top of page

Barosma betulina

Imeandikwa na:

@ULY CLINIC

28 Juni 2021 19:28:44

Utangulizi

Ni mmea wa dawa wenye asili ya Afrika Kusini na hukuzwa kwenye baadhi ya nchi Amerika ya kusini. Hukua kwenye mazingira yenye jua kali na yenye maji.

Sifa za mmea Barosma betulina

Mmea wa buchu kitamaduni umekuwa ukitumika kama kichocheo cha mfumo wa fahamu na tiba ya kupunguza maji mwilini, pia hufanya kazi ya kutibu magonjwa ya tumbo. Baadhi ya watu wa magharibi wamekuwa wakitumia dawa hii kama tiba ya UTI na magonjwa mengine ya mfumo wa mkojo.

Uwezo wa Barosma betulina kitiba

Barosma betulina kitiba umekuwa ukitumika kupunguza maji mwilini na kupunguza kiungulia na gesi tumboni

Nchi za magharibi zilianza kutumia mmea huu mwaka 1790 kama dawa asilia ya kutibu maambukizi ya bakteria kwenye njia ya mkojo(UTI) na michomo kwenye kibofu cha mkojo.

Hata sasa Barosma betulina bado unaendelea kufanya kazi hiyo ya kutibu magonjwa mbalimbali katika mfumo wa mkojo

Matumizizi ya infusheni au tinkcha ya mmea huu hutibu UTI ya kibofu cha mkojo na mrija wa urethra.
Kwa bahati mbaya infusheni ya dawa ilipowekwa kwenye uke kwa wagonjwa waliokuwa na uchafu mweupe ukeni, ilisababisha kujongea kwa misuli ya uzazi hivyo ilionekana kuwa na uwezo wa kutoa mimba. Haishauriwi kutumika kwa mjamzito.

Matumizi ya Barosma betulina kama dawa

Kutibu tezi dume, tumia infusheni ya dawa vikombe viwili kila baada ya masaa 12

Kwa maambukizi sugu ya UTI, tumia matone 40 ya tinkcha ya dawa kwenye maji kila baada ya masaa 8
Kwa maambukizi ya UTI ya kibofu cha mkojo, tumia tembe ya miligramu 500 mara mbili kwa siku

Majina mengine ya dawa Barosma betulina

Mmea wa Barosma betulina hufahamika kwa majina mengine ya;

• Dawa asili ya tezi dume
• Dawa asili ya gesi tumboni
• Dawa asili ya kutoa mimba
• Dawa asili ya UTI sugu
• Dawa asili ya kupunguza maji mwilini
• Dawa asili ya kuanzisha uchungu

Namna ya kuandaa aina mbalimbali za dawa kutoka kwenye mmea

Namna ya kuandaa infusheni ya dawa asilia

Infusheni huandaliwa kwa kuzamisha sehemu ya mmea unayotaka kutumia kama dawa kwenye kiasi cha maji yaliyochemka. Baada ya kuzamisha kwenye maji yaliyochemka, maji hayo huchujwa baada ya dakika 15. Dozi ya dawa inayotakiwa kuandaliwa kwa wastani huwa ni gramu 1 kwa kila mililita 10 za maji.

Kuna dawa nyingi asilia zimeshatengenezwa na kufungwa kwenye vifungashio vya karatasi ambapo unaweza kutumia kirahisi kama majani ya chai ya kuchovywa. Dawa kwenye fomu hiyo zitapunguza muda wa kuandaa.

Namna ya kuandaa dikokshen ya dawa asilia

Dikokshen hutumika kuvuna kiini cha dawa ambacho hakiathiriwi na joto.

Ili kuandaa dikokshen ya dawa, chemsha magome au mizizi ya mmea kwa muda wa dakika 15 hadi 60 (hutegemea aina ya mmea au kiini cha dawa), kisha pooza na ongeza maji ya baridi ili kutengeneza kiasi cha dawa na wingi wa kiini unachohitaji.

Endapo dawa inatakiwa kuchemka kwa muda mrefu, unatakiwa ongezea kiasi cha maji yaliyopotea ili dawa isiungue.

Dozi ya dikoksheni ni sawa na infusheni yaani gramu moja ya mmea kwa mililita 10 za maji isipokuwa endapo dawa ina uteute mwingi, gramu moja inatakiwa kuchanganywa na mililita 20 za maji.

 

Namna ya kuandaa mmengenyo wa dawa

 

Kuandaa mmeng’enyo wa dawa kwa njia hii unatakiwa weka dawa yako kwenye chombo kisha ongeza maji yenye joto linalotakiwa, mara nyingi joto linatakiwa kuwa kati ya nyuzi za sentigrade 35 hadi 40 ikitegemea aina ya dawa. Lengo kuu la kuzingatia joto ni kutoharibu kiini cha dawa ambacho kinategemea joto.

Namna ya kuandaa masalesheni ya dawa

 

Ili kuandaa masalesheni ya dawa, saga au katakata dawa kwenye vipande vidodo vidogo sana kisha weka kwenye jaa ya kioo yenye kimiminika cha kufyonza dawa. Funika mchanganyiko na acha kwa muda wa siku tatu au zaidi kwenye joto la ndani ya nyumba.Baada ya kutimia kwa siku tatu, tikisa kwa nguvu mara nyingi ili dawa iingie kwenye kimiminika. Baada ya hapo chuja dawa na kamua unga au vipande ili dawa yote itoke. Baada ya hapo unaweza kuchuja dawa kwa ajili ya matumizi au kuifanyia dekatensheni ili kupata kiini safi cha dawa.

Namna ya kuandaa pakolesheni ya dawa

 

Hii ni njia maarufu ya kuandaa tinkcha ya dawa au kufyonza dawa kutoka kwenye kimiminika.  Njia hii inahitaji chombo maalumu chenye jina la pakoleta na unatakiwa kuwa mtaalamu zaidi kuandaa dawa kwa njia hii. Soma zaidi maelezo kwa kutumia linki chini ya tovuti hii.

 

Namna ya kuandaa dawa ya kufyonza kwa kimiminika

Njia hii huandaa dawa kutoka kwenye kimiminika chenye dawa au tishu za mnyama kwa kufyonzwa dawa hiyo kwa kutumia kimiminika kingine haswa pombe aina ya ehthanol  au maji.

 

Kiasi cha pombe na maji yanayowekwa hutegemea aina ya dawa. Njia hii inahitaji uwe mtaalamu wa kuandaa dawa, unaweza kujifunza zaidi namna ya kuandaa dawa kwa njia hii kupitia linki chini ya tovuti hii au tumia dawa ambazo tayari zimekwisha andaliwa.

Namna ya kuandaa tinkcha ya dawa

 

Tinkcha ya dawa huandaliwa kwa kufanya masalesheni au pakolesheni ya dawa kwa kutumia kimiminika cha pombe tu. Njia hii ni nzuri ya kuvuna kiwango cha kiini unachotaka kutoka kwenye mimea au mnyama. Soma zaidi kuhusu njia hii kupitia rejea chini ya Makala hii.

KUMBUKA:

 

Kama kuna haja ya kuchemsha dawa, hakikisha unatumia chomo kilichotengenezwa na udongo au sufuria za stainless steel na usifunike wakati wa kuchemsha ili kutoa sumu na kutobadili kiini cha dawa.

 

Usitumie dawa zaidi moja na kutibu tatizo moja au mawili tofauti ili kuepuka madhara na mwingiliano

Endapo unatumia dawa za hospitali, wasilina na daktari wako kukushauri ili kuepuka mwingiliano wa dawa na madhara yanayoweza kutokea.

ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute msaada kutoka kwa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala hii

Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na Tiba kupitia kitufe cha 'Pata tiba' au 'Mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

28 Juni 2021 19:35:26

Rejea za mada hii;

bottom of page