top of page

Butyrospermum parkii

Imeandikwa na:

Dkt. Benjamin L, MD

5 Agosti 2021 19:27:38

Utangulizi

Butyrospermum parkii, hujulikana kwa jina jingine la shea, hufahamika sana Afrika kutokana na uwezo wake wa kutibu magonjwa ya ngozi kavu, pumu ya ngozi na kutumiwa kwenye urembo wa ngozi na nywele kwa wanawake.

Sifa za Butyrospermum parkii

Butyrospermum parkii ni mti poli unaostawi karibia nchi 20 za ukanda wa joto Afrika ikiwa pamoja na Senegal, Uganga, Kenya na sehemu chache Tanzania.

• Tunda lake ni tamu, huwa na kipenyo cha sentimita 2 hadi 5
• Ndani ya karanga kuna mafuta. Karanga imefunikwa kwa gamba gumu
• Mafuta yake huwa na kiwango kikubwa cha ascorbic acid ukilinganisha na chungwa
• Mafuta pia huwa na madini chuma na kalisiamu, manganese, sodiamu, potasiamu, zinki, vitamin C, B n.k

Uwezo wa Butyrospermum parkii kitiba

Majani, magome, mizizi na Tunda la mbegu ya Butyrospermum parkii limekuwa likitumiwa kama tiba ya;

• Ngozi kavu
• Pumu ya ngozi
• Maumivu ya tumbo
• Maumivu ya kichwa
• Homa
• Manjano
• Kuongeza uzalishaji wa maziwa kwa wajawazito
• Kuondoa sumu ya nyoka iliyotemwa kwenye macho

Matumizi ya nje

• Kulainisha nywele
• Kuzuia ngozi kupigwa na mwanga wa jua

Matumizi ya Butyrospermum parkii kitabibu

• Kutibu pumu ya ngozi
• Kupunguza michomo kinga kwenye ngozi
• Kuondoa maumivu ya ngozi kutokana na jeraha au kuungua moto

Namna ya kutumia Butyrospermum parkii

Kutibu maumivu ya kichwa na homa, jifukize kwa kutumia majani yake au osha kichwa kwa kutumia maji yaliyotokana na kuloweka mizizi yake

Kutibu pumu ya ngozi- Paka mafuta yake kwenye maeneo yenye tatizo kila siku.

Matokeo ya matumizi ya mafuta ya Butyrospermum parkii

Tafiti zinaonyesha kuwa, kupaka mafuta au kula karanga ya Butyrospermum parkii husababisha

• Kutozeeka kwa ngozi haraka
• Kupungua kwa kiwango cha protini kwenye damu na figo
• Kupungua kwa kiwango cha lehemu(kolestro) kwenye damu
• Huondoa dalili kali za pumu ya ngozi

Majina mengine ya Butyrospermum parkii na sehemu unapoweza kupata mazao yake

Hufahamika pia kwa jina la kisayansi kama Vitellaria parkii.

Unaweza kupata mazao ya mtu huu kwa ajili ya matibabu ya pumu ya ngozi Tanzania, Kenya na Uganda.

Tumia kitufe cha mawasiliano yetu chini ya tovuti hii kwa kutuma ujumbe wa 'Nahitaji dawa ya Butyrospermum parkii'

Namna ya kuandaa aina mbalimbali za dawa kutoka kwenye mmea

Namna ya kuandaa infusheni ya dawa asilia

Infusheni huandaliwa kwa kuzamisha sehemu ya mmea unayotaka kutumia kama dawa kwenye kiasi cha maji yaliyochemka. Baada ya kuzamisha kwenye maji yaliyochemka, maji hayo huchujwa baada ya dakika 15. Dozi ya dawa inayotakiwa kuandaliwa kwa wastani huwa ni gramu 1 kwa kila mililita 10 za maji.

Kuna dawa nyingi asilia zimeshatengenezwa na kufungwa kwenye vifungashio vya karatasi ambapo unaweza kutumia kirahisi kama majani ya chai ya kuchovywa. Dawa kwenye fomu hiyo zitapunguza muda wa kuandaa.

Namna ya kuandaa dikokshen ya dawa asilia

Dikokshen hutumika kuvuna kiini cha dawa ambacho hakiathiriwi na joto.

Ili kuandaa dikokshen ya dawa, chemsha magome au mizizi ya mmea kwa muda wa dakika 15 hadi 60 (hutegemea aina ya mmea au kiini cha dawa), kisha pooza na ongeza maji ya baridi ili kutengeneza kiasi cha dawa na wingi wa kiini unachohitaji.

Endapo dawa inatakiwa kuchemka kwa muda mrefu, unatakiwa ongezea kiasi cha maji yaliyopotea ili dawa isiungue.

Dozi ya dikoksheni ni sawa na infusheni yaani gramu moja ya mmea kwa mililita 10 za maji isipokuwa endapo dawa ina uteute mwingi, gramu moja inatakiwa kuchanganywa na mililita 20 za maji.

 

Namna ya kuandaa mmengenyo wa dawa

 

Kuandaa mmeng’enyo wa dawa kwa njia hii unatakiwa weka dawa yako kwenye chombo kisha ongeza maji yenye joto linalotakiwa, mara nyingi joto linatakiwa kuwa kati ya nyuzi za sentigrade 35 hadi 40 ikitegemea aina ya dawa. Lengo kuu la kuzingatia joto ni kutoharibu kiini cha dawa ambacho kinategemea joto.

Namna ya kuandaa masalesheni ya dawa

 

Ili kuandaa masalesheni ya dawa, saga au katakata dawa kwenye vipande vidodo vidogo sana kisha weka kwenye jaa ya kioo yenye kimiminika cha kufyonza dawa. Funika mchanganyiko na acha kwa muda wa siku tatu au zaidi kwenye joto la ndani ya nyumba.Baada ya kutimia kwa siku tatu, tikisa kwa nguvu mara nyingi ili dawa iingie kwenye kimiminika. Baada ya hapo chuja dawa na kamua unga au vipande ili dawa yote itoke. Baada ya hapo unaweza kuchuja dawa kwa ajili ya matumizi au kuifanyia dekatensheni ili kupata kiini safi cha dawa.

Namna ya kuandaa pakolesheni ya dawa

 

Hii ni njia maarufu ya kuandaa tinkcha ya dawa au kufyonza dawa kutoka kwenye kimiminika.  Njia hii inahitaji chombo maalumu chenye jina la pakoleta na unatakiwa kuwa mtaalamu zaidi kuandaa dawa kwa njia hii. Soma zaidi maelezo kwa kutumia linki chini ya tovuti hii.

 

Namna ya kuandaa dawa ya kufyonza kwa kimiminika

Njia hii huandaa dawa kutoka kwenye kimiminika chenye dawa au tishu za mnyama kwa kufyonzwa dawa hiyo kwa kutumia kimiminika kingine haswa pombe aina ya ehthanol  au maji.

 

Kiasi cha pombe na maji yanayowekwa hutegemea aina ya dawa. Njia hii inahitaji uwe mtaalamu wa kuandaa dawa, unaweza kujifunza zaidi namna ya kuandaa dawa kwa njia hii kupitia linki chini ya tovuti hii au tumia dawa ambazo tayari zimekwisha andaliwa.

Namna ya kuandaa tinkcha ya dawa

 

Tinkcha ya dawa huandaliwa kwa kufanya masalesheni au pakolesheni ya dawa kwa kutumia kimiminika cha pombe tu. Njia hii ni nzuri ya kuvuna kiwango cha kiini unachotaka kutoka kwenye mimea au mnyama. Soma zaidi kuhusu njia hii kupitia rejea chini ya Makala hii.

KUMBUKA:

 

Kama kuna haja ya kuchemsha dawa, hakikisha unatumia chomo kilichotengenezwa na udongo au sufuria za stainless steel na usifunike wakati wa kuchemsha ili kutoa sumu na kutobadili kiini cha dawa.

 

Usitumie dawa zaidi moja na kutibu tatizo moja au mawili tofauti ili kuepuka madhara na mwingiliano

Endapo unatumia dawa za hospitali, wasilina na daktari wako kukushauri ili kuepuka mwingiliano wa dawa na madhara yanayoweza kutokea.

ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute msaada kutoka kwa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala hii

Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na Tiba kupitia kitufe cha 'Pata tiba' au 'Mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

26 Agosti 2021 18:28:10

Rejea za mada hii;

1. Butyrospermum parkii. https://puracy.com/blogs/ingredients/butyrospermum-parkii-0. Imechukuliwa 05.08.2021

2. Butyrospermum Parkii Shea Butter Extract. https://www.tabletwise.net/medicine/butyrospermum-parkii-shea-butter-extract/amp. Imechukuliwa 05.08.2021

3. Butyrospermum Parkii . https://core.ac.uk/download/pdf/234662463.pdf.Imechukuliwa 05.08.2021
Infusion methods. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/infusion/#. Imechukuliwa 27.06.2021

4. Decoction extraction. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/decoction/. Imechukuliwa 27.06.2021

5. Extraction methods digestion. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/digestion/. Imechukuliwa 27.06.2021

6. Fluid extract. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extracts/fluid-extract/. Imechukuliwa 27.06.2021

7. Tincture. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extracts/tincture/. Imechukuliwa 27.06.2021

8. Perolation. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/percolation/. Imechukuliwa 27.06.2021

9. Maceration. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/maceration/. Imechukuliwa 27.06.2021

10. S. Essengue Belibi, et al. The Use of Shea Butter as an Emollient for Eczema. https://www.jacionline.org/article/S0091-6749%2808%2903527-6/fulltext. Imechukuliwa 05.08.2021

bottom of page