Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
ULY CLINIC
18 Septemba 2026, 14:24:24


Kigelia Africana
Kigelia africana ni mti unaotajwa katika tiba asilia, hasa katika matibabu ya ugumba. Hupatikana katika maeneo mbalimbali barani Afrika, ikiwemo katika mbuga za wanyama kama Mbuga ya Wanyama ya Manyara nchini Tanzania.
Mti huu pia hutumika katika kukuza matiti kwa mabinti kwa kupaka maandalizi yanayotokana na mmea huo kwenye titi. Matumizi haya yamehusishwa na mwonekano wa matunda yake na kazi inayodaiwa kufanywa na mmea huu katika kukuza titi.
Sifa za mmea Kigelia africana
Kigelia africana ni mti unaoweza kukua na kufikia urefu wa mita 10 hadi 15. Maua yake huwa ya zambarau yenye mistari ya njano.
Matunda yake huwa na umbo linalofanana na soseji, huku miisho yake ikiwa ya mviringo. Ndani ya matunda hayo hupatikana mbegu nyingi.
Uwezo wa Kigelia africana kitiba
Majimaji yanayopatikana baada ya kuchemsha maganda ya tunda lililoiva hutumika kusuguliwa kwenye titi kwa lengo la kufanya titi likue na kuwa kubwa.
Tafiti zinaonyesha kuwa tunda hili lina steroli ambazo mwonekano wake unafanana na homoni zinazohusishwa na ukuaji wa titi.
Matumizi ya Kigelia africana kama dawa
Chemsha maganda ya tunda katika mililita 200 za maji, kisha tumia maji hayo kusugulia kwenye titi asubuhi na jioni.
Majina mengine ya Kigelia africana
Kigelia africana hufahamika kwa majina mengine kama:
Dawa asili ya kukuza titi
Dawa asili ya kukuza matiti
Dawa asili ya kufanya titi likue
Namna ya kuandaa aina mbalimbali za dawa kutoka kwenye mmea
Namna ya kuandaa infusheni ya dawa asilia
Infusheni huandaliwa kwa kuzamisha sehemu ya mmea unayotaka kutumia kama dawa kwenye kiasi cha maji yaliyochemka. Baada ya kuzamisha kwenye maji yaliyochemka, maji hayo huchujwa baada ya dakika 15. Dozi ya dawa inayotakiwa kuandaliwa kwa wastani huwa ni gramu 1 kwa kila mililita 10 za maji.
Kuna dawa nyingi asilia ambazo tayari zimetengenezwa na kufungwa kwenye vifungashio vya karatasi, ambapo unaweza kuzitumia kwa urahisi kama majani ya chai ya kuchovywa. Dawa zilizo katika fomu hiyo hupunguza muda wa kuandaa.
Namna ya kuandaa dikokshen ya dawa asilia
Dikokshen hutumika kuvuna kiini cha dawa ambacho hakiathiriwi na joto.
Ili kuandaa dikokshen ya dawa, chemsha magome au mizizi ya mmea kwa muda wa dakika 15 hadi 60, kutegemea aina ya mmea au kiini cha dawa. Kisha ipooze na ongeza maji ya baridi ili kutengeneza kiasi cha dawa na wingi wa kiini unaohitaji.
Endapo dawa inatakiwa kuchemshwa kwa muda mrefu, unatakiwa kuongeza kiasi cha maji yaliyopotea ili dawa isiungue.
Dozi ya dikokshen ni sawa na infusheni, yaani gramu 1 ya mmea kwa kila mililita 10 za maji, isipokuwa endapo dawa ina uteute mwingi. Katika hali hiyo, gramu 1 inatakiwa kuchanganywa na mililita 20 za maji.
Namna ya kuandaa mmeng’enyo wa dawa
Kuandaa mmeng’enyo wa dawa kwa njia hii, unatakiwa kuweka dawa yako kwenye chombo kisha kuongeza maji yenye joto linalotakiwa. Mara nyingi joto linatakiwa kuwa kati ya nyuzi 35 hadi 40 za sentigredi, kutegemea aina ya dawa.
Lengo kuu la kuzingatia joto ni kutoharibu kiini cha dawa ambacho kinategemea joto.
Namna ya kuandaa masalesheni ya dawa
Ili kuandaa masalesheni ya dawa, saga au katakata dawa katika vipande vidogo sana, kisha viweke kwenye chombo cha kioo chenye kimiminika cha kufyonza dawa.
Funika mchanganyiko huo na uache kwa muda wa siku tatu au zaidi kwenye joto la ndani ya nyumba. Baada ya kutimia kwa siku tatu, tikisa kwa nguvu mara nyingi ili dawa iingie kwenye kimiminika.
Baada ya hapo, chuja dawa na kamua unga au vipande ili dawa yote itoke. Kisha unaweza kuchuja dawa kwa ajili ya matumizi au kuifanyia dekatensheni ili kupata kiini safi cha dawa.
Namna ya kuandaa pakolesheni ya dawa
Hii ni njia maarufu ya kuandaa tinkcha ya dawa au kufyonza dawa kutoka kwenye kimiminika. Njia hii inahitaji chombo maalumu chenye jina la pakoleta na unatakiwa kuwa mtaalamu zaidi ili kuandaa dawa kwa njia hii.
Soma zaidi kuhusu njia hii kupitia kiungo kilichowekwa chini ya tovuti hii.
Namna ya kuandaa dawa ya kufyonza kwa kimiminika
Njia hii huandaa dawa kutoka kwenye kimiminika chenye dawa au tishu za mnyama kwa kufyonza dawa hiyo kwa kutumia kimiminika kingine, hasa pombe aina ya ethanol au maji.
Kiasi cha pombe na maji kinachowekwa hutegemea aina ya dawa. Njia hii inahitaji uwe mtaalamu wa kuandaa dawa. Unaweza kujifunza zaidi namna ya kuandaa dawa kwa njia hii kupitia kiungo kilichowekwa chini ya tovuti hii au kutumia dawa ambazo tayari zimeandaliwa.
Namna ya kuandaa tinkcha ya dawa
Tinkcha ya dawa huandaliwa kwa kufanya masalesheni au pakolesheni ya dawa kwa kutumia kimiminika cha pombe pekee. Njia hii ni nzuri ya kuvuna kiwango cha kiini unachotaka kutoka kwenye mimea au mnyama.
Soma zaidi kuhusu njia hii kupitia rejea zilizo chini ya makala hii.
KUMBUKA
Kama kuna haja ya kuchemsha dawa, hakikisha unatumia chombo kilichotengenezwa kwa udongo au sufuria za chuma cha pua (stainless steel), na usifunike wakati wa kuchemsha ili kutoa sumu na kutobadili kiini cha dawa.
Usitumie zaidi ya dawa moja kutibu tatizo moja au mawili tofauti ili kuepuka madhara na mwingiliano wa dawa.
Endapo unatumia dawa za hospitali, wasiliana na daktari wako akushauri ili kuepuka mwingiliano wa dawa na madhara yanayoweza kutokea.
Imeandikwa:
28 Juni 2021, 22:33:47
ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute msaada kutoka kwa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala hii
Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na Tiba kupitia kitufe cha 'Pata tiba' au 'Mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii.
Rejea za mada hii;
Infusion methods. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/infusion/#. Imechukuliwa 27.06.2021
Decoction extraction. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/decoction/. Imechukuliwa 27.06.2021
Extraction methods digestion. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/digestion/. Imechukuliwa 27.06.2021
Fluid extract. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extracts/fluid-extract/. Imechukuliwa 27.06.2021
Tincture. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extracts/tincture/. Imechukuliwa 27.06.2021
Perolation. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/percolation/. Imechukuliwa 27.06.2021
Maceration. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/maceration/. Imechukuliwa 27.06.2021

