokshen hutumika kuvuna kiini cha dawa ambacho hakiathiriwi na joto.

Ili kuandaa dikokshen ya dawa, chemsha magome au mizizi ya mmea kwa muda wa dakika 15 hadi 60, kutegemea aina ya mmea au kiini cha dawa. Kisha ipooze na ongeza maji ya baridi ili kutengeneza kiasi cha dawa na wingi wa kiini unaohitaji.


Endapo dawa inatakiwa kuchemshwa kwa muda mrefu, unatakiwa kuongeza kiasi cha maji yaliyopotea ili dawa isiungue.


Dozi ya dikokshen ni sawa na infusheni, yaani gramu 1 ya mmea kwa kila mililita 10 za maji, isipokuwa endapo dawa ina uteute mwingi. Katika hali hiyo, gramu 1 inatakiwa kuchanganywa na mililita 20 za maji.


Namna ya kuandaa mmeng’enyo wa dawa

Kuandaa mmeng’enyo wa dawa kwa njia hii, unatakiwa kuweka dawa yako kwenye chombo kisha kuongeza maji yenye joto linalotakiwa. Mara nyingi joto linatakiwa kuwa kati ya nyuzi 35 hadi 40 za sentigredi, kutegemea aina ya dawa.

Lengo kuu la kuzingatia joto ni kutoharibu kiini cha dawa ambacho kinategemea joto.


Namna ya kuandaa masalesheni ya dawa

Ili kuandaa masalesheni ya dawa, saga au katakata dawa katika vipande vidogo sana, kisha viweke kwenye chombo cha kioo chenye kimiminika cha kufyonza dawa.

Funika mchanganyiko huo na uache kwa muda wa siku tatu au zaidi kwenye joto la ndani ya nyumba. Baada ya kutimia kwa siku tatu, tikisa kwa nguvu mara nyingi ili dawa iingie kwenye kimiminika.


Baada ya hapo, chuja dawa na kamua unga au vipande ili dawa yote itoke. Kisha unaweza kuchuja dawa kwa ajili ya matumizi au kuifanyia dekatensheni ili kupata kiini safi cha dawa.


Namna ya kuandaa pakolesheni ya dawa

Hii ni njia maarufu ya kuandaa tinkcha ya dawa au kufyonza dawa kutoka kwenye kimiminika. Njia hii inahitaji chombo maalumu chenye jina la pakoleta na unatakiwa kuwa mtaalamu zaidi ili kuandaa dawa kwa njia hii.


Soma zaidi kuhusu njia hii kupitia kiungo kilichowekwa chini ya tovuti hii.


Namna ya kuandaa dawa ya kufyonza kwa kimiminika

Njia hii huandaa dawa kutoka kwenye kimiminika chenye dawa au tishu za mnyama kwa kufyonza dawa hiyo kwa kutumia kimiminika kingine, hasa pombe aina ya ethanol au maji.

Kiasi cha pombe na maji kinachowekwa hutegemea aina ya dawa. Njia hii inahitaji uwe mtaalamu wa kuandaa dawa. Unaweza kujifunza zaidi namna ya kuandaa dawa kwa njia hii kupitia kiungo kilichowekwa chini ya tovuti hii au kutumia dawa ambazo tayari zimeandaliwa.


Namna ya kuandaa tinkcha ya dawa

Tinkcha ya dawa huandaliwa kwa kufanya masalesheni au pakolesheni ya dawa kwa kutumia kimiminika cha pombe pekee. Njia hii ni nzuri ya kuvuna kiwango cha kiini unachotaka kutoka kwenye mimea au mnyama.


Soma zaidi kuhusu njia hii kupitia rejea zilizo chini ya makala hii.


KUMBUKA

Kama kuna haja ya kuchemsha dawa, hakikisha unatumia chombo kilichotengenezwa kwa udongo au sufuria za chuma cha pua (stainless steel), na usifunike wakati wa kuchemsha ili kutoa sumu na kutobadili kiini cha dawa.


Usitumie zaidi ya dawa moja kutibu tatizo moja au mawili tofauti ili kuepuka madhara na mwingiliano wa dawa.


Endapo unatumia dawa za hospitali, wasiliana na daktari wako akushauri ili kuepuka mwingiliano wa dawa na madhara yanayoweza kutokea.

Imeandikwa:

27 Juni 2021, 20:06:35

ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute msaada kutoka kwa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala hii

Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na Tiba kupitia kitufe cha 'Pata tiba' au 'Mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii.

Rejea za mada hii;

bottom of page