top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Dkt. Sospeter M, MD

Dkt. Lugonda B, MD

Imeboreshwa:

26 Februari 2026, 06:12:21

Dawa Amoxyclav

Dawa Amoxyclav

Amoxyclav ni dawa ya antibayotiki yenye mchanganyiko wa Amoxicillin na Clavunic acid, dawa hi hujulikana kwa jina jingine la amoxiclav, aphaclav. Hutumika kutibu maambukizi mbalimbali ya Bakteria kwa binadamu Dawa hii hufanya kazi kwa kuzuia ukuaji na utengenezaji ukuta wa nje wa bakteria hivyo kuzuia kuzaliwa kwa bakteria wapya. Amoxclav imekuwa ikitumika kama dawa nzuri ya kutibu maambukizi kwenye njia ya hewa, sikio la kati, sainas, ngozi na njia ya mkojo.


Fomu ya na uzito wa dawa Amoxyclav

Dawa hii hupatikana katika fomu ya kidonge na kimiminika Kutokana na kupatika kwenye fomu ya kidonge na kimiminika huweza kutumiwa na Watoto pamoja na watu wazima. Amoxclavu huwa na mchanganyiko wa miligramu 500 amoxicillin na miligramu 125 za clavulanic acid Vidonge vya kunywa huwa na uzito mbalimbali kwa kila miligramu 125 za clavulanic asidi mfano

  • 228.5/125

  • 250/125

  • 500/125

  • 875/125 Dawa ya kunywa huwa na uzito mbalimbali wa kiini cha dawa cha amoxcillin na clavulanic aside.

Unaweza tumia Amoxyclav na chakula?


Amoxyclav hufyonzwa vizuri inapotumika pamoja na chakula, hivyo Unashauri kutumika pamoja na chakula jinsi utakavyoshauriwa na daktari wako.


Maudhi ya Amoxyclav

  • Mzio

  • Homa

  • Kuhara

  • Maumivu ya maungio ya mwili

  • Manjano

  • Kutokwa na damu kirahisi au kuumia kirahisi

  • Kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi

  • Kubadilika rangi kwa meno

  • Kichefuchefu na kutapika

  • Kubadilika radha ya chakula

  • Degedege

  • Maumivu wakati wa kujamiana

  • Kuvimba uso, lipsi, kope, ulimi, mikono na miguu

  • Choo kuwa cheusi kama rami

  • Maumivu ya misuli na jointi

  • Kusinzia sinzia

  • Mapigo ya moyo kwenda vibaya


Amoxyclav hutibu nini?

Amoxyclav hutumika kutibu maambukizi ya bakteria kwenye;

  • Mfumo wa kati wa sikio

  • Pua au sinusaitis

  • Mfumo wa chini juu wa upumuaji

  • Ngozi

  • Tonses na falinksi

  • Mfumo wa chini wa upumuaji

  • Tumbo ( Vidonda vya tumbo vinavyosababishwa na H. pyroli)

  • Nutropenia iliyosababishw ana homa homa

  • Mfumo wa mkojo


Magonjwa yanayotibiwa na amoxyclav

Amoxyclav huwa na uwezo wa kutibu magonjwa yaliyosababishwa na bakteria kama;

  • Otaitis ya mfumo wa kati wa sikio

  • Sinusaitis

  • Nimoni

  • Jipu kwenye ngozi

  • Tonses na falinjaitis

  • Vidonda vya tumbo vinavyosababishwa na H. pyroli

  • Nutropenia iliyosababishwa na homa homa

  • UTI


Dawa zenye mwingiliano na Amoxyclav

Amoxiclav huwa na mwingiliano na dawa zifuatazo:

  • Chanjo ya BCG kwa watoto

  • Doxycycline

  • Tetracycline

  • Methotrexate

  • Chloramphenicol

  • Clarithromycin

  • Warfarin

  • Vitamin K

  • Allopurinol

  • Anticoagulants

  • Dawa za uzazi wa mpango

  • Methotrexate

  • Probenecid


Dawa zisizopaswa kutumika na amoxyclav

Usitumie dawa hizi kwani huwa namwingiliano mkali wa amoxyclav

  • Pexidartinib

  • Pretomanid


Wakati wa kuchukua tahadhari kwa mtumiaji wa amoxyclav

  • Wagonjwa wenye mzio na dawa kundi la cephalosporins au carbapenems

  • Wagonjwa wenye utendaji kazi wa figo <30 mL/dakika

  • Hatari ya maambukizi makali ya bakteria mbalimbali

  • Kuota harara wakati wamatumizi


Wagongwa wasiopaswa kutumia Amoxyclav

  • Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao:

  • Wagonjwa wenye aleji na Penicillin

  • Wagonjwa wenye shida ya ini ambao ishawahi sababishwa na Amoxcillin au Clavunic acid


Amoxyclav itumike kwa tahadhari kwa wagonjwa wapi?

Dawa hii inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wafuatao:

  • Wenye aleji na Cephalosporins

  • Historia ya kuwa na manjano ya kukaa kutokana na matumizi ya amoxiclav

  • Kama akiharisha zaidi ya Amoxcillin ikitumika yenyewe

  • Wagonjwa wenye shida ya ini

  • Dawa hii haipaswi kutumika kwa watu ambao hawana Maambukizi ya bakteria ili kuepusha dawa kuishiwa nguvu na vimelea kuwa sugu.


Matumizi ya Amoxyclav Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha

Amoxyclavu haipaswi kutumika kwa mama mjamzito isipokuwa endapo faida za matumizi zinazidi madhara yanayoweza kujitokeza. Fuata maelekezo ya daktarin wako kabla ya kutumia dawa hii. Soma kuhusu matumizi ya amoxyclav kwa mama mjamzito na anayenyonyesha kwenye mada za 'Ushauri wa dawa kipindi cha ujauzito na kunyonyesha' ndani ya tovuti hii.


Je amoxyclav inatumika kwa mama anyenyonyesha?

Soma kuhusu matumizi ya amoxyclav kwa mama mjamzito na anayenyonyesha kwenye mada za 'Ushauri wa dawa kipindi cha ujauzito na kunyonyesha' ndani ya tovuti hii.


Je endapo utasahau dozi yako ya Amoxyclav ufanyaje ?

Endapo umesahau kutumia dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka, isipokuwa endapo muda wa dozi nyingine umeshafika unatakiwa kuruka dozi uliyosahau na kuendelea kama ulivyopangiwa na daktari wako.


Maswali yaliyoulizwa mara kwa mara na majibu yake kuhusu Amoxyclav

1. Je, Amoxyclav ni dawa ya kwanza kuchaguliwa kwa maambukizi ya bakteria?

Si kila wakati. Ingawa Amoxyclav ina wigo mpana, madaktari huchagua dawa kulingana na aina ya bakteria, ukali wa maambukizi, historia ya mgonjwa ya mzio, na matokeo ya kipimo cha kuotesha vimelea na kuangalia mwitikio wae kwenye dawa. Wakati mwingine dawa nyembamba-wigo hupendekezwa ili kuepuka usugu wa bakteria.

2. Kwa nini baadhi ya wagonjwa hupata maumivu ya tumbo wanapotumia Amoxyclav?

Baadhi ya watu huwa na utumbo unaoathirika kirahisi na mabadiliko ya bakteria wa tumboni. Amoxyclav inaweza kubadilisha uwiano wa bakteria rafiki na kusababisha maumivu ya tumbo au hisia ya kutosaga vizuri chakula. Mara nyingi hali hii hupungua baada ya kukamilisha dozi.

3. Je, Amoxyclav inaweza kuathiri matokeo ya vipimo vya maabara?

Ndiyo, baadhi ya vipimo kama vipimo vya sukari kwenye mkojo, vipimo vya ini, na hesabu ya chembe za damu vinaweza kuonekana tofauti wakati mtu anatumia antibiotics. Ni muhimu kumfahamisha daktari au maabara kuhusu matumizi ya dawa kabla ya vipimo.

4. Ni kwa nini watu wengine hupata hisia ya uchovu au kizunguzungu wakitumia Amoxyclav?

Hii hutokana na mwitikio wa mwili unapopambana na maambukizi pamoja na athari ndogo za dawa zinazoweza kuathiri mfumo wa neva. Kwa kawaida ni hali ya muda na hupungua kadri afya inavyorejea.

5. Je, Amoxyclav inaweza kuathiri uwezo wa kinga ya mwili?

Hasa haiudhuru mfumo wa kinga moja kwa moja, lakini kwa baadhi ya watu husababisha mabadiliko madogo ya muda katika bakteria wa kawaida kwenye mwili, jambo linaloweza kufanya mwili kuhisi dhaifu kwa kipindi kifupi wakati wa matibabu.

6. Kwa nini baadhi ya watu hupata fangasi ukeni au mdomoni baada ya kutumia Amoxyclav?

Amoxyclav huua bakteria wabaya na wakati mwingine pia hupunguza kwa muda idadi ya bakteria wazuri wanaodhibiti fangasi. Hii inaweza kusababisha ukuaji wa fangasi kama Candida kwa watu wanaohisiwa kuwa na hatari zaidi.

7. Je, Amoxyclav inaweza kuleta usugu wa bakteria kwenye dawa ikiwa inatumiwa mara kwa mara?

Ndiyo, matumizi ya mara kwa mara bila uangalizi wa daktari yanaweza kuchochea bakteria kujenga kinga dhidi ya dawa, hali inayofanya matibabu kuwa magumu baadaye. Hii ndiyo sababu Amoxyclav haitumiki bila ushahidi wa maambukizi ya bakteria.

8. Kwa nini baadhi ya wagonjwa hupata upele mwilini baada ya kuanza Amoxyclav?

Upele unaweza kuwa ishara ya mzio, mwitikio wa kinga kwa maambukizi, au athari ya kinga ya mwili yenyewe. Upele wa mzio wa kweli mara nyingi huambatana na kuwashwa au kuvimba, na unahitaji tathmini ya daktari.

9. Je, kuna vyakula au vinywaji vinavyoweza kupunguza ufanisi wa Amoxyclav?

Hakuna chakula kinachojulikana kupunguza nguvu ya dawa, lakini ulaji wa vyakula vizito vya mafuta unaweza kuchelewesha ufyonzwaji kwa baadhi ya watu. Kunywa maji ya kutosha na kula chakula chenye mizani husaidia kupunguza madhara ya tumbo.

10. Ni kwa nini baadhi ya watu huhisi ladha ya chuma au mdomo kuwa mkavu wakitumia Amoxyclav?


Hii ni athari ndogo ya dawa kwenye tezi za mate na mabadiliko ya muda ya bakteria wa mdomoni. Si hatari na mara nyingi hupotea ndani ya siku chache baada ya kukamilisha dozi.

11. Je, Amoxyclav inaweza kusababisha muwasho ukeni kila unapoitumia?

Ndiyo, kwa baadhi ya watumiaji Amoxyclav inaweza kusababisha muwasho ukeni, na hii mara nyingi hutokana na kubadilika kwa uwiano wa bakteria na fangasi kwenye uke. Antibayotiki huua bakteria “wakazi” wanaolinda mazingira ya uke, na hivyo kuruhusu fangasi kama Candida albicans kuongezeka kupita kiasi. Mabadiliko haya yanaweza kusababisha:

  • Muwasho ukeni

  • Kuwaka au hisia za kuungua ukeni

  • Kuchomachoma

  • Hisia ya kuwashwa kwenye uke na mlango wa uke

  • Maumivu wakati wa kukojoa

  • Kukauka kwa uke

  • Uchafu mweupe mzito kama maziwa mgando


Hata hivyo, si kila mtu atapata tatizo hili, na mara nyingi hali hutokea kwa wanaotumia antibayotiki mara kwa mara au kwa muda mrefu.


Nini cha kufanya:

  • Mjulishe daktari wako kama muwasho hurudia kila unapoitumia Amoxyclav; huenda ukahitaji dawa kinga dhidi ya fangasi wakati wa matibabu.

  • Epuka kujitibu mwenyewe bila ushauri wa mtaalamu, kwa sababu muwasho unaweza kusababishwa na mambo mengine pia kama maambukizi ya bakteria au mzio.

  • Tumia Amoxyclav tu inapohitajika na ilivyoelekezwa ili kupunguza uwezekano wa athari hizi.


ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeandikwa:

6 Aprili 2020, 17:34:25

Rejea za mada hii:-

bottom of page