top of page

Imeandikwa na daktari wa ULY CLINIC

​

Dawa za kutibu UTI

​

UTI kwa asilimia zaidi ya 80 husababishwa na maambukizi ya bakteria ingawa kwa baadhi ya wagonjwa haswa wale wenye UKIMWI, kisukari, wenye matatizo ya maumbile ya mfumo wa mkojo na wanaotumia dawa za kushusha kinga za mwili huweza kupata UTI inayotokana na maambukizi ya fangasi, virusi na vimelea.

 

Mgonjwa wa UTI anaweza kuwa na UTI iliyosababishwa na bakteria aina moja au zaidi ya moja. Maambukizi hayo hutibiwa kwa kutumia dawa za kuua bakeria husika zenye jina la antibayotiki.

 

Dawa zilizooroswshwa hapa chini zinatibu maambukizi ya bakteria. Dawa nyingi za kutibu UTI isiyo sugu dozi yake inatakiwa kutumia kuanzia siku 3 hadi 7. Na ile iliyo sugu inaweza kutibiwa kwa muda wa siku saba hadi siku 14.

 

Uchaguzi wa wewe utumie dawa ipi hutegemea mambo mengi kama vile, aina ya bakteria au fangasi anayesababisha, hali ya mgonjwa na aina ya UTI

 

​

Kumbuka: Wasiliana na daktari wako siku zote kabla ya kuanza tiba

​​

Bonyeza dawa kusoma zaidi;

​

​

UTI isiyo kali kwa wanawake dawa zinazotumika ni;

​

​

Unaamuaje kuchagua kutumia dawa aina fulani kwa ajili ya kutibu UTI?

​

Uchaguzi wa dawa ya kutibu UTI hutegemea mambo yafuatayo;

​

  • Dawa inayofanya kazi kwenye eneo unaloishi- kuna baadhi ya dawa zinofahamika kutibu UTI na kwa sasa hazitibu kutokana na bakteria wanaosababisha UTI kutosikia dawa hizo(kuwa sugu) hivyo dawa itayochaguliwa kutumia ni ile tu ambayo inaweza kuua bakteria wanaosababisha UTI.

  • Dawa aina ya amoxclav,cefdinir, cefaclor, cefpodoxime-proxetil zinaweza kutumia endapo dawa zinazotakiwa kutumika hapaswi kutumia kulingana na hali ya mgonjwa.

  • Dawa ya Fosfomycin na nitrofurantoin inatakiwa kuepukwa kutumika kwa mgonjwa mwenye maambukizi ya awali ya UTI iliyo kwenye mfumo wa juu wa mkojo(figo)

  • Dawa aina ya (TMP-SMX)inaweza kuzuiwa kutumika ili kuandoa usugu wa bakteria kwenye dawa

  • Dawa za jamii ya fluoroquinolones zitumike kwa UTI sugu tu

​

ULY CLINIC inakushauri usitumie dawa yoyote ile kabla ya kuwasiliana na daktari wako

​

Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kubonyeza pata tiba au kutumia namba za simu chini ya tovuti yetu.

​

Imeboreshwa, 06.11.2020

​

Rejea

​

  1. ULY CLINIC. Dalili za UTI kwa watu wazima. https://www.ulyclinic.com/dalili-za-ugonjwa/Dalili-za-UTI-kwa-watu-wazima. Imechukuliwa 06.11.2020

  2. MSD manual. Fungal urinary tract infection. https://www.msdmanuals.com/professional/genitourinary-disorders/urinary-tract-infections-utis/fungal-urinary-tract-infections#. Imechukuliwa 06.11.2020

  3. MSD manual. Introduction to UTI. https://www.msdmanuals.com/professional/genitourinary-disorders/urinary-tract-infections-utis/introduction-to-urinary-tract-infections-utis.Imechukuliwa 06.11.2020

bottom of page