Imeandikwa na daktari wa ulyclinic
Dawa za kutibu kichefuchefu na kutapika
​
Kichefuchefu na kutapika kunaweza sababishwa na Matatizo mbalimbali ndani ya mwili yanayoweza kuwa ya hatari au yasiyo ya hatari. Endapo mtu ana kichefuchefu na kutapika, kitiba huashiria kuna shida fulani inaendelea ndani ya mwili inayosababisha dalili hizi (mfano maambukizi ndani ya mfumo wa chakula-minyoo, amoeba, kipindupindu,homa ya matumbo-typhoid, maambukizi kwenye mfumo wa fahamu n.k), kutafuta ushauri wa daktari ni lazima kabla ya kutumia dawa yoyote ya kuzuia kichefuchefu na kutapika. Wakati mwingine kutapika ni bora kuliko kuzuia kutapika kwa sababu huondoa tatizo ndani ya mwili,mfano mtu amekunywa sumu au ana maambukizi ndani ya tumbo ambapo mwilikwa asili yake unataka kuyatoa nje ya tumbo kwa njia ya kutapika. Lakini pia kutapika kupita kiasi kunaweza kusababisha mtu kuishiwa nguvu na kulegea, figo kuferi ghafla, mapigo ya moyo kutokueleweka na hata kifo hii ni kwa sababu kupoteza madini muhimu na maji mwilini.
​
Dawa zinazoweza kuzuia kutapika ni pamoja na;
-
Promethazine (phenergan)
-
Prochlorperazine(compazine)
-
Metoclopramide(reglan)
-
Diphenhydramine
​
Dawa zilizoorodheshwa hapa chini hukinga mtu asitapike au kupata kichefuchefu na kutapika;
​
-
Ondasetron
-
Promethazine
-
Prochlorperazine
-
Prochlorperazine
-
Cyproheptadine
-
Diphenhydramine
-
Amitriptyline
-
Propanol
-
Phenobarbital
-
Topiramate
-
Zonisamide
-
Sumatriptan
-
Lorazepam
​
Wasiliana na daktari kwa ushauri na tiba kabla ya kutumia dawa yoyote ile.
​
Imeboreshwa 12.02.2020
