top of page

Chenopodium ambrosioides

Imeandikwa na:

Dkt. Benjamin L, MD

4 Agosti 2021 18:57:35

Sifa za Chenopodium ambrosioides

Chenopodium ambrosioides Hufahamika kwa jina jingine la mchaichai wa ki mexico, ni aina yam mea unaostawi mwaka mzima n ahata hivyo pia baadhi ya sehemu hukua katika majira fulani tu ya mwaka.
Hukua na kufikia urefu wa mita 1 na hufunikwa na vinyweleo vyenye harufu nzuri.

Hupatikana sana Afrika magharibi haswa Nigeria, Senegal, Ghana na Cameroon

Uwezo wa Chenopodium ambrosioides kitiba

Uwezo wa Chenopodium ambrosioides ni kutibu maradhi yafuatayo
• Michomo kinga
• Kuvia kwa damu
• Maambukizo ya mapafu
• Kuondoa sumu mwilini kwa kuamsha kuharisha
• Kupunguza maumivu
• Kuua na Kuondoa minyoo mwilini
• Fangasi

Minyoo wanaoweza kuuliwa na Chenopodium ambrosioides

• Minyoo ya uviringo
• Minyoo ndoano

Tahadhari kwa matumizi ya chenopodium ambrosioides

• Huweza kusababisha mzio
• Kwa matumizi ya kuua na kuondoa minyoo, mara baada ya kunywa mafuta inatakiwa kutumia dawa ya kuongeza kuharisha ili kusafisha minyoo waliokufa tumboni.

Matumizi ya Chenopodium ambrosioides

Kwa matibabu ya minyoo

Tengeneza infusheni ya gramu 100 za majani mabichi au vikonyo vinavyobonoa maua kwenye lita moja ya maji kisha kunywa mara tatu kwa siku. Baada ya siku tatu kupita, unahsauriwa kutumia dawa za kuharisha ili kuondoa minyoo ilyokufia kwenye utumbo.

Dozi kwa watoto inatakiwa kuwa nusu ya watu wazima

Maudhi ya chenopodium ambrosioides

Matumizi yanatakiwa kuwa na uchunguzi wa karibu kwa sababu endapo dozi itazidi inaweza kusababisha;
• Kizunguzungu
• Maumivu ya kichwa
• Kutapika

Namna ya kuandaa aina mbalimbali za dawa kutoka kwenye mmea

Namna ya kuandaa infusheni ya dawa asilia

Infusheni huandaliwa kwa kuzamisha sehemu ya mmea unayotaka kutumia kama dawa kwenye kiasi cha maji yaliyochemka. Baada ya kuzamisha kwenye maji yaliyochemka, maji hayo huchujwa baada ya dakika 15. Dozi ya dawa inayotakiwa kuandaliwa kwa wastani huwa ni gramu 1 kwa kila mililita 10 za maji.

Kuna dawa nyingi asilia zimeshatengenezwa na kufungwa kwenye vifungashio vya karatasi ambapo unaweza kutumia kirahisi kama majani ya chai ya kuchovywa. Dawa kwenye fomu hiyo zitapunguza muda wa kuandaa.

Namna ya kuandaa dikokshen ya dawa asilia

Dikokshen hutumika kuvuna kiini cha dawa ambacho hakiathiriwi na joto.

Ili kuandaa dikokshen ya dawa, chemsha magome au mizizi ya mmea kwa muda wa dakika 15 hadi 60 (hutegemea aina ya mmea au kiini cha dawa), kisha pooza na ongeza maji ya baridi ili kutengeneza kiasi cha dawa na wingi wa kiini unachohitaji.

Endapo dawa inatakiwa kuchemka kwa muda mrefu, unatakiwa ongezea kiasi cha maji yaliyopotea ili dawa isiungue.

Dozi ya dikoksheni ni sawa na infusheni yaani gramu moja ya mmea kwa mililita 10 za maji isipokuwa endapo dawa ina uteute mwingi, gramu moja inatakiwa kuchanganywa na mililita 20 za maji.

 

Namna ya kuandaa mmengenyo wa dawa

 

Kuandaa mmeng’enyo wa dawa kwa njia hii unatakiwa weka dawa yako kwenye chombo kisha ongeza maji yenye joto linalotakiwa, mara nyingi joto linatakiwa kuwa kati ya nyuzi za sentigrade 35 hadi 40 ikitegemea aina ya dawa. Lengo kuu la kuzingatia joto ni kutoharibu kiini cha dawa ambacho kinategemea joto.

Namna ya kuandaa masalesheni ya dawa

 

Ili kuandaa masalesheni ya dawa, saga au katakata dawa kwenye vipande vidodo vidogo sana kisha weka kwenye jaa ya kioo yenye kimiminika cha kufyonza dawa. Funika mchanganyiko na acha kwa muda wa siku tatu au zaidi kwenye joto la ndani ya nyumba.Baada ya kutimia kwa siku tatu, tikisa kwa nguvu mara nyingi ili dawa iingie kwenye kimiminika. Baada ya hapo chuja dawa na kamua unga au vipande ili dawa yote itoke. Baada ya hapo unaweza kuchuja dawa kwa ajili ya matumizi au kuifanyia dekatensheni ili kupata kiini safi cha dawa.

Namna ya kuandaa pakolesheni ya dawa

 

Hii ni njia maarufu ya kuandaa tinkcha ya dawa au kufyonza dawa kutoka kwenye kimiminika.  Njia hii inahitaji chombo maalumu chenye jina la pakoleta na unatakiwa kuwa mtaalamu zaidi kuandaa dawa kwa njia hii. Soma zaidi maelezo kwa kutumia linki chini ya tovuti hii.

 

Namna ya kuandaa dawa ya kufyonza kwa kimiminika

Njia hii huandaa dawa kutoka kwenye kimiminika chenye dawa au tishu za mnyama kwa kufyonzwa dawa hiyo kwa kutumia kimiminika kingine haswa pombe aina ya ehthanol  au maji.

 

Kiasi cha pombe na maji yanayowekwa hutegemea aina ya dawa. Njia hii inahitaji uwe mtaalamu wa kuandaa dawa, unaweza kujifunza zaidi namna ya kuandaa dawa kwa njia hii kupitia linki chini ya tovuti hii au tumia dawa ambazo tayari zimekwisha andaliwa.

Namna ya kuandaa tinkcha ya dawa

 

Tinkcha ya dawa huandaliwa kwa kufanya masalesheni au pakolesheni ya dawa kwa kutumia kimiminika cha pombe tu. Njia hii ni nzuri ya kuvuna kiwango cha kiini unachotaka kutoka kwenye mimea au mnyama. Soma zaidi kuhusu njia hii kupitia rejea chini ya Makala hii.

KUMBUKA:

 

Kama kuna haja ya kuchemsha dawa, hakikisha unatumia chomo kilichotengenezwa na udongo au sufuria za stainless steel na usifunike wakati wa kuchemsha ili kutoa sumu na kutobadili kiini cha dawa.

 

Usitumie dawa zaidi moja na kutibu tatizo moja au mawili tofauti ili kuepuka madhara na mwingiliano

Endapo unatumia dawa za hospitali, wasilina na daktari wako kukushauri ili kuepuka mwingiliano wa dawa na madhara yanayoweza kutokea.

ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute msaada kutoka kwa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala hii

Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na Tiba kupitia kitufe cha 'Pata tiba' au 'Mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

4 Agosti 2021 18:57:35

Rejea za mada hii;

1. Chenopodium ambrosioides L. https://www.gbif.org/species/3083836.Imechukuliwa 04.08.2021

2. Victor Kuete, et al.

3. Physical, Hematological, and Histopathological Signs of Toxicity Induced by African Medicinal Plants. https://www.sciencedirect.com/topics/pharmacology-toxicology-and-pharmaceutical-science/chenopodium-ambrosioides. Imechukuliwa 04.08.2021

4. Carlos E. P. Rios, et al. Chenopodium ambrosioides L. Improves Phagocytic Activity and Decreases Bacterial Growth and the Systemic Inflammatory Response in Sepsis Induced by Cecal Ligation and Puncture. https://www.frontiersin.org/articles/10.3389/fmicb.2017.00148/full. Imechukuliwa 04.08.2021

5. Cysne, D N, et al. Antimalarial potential of leaves of Chenopodium ambrosioides L. Parasitol. Res. 115, 4327–4334. doi: 10.1007/s00436-016-5216-x

6. Burkovskiy I, et al. Cytokine release in sepsis. Adv. Biosci. Biotechnol. 4, 860–865. doi: 10.4236/abb.2013.49114

7. Gustavo P. Calado, et al. Chenopodium ambrosioides L. Reduces Synovial Inflammation and Pain in Experimental Osteoarthritis. https://journals.plos.org/plosone/article?id=10.1371/journal.pone.0141886. Imechukuliwa 04.08.2021

8. Infusion methods. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/infusion/#. Imechukuliwa 27.06.2021

9. Decoction extraction. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/decoction/. Imechukuliwa 27.06.2021

10. Extraction methods digestion. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/digestion/. Imechukuliwa 27.06.2021

11. Fluid extract. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extracts/fluid-extract/. Imechukuliwa 27.06.2021

12. Tincture. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extracts/tincture/. Imechukuliwa 27.06.2021

13. Perolation. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/percolation/. Imechukuliwa 27.06.2021

14. Maceration. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/maceration/. Imechukuliwa 27.06.2021

bottom of page