Dawa Za Kutibu Fangasi Wa kanyagio na maeneo katikati ya vidole vya miguu- Tinea pedis
​
Maambukizi haya ya Tinea pedis yanaathiri maeneo ya viganja vya miguu na katikati ya vidole vya miguu, ni maambukizi yaliyoathiri binadamu kwa kipindi kirefu kabla ya kugunduliwa mwaka 1908 kwa mara ya kwanza. Fangasi anayesababisha maambukizi haya hufahamika kama Trichophyton rubrum wanaopatikana sana maeneo ya mashariki mwa bala la Ulaya na sehemu za Afrika na bala la Australia. Matumizi ya viatu vya kufunika, vita, kuongezeka kwa njia za kusafiri, kutembea kwenye makundi kumeonekana kuongeza wingi wa ugonjwa huu.
​
Dawa zinazotumika kutibu ugonjwa huu ni pamoja na;
​
-
Dawa ya kupaka ya clotrimazole
-
Dawa ya kupaka ya Econazole
-
Dawa ya kupaka ya Ketoconazole
-
Dawa ya kupaka ya Miconazole
-
Dawa ya kupaka ya Oxiconazole 1%
-
Dawa ya kupaka ya Sertaconazole
-
Luliconazole
-
Ciclopirox
-
Naftifine
-
Terbinafine
-
Butenafine
-
Itraconazole
-
Fluconazole
-
Dawa ya kupaka ya Aluminum lactate
-
Dawa ya kupaka ya Urea
​
Kumbuka kuwasiliana na daktari wako kabla ya kutumia dawa yoyote ile ili akuchunguze na ukupa dawa inayoendana na mahitaji ya mwili wako.
​
Imeboreswhwa 12.02.2020
