Vitex agnus-castus
Imeandikwa na:
Dkt. Benjamin L, MD
6 Agosti 2021, 13:13:33


Utangulizi
Vitex agnus-castus ni mmea poli unaotumika kama tiba asili ya maumivu ya titi na kuondoa dalili tangulizi za hedhi.
Uwezo wa Vitex agnus-castus kitiba
Vitex agnus-castus hutumika kama dawa asili ya matatizo mbalimbali yanayohusiana na mzunguko wa hedhi kama vile kutibu;
• Maumivu ya titi
• Dalili tangulizi za hedhi
• Dalili kali za hedhi
Namna Vitex agnus-castus unavyofanya kazi
Vitex agnus-castus hufanya kazi kwa kuingilia kazi za homon za uzazi wa mwanamke.
Matumizi ya Vitex agnus-castus kitiba
Hutumika katika tiba ya maumivu ya titi wakati wa hedhi
• Kutibu dalili kali kabla ya kuingia hedhi kama vile maumivu ya titi, maumivu ukishika chuchu, hulka ya chini au kutokuwa na hulka nzuri, hasira, kukasilika haraka, maumivu ya kichwa.
Baadhi ya tafiti pia zimeonuyesha huwa na uwezo mdogo wa
• Kuzuia mimba
• Kuua mbu
• Kuondoa dalili za hedhi
• Kupunguza damu nyingi ya hedhi
• Dalili kali za hedhi
• Chunuzi
• Hofu
• Kukosa usingizi
Maudhi ya Vitex agnus-castus
Vitex agnus-castus ni salama kwa watu wengi kama ikitumika kwa kunywa hata hivyo endapo itatumika kwa muda mrefu huweza kusababisha;
• Kichefuchefu
• Mvurugiko wat umbo
• Harara
• Maumivu ya kichwa
• Chunusi
• Kushindwa kulala
• Kuongezeka uzito
• Mabadiliko ya mzunguko wa hedhi
Watumiaji wanaopaswa kuchukua tahadhali wakati wa kutumia vitex agnus-castus na dawa zenye mwingiliano
Watumiaji wanaopaswa kuchukua tahadhali wakati wa kutumia vitex agnus-castus
• Tahadhali inapaswa kuchukuliwa kwa wajawazito, ikiwezekana isitumike kwa mjamzito kwa sababu hakuna taarifa zinazohusu usalama wake
• Kwa kuwa Vitex agnus-castus hudhuru kiwango cha homon estrogen kwenye damu, tahadhali ichukuliwe kwa wenye magonjwa ya homon mfano, wenye faibroidi, saratani ya titi, kizazi na ovari.
• Usitumie Vitex agnus-castus kama mwili wako una mwitikio mkali kwenye homon zingine.
• Kama unatumia dawa za kutibu Parkinson disease, Schizophrenia au magonjwa mengine ya akili, unapaswa kufahamu kuwa zinazweza kuwa na mwingiliano na Vitex agnus-castus kwa kuwa hudhuru pia homon na kemikali ndani ya ubongo.
Dawa zinazoingiliana na Vitex agnus-castus
• Dawa za uzazi wa mpango
• Homon estrogen
• Chlorpromazine (Thorazine),
• Clozapine (Clozaril),
• Fluphenazine (Prolixin),
• Haloperidol (Haldol),
• Olanzapine (Zyprexa),
• Perphenazine (Trilafon),
• Prochlorperazine (Compazine),
• Quetiapine (Seroquel),
• Risperidone (risperdal),
• Thioridazine (mellaril)
• Thiothixene (navane)
• Bromocriptine (parlodel)
• Levodopa (dopar)
• Pramipexole (mirapex)
• Ropinirole (requip)
• Metoclopramide (Reglan)
Namna ya kutumia Vitex Agnus-Castus
Kwa maumivu ya titi
Kunywa miligramu 3.2 hadi 4.5 ya kiini cha dawa kutoka kwenye matunda yaliyokaushwa kila siku kwa muda wa miezi miwili
Au
Kunywa miligramu 40 za kiini cha dawa kutoka kwenye matunda yeke kila siku kwa muda wa miezi 3
Kwa matibabu ya dalili awali za hedhi
Kunywa miligramu 8 hadi 40 za kiini cha dawa ya vitex agnus-castus kila siku kwenye mizungoko 2 hadi 3 ya hedhi
Namna ya kuandaa aina mbalimbali za dawa kutoka kwenye mmea
Namna ya kuandaa infusheni ya dawa asilia
Infusheni huandaliwa kwa kuzamisha sehemu ya mmea unayotaka kutumia kama dawa kwenye kiasi cha maji yaliyochemka. Baada ya kuzamisha kwenye maji yaliyochemka, maji hayo huchujwa baada ya dakika 15. Dozi ya dawa inayotakiwa kuandaliwa kwa wastani huwa ni gramu 1 kwa kila mililita 10 za maji.
Kuna dawa nyingi asilia zimeshatengenezwa na kufungwa kwenye vifungashio vya karatasi ambapo unaweza kutumia kirahisi kama majani ya chai ya kuchovywa. Dawa kwenye fomu hiyo zitapunguza muda wa kuandaa.
Namna ya kuandaa dikokshen ya dawa asilia
Dikokshen hutumika kuvuna kiini cha dawa ambacho hakiathiriwi na joto.
Ili kuandaa dikokshen ya dawa, chemsha magome au mizizi ya mmea kwa muda wa dakika 15 hadi 60 (hutegemea aina ya mmea au kiini cha dawa), kisha pooza na ongeza maji ya baridi ili kutengeneza kiasi cha dawa na wingi wa kiini unachohitaji.
Endapo dawa inatakiwa kuchemka kwa muda mrefu, unatakiwa ongezea kiasi cha maji yaliyopotea ili dawa isiungue.
Dozi ya dikoksheni ni sawa na infusheni yaani gramu moja ya mmea kwa mililita 10 za maji isipokuwa endapo dawa ina uteute mwingi, gramu moja inatakiwa kuchanganywa na mililita 20 za maji.
Namna ya kuandaa mmengenyo wa dawa
Kuandaa mmeng’enyo wa dawa kwa njia hii unatakiwa weka dawa yako kwenye chombo kisha ongeza maji yenye joto linalotakiwa, mara nyingi joto linatakiwa kuwa kati ya nyuzi za sentigrade 35 hadi 40 ikitegemea aina ya dawa. Lengo kuu la kuzingatia joto ni kutoharibu kiini cha dawa ambacho kinategemea joto.
Namna ya kuandaa masalesheni ya dawa
Ili kuandaa masalesheni ya dawa, saga au katakata dawa kwenye vipande vidodo vidogo sana kisha weka kwenye jaa ya kioo yenye kimiminika cha kufyonza dawa. Funika mchanganyiko na acha kwa muda wa siku tatu au zaidi kwenye joto la ndani ya nyumba.Baada ya kutimia kwa siku tatu, tikisa kwa nguvu mara nyingi ili dawa iingie kwenye kimiminika. Baada ya hapo chuja dawa na kamua unga au vipande ili dawa yote itoke. Baada ya hapo unaweza kuchuja dawa kwa ajili ya matumizi au kuifanyia dekatensheni ili kupata kiini safi cha dawa.
Namna ya kuandaa pakolesheni ya dawa
Hii ni njia maarufu ya kuandaa tinkcha ya dawa au kufyonza dawa kutoka kwenye kimiminika. Njia hii inahitaji chombo maalumu chenye jina la pakoleta na unatakiwa kuwa mtaalamu zaidi kuandaa dawa kwa njia hii. Soma zaidi maelezo kwa kutumia linki chini ya tovuti hii.
Namna ya kuandaa dawa ya kufyonza kwa kimiminika
Njia hii huandaa dawa kutoka kwenye kimiminika chenye dawa au tishu za mnyama kwa kufyonzwa dawa hiyo kwa kutumia kimiminika kingine haswa pombe aina ya ehthanol au maji.
Kiasi cha pombe na maji yanayowekwa hutegemea aina ya dawa. Njia hii inahitaji uwe mtaalamu wa kuandaa dawa, unaweza kujifunza zaidi namna ya kuandaa dawa kwa njia hii kupitia linki chini ya tovuti hii au tumia dawa ambazo tayari zimekwisha andaliwa.
Namna ya kuandaa tinkcha ya dawa
Tinkcha ya dawa huandaliwa kwa kufanya masalesheni au pakolesheni ya dawa kwa kutumia kimiminika cha pombe tu. Njia hii ni nzuri ya kuvuna kiwango cha kiini unachotaka kutoka kwenye mimea au mnyama. Soma zaidi kuhusu njia hii kupitia rejea chini ya Makala hii.
KUMBUKA:
Kama kuna haja ya kuchemsha dawa, hakikisha unatumia chomo kilichotengenezwa na udongo au sufuria za stainless steel na usifunike wakati wa kuchemsha ili kutoa sumu na kutobadili kiini cha dawa.
Usitumie dawa zaidi moja na kutibu tatizo moja au mawili tofauti ili kuepuka madhara na mwingiliano
Endapo unatumia dawa za hospitali, wasilina na daktari wako kukushauri ili kuepuka mwingiliano wa dawa na madhara yanayoweza kutokea.
ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute msaada kutoka kwa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala hii
Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na Tiba kupitia kitufe cha 'Pata tiba' au 'Mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
26 Agosti 2021, 18:23:06
Rejea za mada hii;
Turner S and Mills S. A double-blind clinical trial on a herbal remedy for premenstrual syndrome: a case study. Complementary Therapies in Medicine 1993;1(2):73-77
Sliutz G, et al. Agnus castus extracts inhibit prolactin secretion of rat pituitary cells. Horm.Metab Res 1993;25(5):253-255.
Singleton G. Premenstrual disorders in adolescent females-- integrative management. Aust.Fam.Physician 2007;36(8):629-630.
Schwalbe E. [Treatment of mastodynia]. ZFA.(Stuttgart.) 8-10-1979;55(22):1239-1242.
Schellenberg R, Schrader E, and Brattström A. Vitex agnus castus extrakt Ze440 bei pramenstruellem syndrom: ergebnisse einer RCT im vergleich mit plazebo bei 170 patientinnen.
Roth OA. Zur therapie der gelbkörperinsuffizienz in der praxis. Med Klin 1956;51:1263-1265.
Propping D. Vitex agnus-castus: treatment of gynecological syndromes. [in German]. Therapeutikon 1991;5:581-585.
Propping D, et al. Diagnostik und therapie der gelbkorperschwache in der praxis. Therapiewoche 1988;38:2992-3001.
Probst V and Roth OA. On a plant extract with a hormone-like effects. Deutsch Medizin Zeitschrift 1954;35:1271-1274.
Prilepskaya V. N, et al. Vitex agnus castus: Successful treatment of moderate to severe premenstrual syndrome. Maturitas 2006;55(Suppl 1):S55-63.
Peters-Welte C , et al. [Menstrual abnormalities and PMS. Vitex agnus-castus in a study of application]. Therapiewoche Gynakologie 1994;7(1):49-52.
Pepeljnjak S, et al. Antibacterial and antifungal activities of the Vitex agnus-castus L. extracts. Acta Pharmaceutica Zagreb 1996;46(3):201-206.
Pearlstein T. Psychotropic medications and other non-hormonal treatments for premenstrual disorders. Menopause.Int 2012;18(2):60-64.
Opitz G. et al. [Conservative treatment of mastopathy with Mastodynon]. Ther Ggw. 1980;119(7):804-809.
Newton K. et al. The Herbal Alternatives for Menopause (HALT) Study: background and study design. Maturitas 10-16-2005;52(2):134-146.
Mishurova SS. Essential oil in Vitex agnus astus L., its component composition and antimicrobial activity. Rastitel 'nye Resursy 1986;22(4):526-530.
Meyl C. Therapie des prämenstruellen syndroms. Vergleich einer kombinierten behandlung von mastodynon und vitamin E mit der vitamin E-monotherapie. Therapeutikon 1991;5(10):518-525.
Mergner R. Zyklusstörungen: therapie mit einem vitex-agnus-castus-haltigen kombinationsarzneimittel. Der Kassenarzt 1992;7:51-60.
Mazaro-Costa R, et al. Medicinal plants as alternative treatments for female sexual dysfunction: utopian vision or possible treatment in climacteric women? J.Sex Med. 2010;7(11):3695-3714.
Mancho P, et al. Chaste tree for premenstrual syndrome. An evolving therapy in the United States. Adv.Nurse Pract. 2005;13(5):43-4, 46.
Ma L, et al. Treatment of moderate to severe premenstrual syndrome with Vitex agnus castus (BNO 1095) in Chinese women. Gynecol.Endocrinol. 2010;26(8):612-616.
Ma L, et al. Evaluating therapeutic effect in symptoms of moderate-to-severe premenstrual syndrome with Vitex agnus castus (BNO 1095) in Chinese women. Aust.N.Z.J Obstet.Gynaecol. 2010;50(2):189-193.
Lucks B, et al. Vitexagnus-castus essential oil and menopausal balance: a self-care survey. Complement Ther Nurs.Midwifery 2002;8(3):148-154.
Liebel H. Behandlung des prämenstruellen Syndromes. Agnus castus-haltige Kombinationsarzneimittel im Test. Therapiewoche Gynakol 1992;5:2-12.
Lauritzen C, et al. Treatment of premenstrual tension syndrome with Vitex agnus castus controlled, double-blind study versus pyridoxine. Phytomedicine. 1997;4(3):183-189.
Laakmann E, et al. Efficacy of Cimicifuga racemosa, Hypericum perforatum and Agnus castus in the treatment of climacteric complaints: a systematic review. Gynecol.Endocrinol. 2012;28(9):703-709.
Kubista, E., Muller, G., and Spona, J. [Treatment of mastopathies with cyclic mastodynia. Clinical results and hormonal profiles]. Rev Fr.Gynecol Obstet 1987;82(4):221-227. View abstract.
Kayser HW and Istanbulluoglu S. Vitex agnus castus. Hippokrates 1954;25:717-719.
Jarry H, et al. Evidence for Estrogen Receptor beta-Selective Activity of Vitex agnus-castus and Isolated Flavones. Planta Med 2003;69(10):945-947.
Jarry H Leonhardt S, et al. [Agnus castus as a dopaminergic active constituent in Mastodynon N]. Zeitschrift fur Phytotherapie 1991;12:77-82.
He Z, et al. Treatment for premenstrual syndrome with Vitex agnus castus: A prospective, randomized, multi-center placebo controlled study in China. Maturitas 5-20-2009;63(1):99-103.
Halaska M, et al. Treatment of cyclical mastodynia using an extract of Vitex agnus castus: results of a double-blind comparison with a placebo. Ceska.Gynekol. 1998;63(5):388-392.
Gregl A. Klinik und therapie der mastodynie. Med Welt 1985;36:242-246.
Göbel R. Results of the clinical evaluations of Danazol in benign breast disease compared with local treatment, gestagens, and bromocriptine. In: Baum M, George WD, and Hughes LE. Benign Breast Diseases. London: Roy Soc Med Int;1985.
Fugh-Berman A, et al. Complementary and alternative medicine (CAM) in reproductive-age women: a review of randomized controlled trials. Reprod Toxicol. 2003;17(2):137-152.
Freeman E. W. Therapeutic management of premenstrual syndrome. Expert.Opin.Pharmacother. 2010;11(17):2879-2889.
Fournier D, et al. Behandlung der mastopathie, mastodynie und des prämenstruellen syndroms. Verleich medikamentöser behandlung zu unbehandelten kontrollen. Therapiewoche 1987;37(5):430-434.
Fikentscher, H. [Aetiology, diagnosis und therapy of mastopathy and mastodynia. Experiences of treatment with mastodynon (author's transl)]. Med Klin 8-26-1977;72(34):1327-1330.
Fersizoglou NE. Hormonale und thermographische veränderungen unter konservativer therapie der mastophathie. Vergleich von danazol, tamoxifen, lisurid, lynesterenol und einem phytopharmakon. Dissertation 1989;
Feldmann HU, et al. The treatment of corpus Luteum insufficiency and premenstrual syndrome. Experience in a multicenter study under clinical practice conditions. [in German]. Gyne 1990;11(12):421-425.
Dugoua J. J, et al. Safety and efficacy of chastetree (Vitex agnus-castus) during pregnancy and lactation. Can.J Clin Pharmacol. 2008;15(1):e74-e79.
Doll M. The premenstrual syndrome: effectiveness of Vitex agnus castus. Med.Monatsschr.Pharm. 2009;32(5):186-191.
Dittmar FW. Premenstrual syndrome: treatment with a phytopharmaceutical [in German]. TW Gynakologie 1992;5(1):60-68.
Dennehy C, et al. The use of herbs and dietary supplements in gynecology: an evidence-based review. J Midwifery Womens Health 2006;51(6):402-409.
Dante G, et al. Herbal treatments for alleviating premenstrual symptoms: a systematic review. J Psychosom.Obstet.Gynaecol. 2011;32(1):42-51.
Coeugniet E. Premenstrual syndrome and its treatment. Arztezeitchr Naturheilverf 1986;27:619-622.
Ciotta L, et al. Psychic aspects of the premenstrual dysphoric disorders. New therapeutic strategies: our experience with Vitex agnus castus. Minerva Ginecol. 2011;63(3):237-245.
Bleier W. Therapie von Zyklus- und Blutungsstorungen und weiteren endokrin bedingten Erkrankungen der Frau mit pflanzlichen Wirkstoffen. Zbl Gynakol 1959;81:701-709.
Infusion methods. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/infusion/#. Imechukuliwa 27.06.2021
Decoction extraction. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/decoction/. Imechukuliwa 27.06.2021
Extraction methods digestion. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/digestion/. Imechukuliwa 27.06.2021
Fluid extract. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extracts/fluid-extract/. Imechukuliwa 27.06.2021
Tincture. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extracts/tincture/. Imechukuliwa 27.06.2021
Percolation. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/percolation/. Imechukuliwa 27.06.2021
Maceration. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/maceration/. Imechukuliwa 27.06.2021