top of page
Mwandishi:
Dkt. Sospeter B, MD
Mhariri:
Dkt. Salome A, MD

Dawa za Kuongeza uchavushaji wa mayai

10 Julai 2023 11:40:15
Image-empty-state.png

Zipo dawa ina mbalimbali za kuongeza uchavushaji wa mayai kwa mwanamke na kumfanya apate mimba kwa haraka na wakati mwingine kusababisha mimba ya Watoto Zaidi ya mmoja. Sehemu hii imezungumzia kuhusu dawa jamii ya Choriogonatrophin alpha.

Dawa hizi nyingi zipo kwenye kundi la dawa zinazoitwa Gonadotrophin, yapo majina ya aina tofauti ya dawa hizo kutokana na kiwanda kinachozalisha lakini kazi yake ni moja.

 

Namna ya dawa zinavyofanya kazi

Dawa jamii hii huongeza uzalishaji wa homoni ya Folicle stimulating Homoni (FSH) .Kazi ya  FSH ni kuamsha uchavushaji wa yai kutoka kwenye kiwanda cha kuzalisha mayai kwa mwanamke(ovari), dawa hii hufanya kazi kwa wanawake wale tu ambao ovari zao hazina matatizo ya awali bali kutokana na Matatizo mengine mwilini basi mayai yanashindwa kuzalishwa.

Dawa hizi zikitumiwa na wanaume huweza kuongeza uzalishaji wa mbegu kiume(manii) na pia ufanyaji kazi wake huwanza kuanzia mienzi mitatu hadi 18. Dawa hizi hutumika kwa kuchomwa sindano chini ya ngozi ya tumbo

 

Matumizi
 • Kuamsha uzalishaji wa mayai kwa mwanamke.

 • Kuamsha uzalishaji wa manii(mbegu za kiume)

 

Maudhi ya dawa yanayoweza kutokea ni pamoja na;

Asilimia 1 hadi 10 ya watu wanaotumia dawa hupata

 • Kupata vifuko vya maji kwenye kiwanda cha mayai

 • Kuamsha kwa kasi uzalishaji wa mayai kwenye kiwanda cha mayai

 • Maumivu ya tumbo

 • Kutapika

 • Miunguzo sehemu ya kuchomea sindano

Watu chini ya asilimia 1 hupata
 • Maumivu ya titi

 • Jeraha kwenye shingo ya kizazi

 • Kukojoa protini ya albumin kwenye damu

 • Maumivu ya mgongo

 • Mapigo ya moyo kutokwenda sawa

 • Kizunguzungu

 • Kubadilika kwa hali ya mtu

 • Virusi vya herpes kwenye sehemu za siri

 • Kupanda kwa sukari kwenye damu

 • Kuwashwa

 • Maambukizi ya UTI

 • Kutokwa na damu ukeni

 • Michomo asilia kwenye uke

Dalili zngine ambazo haifahamiki ni watu kiasi gani wanapata huwa pamoja na
 • Maumivu ya kichwa

 • Kuwa mkali

 • Msongo wa mawazo

 • Mwili kuvia maji

 • Kuwa mchovu

 • Matiti kukua kwa wanaume

 • Ujana mzuri

 • Mwili kuchoka sana

 • Kuganda kwa damu kwenye mishipa ya artery

 • Kupasuka kwa vifuko vya maji vya ovary

 

Mfano wa dawa huwa pamoja na 
 • Urofollitrophin

 • chorigonatrophin alpha

 • fertinorm HP

 • Gona-f

 • Menopur 

 • Menotropins

 • Novareal

 • Ovidrel

 • Pregny

 • Repronex

Dawa zingine

Dawa zingine ni jamii ya Selective  Estrogen receptor modulator ambazo ni;

 • Bazedoxifene/conjugated estrogens, 

 • Clomid, clomiphene,

 • Duavee

 • Evista

 • Ospemifene

 • Osphena

 • Raloxifene

 • Serophene

 • Tamoxifen


Majina mengine

Dawa za kuongeza uzalishaji wa mayai hujulikana pia kama

 • Dawa za kutibu ugumba kwa wanawake

 • Dawa za kutibu ugumba kwa wanaume

 • Dawa za kuongeza uzalishaji manii

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
11 Julai 2023 08:54:43
1.BNF 78 , toleo la september 2019
2. DC Dutta's Textbook of Gynecology: Including Contaception (6th Ed)
3. Williams gynecology 4th edition
bottom of page