Ugonjwa na dawa
Kurasa hii utajifunza kuhusu dawa na ugonjwa unaotibiwa na dawa hiyo. Wasiliana na daktari wako kabla ya kutumia dawa yoyotee ile ili kuepuka madhara na usugu wa dawa mwilini mwako. Kumbuka siku zote kuwa dawa ni sumu kwenye mwili wako endapo haitatumika bila ushauri wa daktari

Dawa ya miguu kuwaka moto
Miguu kuwaka moto katika Makala hii inajumuisha pia tatizo la kanyagio kuwaka moto, ambalo huelezewa kuwa ni hisia za joto, kuchomachoma kwa miguu, au kanyagio. Hali hii huweza kutokea wakati wa usiku au wakati wote haswa kwa watu wa makamo lakini haimaanishi kuwa haiwezi kutokea kwa watu walio na umri mdogo. Makala hii imezungumzia kuhusu dawa za tatizo la miguu kuwaka moto, kusoma zaidi kuhusu tatizo la miguu kuwaka moto, dalili na uchunguzi, nenda kwenye makala nyingine ndani ya tovuti ya ulyclinic.