Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
23 Aprili 2020 08:07:55
Acetohexamide
Acetohexamide ni dawa kwenye kundi la sulphonylurea inayotumika kutibu ugonjwa wa kisukari aina ya pili.
Majina ya kibiashara
Dimelin
Dymelor
Gamadiabet
Fomula ya kikemikali
C15H20N2O4S
Jina la kitiba
3-(4-acetylbenzenesulfonyl)-1-cyclohexylurea.
Muonekano wa acetohexamide ni upi?
Kidone cheupe, haina harufu.
Dozi inayopatikana
Hupatikana kama kidonge cha miligramu 500
Sababu za kutumia
Ugonjwa sukari ya juu isiyo tibika kwa insulini ikiwa mlo na mazoezi havitoshi kurekebisha kiwango cha sukari.
Inafanyaje kazi mwilini?
Inashusha kiwango cha sukari kwenye damu kwa:-
Kuchochea seli za kongosho kuazalisha homoni ya insulini.
Inasaidia mwili kuweza kutumia insulini inayozalishwa.
Insulin inayozalishwa hufanya kazi
Huingia kwenye damu kwa njia gani?
Acetahexamide humezwa kwakua hufyonzwa upesi kutoka kwenye mfumo wa chakula kuingia kwenye damu.
Umetaboli wa dawa kwenye ini
Acetohexamide huvunjiwa kwenye ini na kutoa kemikali hydroxyhexamide ambayo ndiyo haswa hufanya kazi ya kushusha sukari.
Utoaji wa taka za dawa
Takamwili za mabaki ya acetohexamide hutolewa kwa njia ya mkojo.
Muda wa ufanyaji kazi
Kiwango kwenye damu hufikia kilele baada ya saa 3. Hufanya kazi mwilini kwa saa 12-24.
Hufaa zaidi kwa wagonjwa wapi?
Wenye mzio na dawa ya insulin
Wagonjwa wa gauti (Ndiyo sulfonylurea pekee inayo ongeza kasi ya mwili kutoa tindkali kutokana urea (yuriki asidi) hivyo kupunguza athari za gauti.
Wenye Uono hafifu
Wagojwa walio katika hatari ya sukari kushuka zaidi mwilini kwa kutumia dawa ya insulin
Tahadhari
Isitumike kwa mgonjwa mwenye
Matatizo kwanye mfumo wa damu mfano saratani ya damu na upungufu wa damu.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia
Kisukari aina ya kwanza
Kisukari cha ujauzito
Ini linaloshindwa kufanya kazi
Figo inayoshindwa kufanya kazi
Wagonjwa wa sukari waliopata shida ya maambukizi makali, upasuaji mkubwa, au asidosisi
Muingiliano na dawa nyingine
Dawa zifuatazo zinaongeza atari ya kushuka kwa sukari zikituiwa na acetohexamide;
Sulfonamides,
Propranolol
Salicylates
Phenylbutazone
Probenecid
Dicumarol
Chloramphenicol
Monoamine oxidase inhibita
Kutumia pamoja na captopril na enalapril ambazo hutibu shikizo la juu la damu hakuna madhara.
Matumizi wakati wa kunyonyesha
Inaweza kushusha sukari ya mtoto anaenyonya na hivyo ni hatari kwa mtoto. Hivyo daktari anaweza kuibadili. Fuatilia kama mtoto anaenyonya ataonesha dalili za sukari kushuka kama vile kuchoka, kushindwa kunyonya,kushindwa kula, degedege, joto la mwili kushuka, kiwango cha sukari kwenye damu ya mtoto.
Epuka
Kutumia na pombe
Maudhi madogo madogo
Kichefuchefu
Kutapika kuharisha
Maumivu ya kichwa
Tumbo kujaa
Kiungulia
Athari kwenye ngozi kama vipele, kuwashwa
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021 11:51:07
Rejea za mada hii:-