Imeandikwa na daktari wa ulyclinic
Dawa za kutibu kuharisha
​
Kuharisha hutokana na kutofyonzwa vema kwa maji maji na virutubisho kwenye mfumo wa chakula, hii hutokana na kutofanyika vema kwa kazi hiyo ya ufyonzaji kwenye maeneo ya utumbo mwembamba na utumbo mpana.
​
Ili mgonjwa aweze kuitwaanaharisha ni lazima awe na dalili ya kupitisha kinyesi chenye maji mara tatu (3) au Zaidi kwa siku, chini ya hapo mtu anahesabika amepata choo kilaini tu.
​
Kuharisha huweza kusababishwa na maambukizi ya bakteria , vimelea, fungasi, au virusi. Ni vema kupata uchunguzi wa daktarin kabla ya kutumia dawa.
​
Dawa za kuondoa/kusimamisha dalili ya kuharisha haishauriwi sana kutumia maana ni hatari, dawa za kutibu tatizo linaloleta kuharisha zimeorodheshwa hapa chini;
-
Cefixime
-
Ceftriaxone
-
Cefotaxime
-
Furazolidone
-
Iodoquinol
-
Paromomycin
-
Quinacrine
-
Vancomycin
-
Nitazoxanide
-
Rifaximin
Chanjo ya kuharisha (Rotarix) kutokana na kirusi cha rotavirusi pia hutolewa hospitali
Ikumbukwe matibabu ya kuharisha kwa Watoto na watu wazima endapo tatizo sio kubwa yanaweza kuanza kwa kumpatia mtoto maji yenye ORS (Oral rehydrating solution) maji haya huwa na madini pamoja na sukari. Matumizi ya maji haya hurejesha madini na sukari iliyopotea wakati wa kuahrisha. Endapo mtoto hatapata maji haya basi anaweza kuishiwa nguvu na kisha kulegea na kushindwa kula.
​
Endapo mtoto au mtu mzima anapata dalili hizi ni vema usisubiri au kumtibu nyumbani mwenyewe bali onana na mtaalamu wa afya haraka Zaidi.
​
-
Mtoto mwenye umri chini ya miezi mitatu
-
Uzito chini ya kilo 8
-
Mwenye historia ya kuzaliwa njiti, anayetumia dawa muda mrefu, au mwenye kuugua ugonjwa mwingine pamoja pia
-
Homa Zaidi ya nyuzi joto za Celsius 38
-
Damu kwenye kinyesi
-
Kutapika kusikoisha
-
Kuharisha sana na kwa wingi wa kinyesi
-
Dalili za kuishiwa maji mwilini kama vile macho kuzama ndani, kupungua kwa machozi, kukauka kwa midomo(lips) na kupungua kwa mkojo
-
Kubadilika kwa ufahamu
-
Kutoacha kuharisha licha ya kutumia ORS
​
Kwa maelezo zaidi soma kuhusu mada ya kuharisha kwa watoto.
​
Unakumbushwa na ULY CLINIC kwamba wasiliana na daktari wako kwa ushauri na uchunguzi kabla ya kuanza matibabu yoyote yale.
​
​
​
Imeboreshwa 24.06.2020
