top of page

Tamarindus indica

Imeandikwa na:

Dkt. Benjamin L, MD

1 Agosti 2021 19:07:00

Utangulizi

Tamarindus Indica ukifahamika kama mkwaju ni mmea unaopatikana sehemu nyingi duniani. Hutumika kama dawa asili ya kutibu haja ngumu, vidonda na harara kwenye ngozi, vidonda vya tumbo, baridi yabisi, pumu, kukosa hedhi n.k.

Sifa za mmea Tamarindus Indica

Mti wa ukwaju unaweza kustawi na kufikia urefu wa mita 30, matawi yake husambaa na kuufanya uwe na mwonekano wa taji. Majani yake huwa madogo na hutengeneza mwonekano kama wa nyonya

Tamarindus Indica huzalisha matunda yenye jina la ukwaju ambayo hutumika kama chakula katika maeneo ya ukanda wa tropiki.

Licha ya kutumika kama chakula, mti huu huwa na faida nyingi kwenye tiba asilia

Tamarindus Indica husatawi dana maeneo ya ukanda wa joto. Asili yake licha ya kutofahamika hufikiriwa kuwa ni Afrika licha ya kupatikana sehemu nyingi sana duniani toka enzi.

Uwezo wa Tamarindus Indica katika tiba

Magome, mizizi, majani, maua na tunda la mkwaju huwa na uwezo wa kutibu;
• Tetekuwanga kwa watoto
• Aleji ya macho
• Maambukizi ya virusi kwenye koo
• Homa
• Kikohozi
• Minyoo ya tumbo
• Vidonda kwenye ngozi
• Hararakwenye ngozi
• Baridi yabisi
• Vidonda vya tumbo
• Haja ngumu
• Kukosa haja kubwa
• Kukojoa kitandani kwa watoto
• Tindikali nyingi tumboni
• Homa ya kuhara damu

Matumizi ya Tamarindus Indica kama tiba

Matumizi ya juisi ya majani madogo na maua iliyochuchwa hutumika kutibu aleji ya macho

Dikoksheni ya majani iliyotiwa sukari kidogo hutumika kutibu maambukizi kwenye koo, homa, kikohozi na minyoo wa tumbo

Majani machanga yaliyosagwa na kuwekwa kwenye ngozi au maungio huwa na uwezo wa kutibu maumivu ya baridi yabisi, kupunguza michomo kinga kwenye vidonda, kupunguza uvimbe na maumivu

Dikoksheni ya majani hutumika kutibu matatizo ya mwatoto kukojoa kitandani na matatizo ya mfumo wa mkojo

Matumizi mengine ya Tamarindus Indica

Juisi ya ukwaju hutumika kama dawa ya kulainisha haja ngumu au kukosa haja kubwa (konstipesheni)

Juisi ya ukwaju pia huwa na uwezo wa kuweka tumbo na viungo vya umeng’enyaji wa chakula kwenye hali nzuri na pia kutibu maambukizi ya virusi kwenye mfumo wa juu wa hewa na kikohozi

Maganda ya tunda kama ayakiliwa hutumika kutibu homa na kuthibiti uzalishaji wa tindikali ndani ya tumbo

Unga wa mbegu za ukwaju hutumika kutibu kuhara damu pamoja na kuharisha

Majani yake huwa na uwezo wa kutibu kuondoa sumu kwenye ini kutokana na radiko za oksijeni na huwa miongoni mwa virutubisho vizuri kwa wagonjwa wa kisukari na moyo

Namna ya kutumia Tamarindus Indica kama tiba ya haja ngumu

Twanga tunda baada ya kuondoa mbegu zake kisha loweka kwenye maji. Tumia maji yake baada ya nusu saa kila siku asubuhi wakati tumbo lako halina kitu.

Je unaweza kuweka sukari?

Unaweza kuongeza sukari kidogo, hata hivyo kama unaweza kunywa bila sukari ni vema


Tahadhari;

Kwa wenye vidonda vya tumbo wanaweza kupata dalili kali kama wakitumia juisi ya ukwaju, hivyo ni vema ukawasiliana na daktari kwa ushauri.

Namna ya kuandaa aina mbalimbali za dawa kutoka kwenye mmea

​

Namna ya kuandaa infusheni ya dawa asilia

​

Infusheni huandaliwa kwa kuzamisha sehemu ya mmea unayotaka kutumia kama dawa kwenye kiasi cha maji yaliyochemka. Baada ya kuzamisha kwenye maji yaliyochemka, maji hayo huchujwa baada ya dakika 15. Dozi ya dawa inayotakiwa kuandaliwa kwa wastani huwa ni gramu 1 kwa kila mililita 10 za maji.

​

Kuna dawa nyingi asilia zimeshatengenezwa na kufungwa kwenye vifungashio vya karatasi ambapo unaweza kutumia kirahisi kama majani ya chai ya kuchovywa. Dawa kwenye fomu hiyo zitapunguza muda wa kuandaa.

​

Namna ya kuandaa dikokshen ya dawa asilia

​

Dikokshen hutumika kuvuna kiini cha dawa ambacho hakiathiriwi na joto.

​

Ili kuandaa dikokshen ya dawa, chemsha magome au mizizi ya mmea kwa muda wa dakika 15 hadi 60 (hutegemea aina ya mmea au kiini cha dawa), kisha pooza na ongeza maji ya baridi ili kutengeneza kiasi cha dawa na wingi wa kiini unachohitaji.

​

Endapo dawa inatakiwa kuchemka kwa muda mrefu, unatakiwa ongezea kiasi cha maji yaliyopotea ili dawa isiungue.

​

Dozi ya dikoksheni ni sawa na infusheni yaani gramu moja ya mmea kwa mililita 10 za maji isipokuwa endapo dawa ina uteute mwingi, gramu moja inatakiwa kuchanganywa na mililita 20 za maji.

 

Namna ya kuandaa mmengenyo wa dawa

 

Kuandaa mmeng’enyo wa dawa kwa njia hii unatakiwa weka dawa yako kwenye chombo kisha ongeza maji yenye joto linalotakiwa, mara nyingi joto linatakiwa kuwa kati ya nyuzi za sentigrade 35 hadi 40 ikitegemea aina ya dawa. Lengo kuu la kuzingatia joto ni kutoharibu kiini cha dawa ambacho kinategemea joto.

​

Namna ya kuandaa masalesheni ya dawa

 

Ili kuandaa masalesheni ya dawa, saga au katakata dawa kwenye vipande vidodo vidogo sana kisha weka kwenye jaa ya kioo yenye kimiminika cha kufyonza dawa. Funika mchanganyiko na acha kwa muda wa siku tatu au zaidi kwenye joto la ndani ya nyumba.Baada ya kutimia kwa siku tatu, tikisa kwa nguvu mara nyingi ili dawa iingie kwenye kimiminika. Baada ya hapo chuja dawa na kamua unga au vipande ili dawa yote itoke. Baada ya hapo unaweza kuchuja dawa kwa ajili ya matumizi au kuifanyia dekatensheni ili kupata kiini safi cha dawa.

​

Namna ya kuandaa pakolesheni ya dawa

 

Hii ni njia maarufu ya kuandaa tinkcha ya dawa au kufyonza dawa kutoka kwenye kimiminika.  Njia hii inahitaji chombo maalumu chenye jina la pakoleta na unatakiwa kuwa mtaalamu zaidi kuandaa dawa kwa njia hii. Soma zaidi maelezo kwa kutumia linki chini ya tovuti hii.

 

Namna ya kuandaa dawa ya kufyonza kwa kimiminika

​

Njia hii huandaa dawa kutoka kwenye kimiminika chenye dawa au tishu za mnyama kwa kufyonzwa dawa hiyo kwa kutumia kimiminika kingine haswa pombe aina ya ehthanol  au maji.

 

Kiasi cha pombe na maji yanayowekwa hutegemea aina ya dawa. Njia hii inahitaji uwe mtaalamu wa kuandaa dawa, unaweza kujifunza zaidi namna ya kuandaa dawa kwa njia hii kupitia linki chini ya tovuti hii au tumia dawa ambazo tayari zimekwisha andaliwa.

​

Namna ya kuandaa tinkcha ya dawa

 

Tinkcha ya dawa huandaliwa kwa kufanya masalesheni au pakolesheni ya dawa kwa kutumia kimiminika cha pombe tu. Njia hii ni nzuri ya kuvuna kiwango cha kiini unachotaka kutoka kwenye mimea au mnyama. Soma zaidi kuhusu njia hii kupitia rejea chini ya Makala hii.

​​

KUMBUKA:

 

Kama kuna haja ya kuchemsha dawa, hakikisha unatumia chomo kilichotengenezwa na udongo au sufuria za stainless steel na usifunike wakati wa kuchemsha ili kutoa sumu na kutobadili kiini cha dawa.

 

Usitumie dawa zaidi moja na kutibu tatizo moja au mawili tofauti ili kuepuka madhara na mwingiliano

​

Endapo unatumia dawa za hospitali, wasilina na daktari wako kukushauri ili kuepuka mwingiliano wa dawa na madhara yanayoweza kutokea.

ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute msaada kutoka kwa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala hii

Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na Tiba kupitia kitufe cha 'Pata tiba' au 'Mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

1 Agosti 2021 19:07:00

Rejea za mada hii;

bottom of page