top of page

Rudi nyuma

​

Imeandikwa na daktari wa ULY-clinic

​

Ugonjwa wa seliak

​

Ugonjwa wa seliak ni ugonjwa wa autoimyun unaoambatana na michomo sugu kwenye utumbo mwembamba. Ugonjwa huu hutokana na protini ya gluteni inayopatikana kwenye chakula aina ya ngano, shayiri iliyosagwa na mikate ya shayiri. Gluteni huamsha kinga za mwili kwenye utumbo mwembamba ambazo husababisha kupungua kwa ufyonzaji wa chakula na kuleta tatizo la kushidwa kufyonzwa kwa chakula.

​

Madhumuni ya matibabu

​

Matibabu ya ugonjwa wa siliak yanalenga kuondoa dalili za uharisha, tumbo kujaa gesi na maumivu ya tumbo na kupunguza hatari ya madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na mal-abzopsheni.

​

Matibabu yasiyo dawa

​

Matibabu ya  msingi ya ugonjwa wa siliak ni kuzingatia mlo wako kwa kuepuka kula vyakula vyenye protini ya gluteni ambavyo ni vyakula vya ngano na shayiri na bidhaa zote zenye ngano au shayiri.

​

Vyakula ambavyo havina protini ya gluteni vinauzwa madukani unaweza kuvinunua. Unaweza kuwasiliana na mtaalamu wa lishe kwa maelezo Zaidi

​

Wasilaina na mtaalamu lishe wa ulyclinic kwa kubonyeza hapa au namba za simu chini ya tovuti hii.

 

Matibabu dawa

​

Watu wenye ugonjwa wa seliak wanapata tatizo la mal-abzopshni ambalo huleta tatizo la kupungukiwa kwa madini na vitamini (Madini ya kalisiamu na vitamin D). Kukosa kwa vitamini na madini haya huwa kihatarishi cha kuwa na mifupa isiyo imara (osteoporosisi) na dhaifu. Tiba ya ugonjwa wa seliak inataiwa kuzingatia madhara haya.

​

Wagonjwa wa seliak hawatakiwi kutumia dawa za vitamini na madini kalisiamu kwa kununua wenyewe madukani. Mgonjwa anatakiwa kushauriana na mtaalamu wa afya kuhusu mahitaji ya dawa hizi na kudhibiti madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na dawa hizi.

​

Wagonjwa ambao wana seliak ya kujirudia rudia wanatakiwa kutbiwa na madaktari wabonezi wa ugonjwa huu katika vituo vya tiba bobezi. Matibabu ya dawa ya predinisolone  yanaweza kutumiwa mwanzo wa tiba wakati mgonjwa anasubiria matibabu ya daktarin bobezi.

 

Dawa zinazotumika kutibu ugonjwa wa seliak ni;

​

​

Bofya hapa kwa Rejea za mada hii

​

Imeboreshwa 09.06.2021

bottom of page