Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dkt. Benjamin l, MD
ULY CLINIC
18 Septemba 2026, 14:24:24


Combretum glutinosum
Combretum glutinosum ni miongoni mwa mimea inayotumika katika tiba asilia kwa matatizo mbalimbali, yakiwemo kupunguza maji mwilini, kushusha shinikizo la juu la damu na kupunguza kikohozi. Tafiti zilizofanyika kuhusu mmea huu zimeonyesha matokeo mbalimbali yanayohusiana na matumizi yake ya tiba.
Combretum glutinosum huwa na misombo mbalimbali ya asili, ikiwemo tindikali za galiki na ellagiki, glikosidi za flavonoidi pamoja na aina mbalimbali za tanini, kama vile 2,3-(S)-hexahydroxydiphenoyl-D-glucose, punicalin, punicalagin na combreglutinin.
Sifa za Combretum glutinosum
Combretum glutinosum una sifa zifuatazo:
Ni mmea wenye umbo la kichaka au mti mdogo unaoweza kufikia urefu wa mita 10.
Huwa na maua ya njano.
Matunda yake huwa na mabawa manne yenye rangi ya njano ambayo hukauka na kubadilika kuwa kahawia.
Uwezo wa Combretum glutinosum kitiba
Combretum glutinosum huuzwa katika baadhi ya nchi za Ulaya na Afrika kama dawa asilia kwa matumizi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na:
Kushusha shinikizo la damu.
Kupunguza maji mwilini.
Kupunguza kikohozi.
Bronkaitisi.
Kupunguza manjano.
Mafua yanayosababishwa na virusi vya influenza.
Baridi yabisi.
Kuongeza nguvu za kiume.
Ugumba kwa wanaume.
Kaswende.
Malaria.
Matumizi ya Combretum glutinosum katika shinikizo la damu
Kwa matumizi ya kupunguza shinikizo la juu la damu na maji mwilini, andaa dawa ya kuchemsha kwa kutumia gramu 30 za majani katika lita moja ya maji.
Baada ya matumizi, pima shinikizo la damu na uzito ili kufuatilia mabadiliko yanayotokea mwilini.
Matumizi ya Combretum glutinosum kwa kikohozi
Kwa kikohozi, andaa dawa ya kuchemsha kwa kutumia gramu 30 za majani katika lita moja ya maji, kisha ongeza kijiko kimoja cha chai cha sukari.
Maudhi ya Combretum glutinosum
Maudhi yanayoweza kusababishwa na Combretum glutinosum hayajafahamika kikamilifu. Hata hivyo, kwa kuwa mmea huu hutumika kushusha shinikizo la damu, matumizi ya kiasi kikubwa yanaweza kusababisha shinikizo la damu kushuka kupita kiasi na kuleta dalili kama:
Kizunguzungu.
Maumivu ya kichwa.
Kupoteza fahamu.
Namna ya kuandaa aina mbalimbali za dawa kutoka kwenye mmea
Namna ya kuandaa infusheni ya dawa asilia
Infusheni huandaliwa kwa kuzamisha sehemu ya mmea unayotaka kutumia kama dawa kwenye kiasi cha maji yaliyochemka. Baada ya kuzamisha kwenye maji yaliyochemka, maji hayo huchujwa baada ya dakika 15. Dozi ya dawa inayotakiwa kuandaliwa kwa wastani huwa ni gramu 1 kwa kila mililita 10 za maji.
Kuna dawa nyingi asilia ambazo tayari zimetengenezwa na kufungwa kwenye vifungashio vya karatasi, ambapo unaweza kuzitumia kwa urahisi kama majani ya chai ya kuchovywa. Dawa zilizo katika fomu hiyo hupunguza muda wa kuandaa.
Namna ya kuandaa dikokshen ya dawa asilia
Dikokshen hutumika kuvuna kiini cha dawa ambacho hakiathiriwi na joto.
Ili kuandaa dikokshen ya dawa, chemsha magome au mizizi ya mmea kwa muda wa dakika 15 hadi 60, kutegemea aina ya mmea au kiini cha dawa. Kisha ipooze na ongeza maji ya baridi ili kutengeneza kiasi cha dawa na wingi wa kiini unaohitaji.
Endapo dawa inatakiwa kuchemshwa kwa muda mrefu, unatakiwa kuongeza kiasi cha maji yaliyopotea ili dawa isiungue.
Dozi ya dikokshen ni sawa na infusheni, yaani gramu 1 ya mmea kwa kila mililita 10 za maji, isipokuwa endapo dawa ina uteute mwingi. Katika hali hiyo, gramu 1 inatakiwa kuchanganywa na mililita 20 za maji.
Namna ya kuandaa mmeng’enyo wa dawa
Kuandaa mmeng’enyo wa dawa kwa njia hii, unatakiwa kuweka dawa yako kwenye chombo kisha kuongeza maji yenye joto linalotakiwa. Mara nyingi joto linatakiwa kuwa kati ya nyuzi 35 hadi 40 za sentigredi, kutegemea aina ya dawa.
Lengo kuu la kuzingatia joto ni kutoharibu kiini cha dawa ambacho kinategemea joto.
Namna ya kuandaa masalesheni ya dawa
Ili kuandaa masalesheni ya dawa, saga au katakata dawa katika vipande vidogo sana, kisha viweke kwenye chombo cha kioo chenye kimiminika cha kufyonza dawa.
Funika mchanganyiko huo na uache kwa muda wa siku tatu au zaidi kwenye joto la ndani ya nyumba. Baada ya kutimia kwa siku tatu, tikisa kwa nguvu mara nyingi ili dawa iingie kwenye kimiminika.
Baada ya hapo, chuja dawa na kamua unga au vipande ili dawa yote itoke. Kisha unaweza kuchuja dawa kwa ajili ya matumizi au kuifanyia dekatensheni ili kupata kiini safi cha dawa.
Namna ya kuandaa pakolesheni ya dawa
Hii ni njia maarufu ya kuandaa tinkcha ya dawa au kufyonza dawa kutoka kwenye kimiminika. Njia hii inahitaji chombo maalumu chenye jina la pakoleta na unatakiwa kuwa mtaalamu zaidi ili kuandaa dawa kwa njia hii.
Soma zaidi kuhusu njia hii kupitia kiungo kilichowekwa chini ya tovuti hii.
Namna ya kuandaa dawa ya kufyonza kwa kimiminika
Njia hii huandaa dawa kutoka kwenye kimiminika chenye dawa au tishu za mnyama kwa kufyonza dawa hiyo kwa kutumia kimiminika kingine, hasa pombe aina ya ethanol au maji.
Kiasi cha pombe na maji kinachowekwa hutegemea aina ya dawa. Njia hii inahitaji uwe mtaalamu wa kuandaa dawa. Unaweza kujifunza zaidi namna ya kuandaa dawa kwa njia hii kupitia kiungo kilichowekwa chini ya tovuti hii au kutumia dawa ambazo tayari zimeandaliwa.
Namna ya kuandaa tinkcha ya dawa
Tinkcha ya dawa huandaliwa kwa kufanya masalesheni au pakolesheni ya dawa kwa kutumia kimiminika cha pombe pekee. Njia hii ni nzuri ya kuvuna kiwango cha kiini unachotaka kutoka kwenye mimea au mnyama.
Soma zaidi kuhusu njia hii kupitia rejea zilizo chini ya makala hii.
KUMBUKA
Kama kuna haja ya kuchemsha dawa, hakikisha unatumia chombo kilichotengenezwa kwa udongo au sufuria za chuma cha pua (stainless steel), na usifunike wakati wa kuchemsha ili kutoa sumu na kutobadili kiini cha dawa.
Usitumie zaidi ya dawa moja kutibu tatizo moja au mawili tofauti ili kuepuka madhara na mwingiliano wa dawa.
Endapo unatumia dawa za hospitali, wasiliana na daktari wako akushauri ili kuepuka mwingiliano wa dawa na madhara yanayoweza kutokea.
Imeandikwa:
4 Agosti 2021, 22:07:14
ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute msaada kutoka kwa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala hii
Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na Tiba kupitia kitufe cha 'Pata tiba' au 'Mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii.
Rejea za mada hii;
https://alchetron.com/Combretum-glutinosum. Imechukuliwa 04.08.2021
Gedson Rodrigues de Morais Lim, et al. Bioactivities of the Genus Combretum (Combretaceae): A Review. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC6268318/. Imechukuliwa 04.08.2021
Alowanou Géorcelin, et al. A review of Bridelia ferruginea, Combretum glutinosum and Mitragina inermis plants used in zootherapeutic remedies in West Africa: historical origins, current uses and implications for conservation. https://www.researchgate.net/figure/Leaves-of-Combretum-glutinosum-Alissou-2013_fig2_282445656. Imechukuliwa 04.08.2021
Alowanou, G.G., et al. In vitro anthelmintic effects of Bridelia ferruginea, Combretum glutinosum, and Mitragyna inermis leaf extracts on Haemonchus contortus, an abomasal nematode of small ruminants. Parasitology research, 118(4), pp.1215-1223.
Infusion methods. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/infusion/#. Imechukuliwa 27.06.2021
Decoction extraction. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/decoction/. Imechukuliwa 27.06.2021
Extraction methods digestion. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/digestion/. Imechukuliwa 27.06.2021
Fluid extract. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extracts/fluid-extract/. Imechukuliwa 27.06.2021
Tincture. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extracts/tincture/. Imechukuliwa 27.06.2021
Perolation. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/percolation/. Imechukuliwa 27.06.2021
Maceration. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/maceration/. Imechukuliwa 27.06.2021

