top of page

Anacardium occidentale

Imeandikwa na:

@ ULY CLINIC

27 Juni 2021 17:49:53

Utangulizi

Anacardium occidentale ni mmea wenye jina jingine la mkorosho, asili yake ni tropiki ya Amerika na kwa sasa unapatikana katika nchi nyingi zilizo kwenye ukanda wa tropiki. Magamba ya Anacardium occidentale yamekuwa yakitumika kama dawa ya maumivu ya tumbo.

Sifa za mti Anacardium occidentale

Mkorosho ni mtu unaokuwa na kufikia urefu wa mita 8 hadi 10, huwa na matawi ya pembeni na majani ya umbile la yai au ya uviringo yenye sentimita 10 za upana na 12 za urefu. Huzaa matunda na chini ya tunda huwa na karanga (korosho) iliyofunikwa na gamba.

Uwezo wa kitiba wa Anacardium occidentale

Magamba ya mkorosho yana uwezo wa kushusha kiwango cha sukari kwenye damu kuanzia dakika 10 hadi 20 toka mgonjwa amekunywa dawa iliyotengenezwa na magome hayo na kukifanya kiwe chini kwa muda wa masaa 3 mfululizo.

Uwezo wake wa kushusha shinikizo la damu umethibitishwa kwenye tafiti za panya na nyani, hii ni kutokana na uwezo wake wa kulegeza misuli laini ya mshipa ya damu. Uwezo wake wa kushusha shinikizo la juu la damu hudumu zaidi ya masaa 10.

Tannis inayotoka kwenye magamba yake pia huwa na uwezo wa kuzuia michomo ya kinga za mwili katika tafiti za panya na mafuta yake huwa na uwezo wa kutuliza/ kushusha hali ya moyo.

Matumizi ya Anacardium occidentale kama tiba

Kupunguza shinikizo la damu na kiwango cha sukari kwenye damu

• Tengeneza masalesheni ya gramu 10 za unga wa magome ya mkorosho kwenye mililita 200 za maji, kunywa mililita 20 mara mbili kwa siku. Hakikisha unapima shinikizo la damu na sukari

Matibabu ya kisukari

• Tumia infusheni ya majani au magamba

Majina mengine ya Anacardium occidentale

Dawa hii hufahamika kwa jina jingine kama;

• Dawa asili ya kisukari
• Dawa asili ya shinikizo la juu la damu
• Dawa asili ya michomo ya kinga za mwili

Namna ya kuandaa aina mbalimbali za dawa kutoka kwenye mmea

​

Namna ya kuandaa infusheni ya dawa asilia

​

Infusheni huandaliwa kwa kuzamisha sehemu ya mmea unayotaka kutumia kama dawa kwenye kiasi cha maji yaliyochemka. Baada ya kuzamisha kwenye maji yaliyochemka, maji hayo huchujwa baada ya dakika 15. Dozi ya dawa inayotakiwa kuandaliwa kwa wastani huwa ni gramu 1 kwa kila mililita 10 za maji.

​

Kuna dawa nyingi asilia zimeshatengenezwa na kufungwa kwenye vifungashio vya karatasi ambapo unaweza kutumia kirahisi kama majani ya chai ya kuchovywa. Dawa kwenye fomu hiyo zitapunguza muda wa kuandaa.

​

Namna ya kuandaa dikokshen ya dawa asilia

​

Dikokshen hutumika kuvuna kiini cha dawa ambacho hakiathiriwi na joto.

​

Ili kuandaa dikokshen ya dawa, chemsha magome au mizizi ya mmea kwa muda wa dakika 15 hadi 60 (hutegemea aina ya mmea au kiini cha dawa), kisha pooza na ongeza maji ya baridi ili kutengeneza kiasi cha dawa na wingi wa kiini unachohitaji.

​

Endapo dawa inatakiwa kuchemka kwa muda mrefu, unatakiwa ongezea kiasi cha maji yaliyopotea ili dawa isiungue.

​

Dozi ya dikoksheni ni sawa na infusheni yaani gramu moja ya mmea kwa mililita 10 za maji isipokuwa endapo dawa ina uteute mwingi, gramu moja inatakiwa kuchanganywa na mililita 20 za maji.

 

Namna ya kuandaa mmengenyo wa dawa

 

Kuandaa mmeng’enyo wa dawa kwa njia hii unatakiwa weka dawa yako kwenye chombo kisha ongeza maji yenye joto linalotakiwa, mara nyingi joto linatakiwa kuwa kati ya nyuzi za sentigrade 35 hadi 40 ikitegemea aina ya dawa. Lengo kuu la kuzingatia joto ni kutoharibu kiini cha dawa ambacho kinategemea joto.

​

Namna ya kuandaa masalesheni ya dawa

 

Ili kuandaa masalesheni ya dawa, saga au katakata dawa kwenye vipande vidodo vidogo sana kisha weka kwenye jaa ya kioo yenye kimiminika cha kufyonza dawa. Funika mchanganyiko na acha kwa muda wa siku tatu au zaidi kwenye joto la ndani ya nyumba.Baada ya kutimia kwa siku tatu, tikisa kwa nguvu mara nyingi ili dawa iingie kwenye kimiminika. Baada ya hapo chuja dawa na kamua unga au vipande ili dawa yote itoke. Baada ya hapo unaweza kuchuja dawa kwa ajili ya matumizi au kuifanyia dekatensheni ili kupata kiini safi cha dawa.

​

Namna ya kuandaa pakolesheni ya dawa

 

Hii ni njia maarufu ya kuandaa tinkcha ya dawa au kufyonza dawa kutoka kwenye kimiminika.  Njia hii inahitaji chombo maalumu chenye jina la pakoleta na unatakiwa kuwa mtaalamu zaidi kuandaa dawa kwa njia hii. Soma zaidi maelezo kwa kutumia linki chini ya tovuti hii.

 

Namna ya kuandaa dawa ya kufyonza kwa kimiminika

​

Njia hii huandaa dawa kutoka kwenye kimiminika chenye dawa au tishu za mnyama kwa kufyonzwa dawa hiyo kwa kutumia kimiminika kingine haswa pombe aina ya ehthanol  au maji.

 

Kiasi cha pombe na maji yanayowekwa hutegemea aina ya dawa. Njia hii inahitaji uwe mtaalamu wa kuandaa dawa, unaweza kujifunza zaidi namna ya kuandaa dawa kwa njia hii kupitia linki chini ya tovuti hii au tumia dawa ambazo tayari zimekwisha andaliwa.

​

Namna ya kuandaa tinkcha ya dawa

 

Tinkcha ya dawa huandaliwa kwa kufanya masalesheni au pakolesheni ya dawa kwa kutumia kimiminika cha pombe tu. Njia hii ni nzuri ya kuvuna kiwango cha kiini unachotaka kutoka kwenye mimea au mnyama. Soma zaidi kuhusu njia hii kupitia rejea chini ya Makala hii.

​​

KUMBUKA:

 

Kama kuna haja ya kuchemsha dawa, hakikisha unatumia chomo kilichotengenezwa na udongo au sufuria za stainless steel na usifunike wakati wa kuchemsha ili kutoa sumu na kutobadili kiini cha dawa.

 

Usitumie dawa zaidi moja na kutibu tatizo moja au mawili tofauti ili kuepuka madhara na mwingiliano

​

Endapo unatumia dawa za hospitali, wasilina na daktari wako kukushauri ili kuepuka mwingiliano wa dawa na madhara yanayoweza kutokea.

ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute msaada kutoka kwa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala hii

Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na Tiba kupitia kitufe cha 'Pata tiba' au 'Mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

27 Juni 2021 17:50:28

Rejea za mada hii;

bottom of page