top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

3 Mei 2020 14:26:14

Benazepril

Benazepril

Benazepril ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyopo kwenye kundi la dawa linaloitwa angiotensini konventing enzaimu inhibita -ACEIs. Dawa hii iliyo maarufu kwa jina la lalotensin huwa na rangi ya pinki, njano na nyeupe lakini mara nyingi hutegemea aina ya kiwanda kinachotengeneza.


Matumizi na chakula


Benazepril inaweza kutumiwa pamoja na au pasipo chakula kama utakavyoelekezwa na Daktari


Kumbukakunywa dawa hii kama ulivyoshauriwa na daktari wako kila siku na kwa kiwango cha dozi uliyopewa . Kupunguza madhara ya mauzi ya dawa hii Daktari atakuanzishia dozi ndogo na kuiongeza kadri ambavyo mwili wako utakavyoitikia dawa .Baada ya wiki mbili au zaidi tangu ulipoanza kutumia dawa hii shinikizo la damu litashuka na kuwa kawaida


Benazepril hupatikana katika mfumo wa kidonge chenye uzito wa milligram zifuatazo;


 • 5mg

 • 10mg

 • 20mg

 • 40mg


Ufanyaji kazi


Dawa jamii ya ACEIs ikiwa pamoja na Benazepril hufanya kazi zifuatazo ili kupunguza shinikizo la damu;


Huongeza kipenyo cha mishipa ya damu ya vena na ateri kwa kupinga utengenezaji wa homoni ya angiotensini II na uvunjwaji wa Bradykinin.


Kuogezeka kwa kipenyo cha mishipa husababisha kushuka kwa shinikizo ndani ya mishipa na hivyo kupunguza mzigo wa damu unaoingia na kutoka kwenye moyo na kupunguza moyo kufanya kazi kupita kiasi


Hupinga kazi za homoni ya angiotensini II kwenye mishipa ya fahamu ya simpathetiki


Huongeza uwezo wa figo kupoteza madini ya sodiamu na maji kwa njia ya mkojo kwa kuzuia uzalishwaji wa homoni ya aldosterone inayochochewa kuzalishwa zaidi na homoni ya angiotensin II. Homoni ya aldosterone kazi yake ni kutunza maji na madini hayo mwilini


Huzuia kuharibika kwa kuta za moyo na mishipa ya damu kutokana na shinikizo la damu ,kuferi kwa moyo na infaksheni ya mayokadia


Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja (Kundi la ACEIs) na dawa hii ni;


 • Quinapril

 • Enalapril

 • Fosinopril

 • Lisinopril

 • Lisinopril

 • Captopril

 • Moexipril

 • Perindopril

 • Ramipril


Kazi ya dawa


 • Hutumika kwenye matibabu ya wagonjwa wenye shinikizo la damu la juu

 • Hutumika kwa wagonjwa wa wenye Nephropathi ambayo isiyosababishwa na kisukari.


Wakati wa kutumika kwa umakini


Mgonjwa mwenye shida ya figo kama kiasi cha Creatinine kinachotolewa ni chini ya mililita 30 kwa dakika anapaswa kuanza na dozi ya mg 5 hapo awali na isizidi mg 40 kwa siku


Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi hili la (ACEIs)


 • Ni chaguo zuri kwa wagonjwa wenye mafuta kwa wingi mwilini

 • Husaidia kutokudhurika kwa figo kwa mgonjwa wa kisukari

 • Hupunguza hatari ya kupata Kiharusi na Nephropathi


Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;

 • Aspirin

 • Azilsartan

 • Candesartan

 • Celecoxib

 • Choline magnesium trisalicylate

 • Dalteparin

 • Diclofenac

 • Diflunisal

 • Eprosartan

 • Etodolac

 • Fenoprofen

 • Flurbiprofen

 • Ibuprofen

 • Idomethacin

 • Irbesartan

 • Ketorolac

 • Lofexidine

 • Losartan

 • Meclofenamate

 • Mefenamic acid

 • Meloxicam

 • Nabumetone

 • Naproxen

 • Olmesartan

 • Oxaprozin

 • Piroxicam


Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao;

Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au dawa jamii ya ACEIs


Dawa hii inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wafuatao


 • Wagonjwa wenye anyuria (figo Kutozalisha mkojo)

 • Huweza kupelekea Haipotension endapo itachanganywa na Diuretics

 • Huweza kuongeza kiasi cha Bradykinin


Matumizi kwa mama mjamzito


Kwa mama mjamzito inapaswa kutumika kwa katika hali ya dharura endapo hakuna dawa nyingine salama kipindi hiki


Inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa mama anayenyonyesha kwa sababu huingia kwenye maziwa ya mama


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa


Maudhi ya Benazepril


 • Kizunguzungu

 • Kukohoa

 • Kuchoka

 • Kichefuchefu

 • Vipele

 • Kuongezeka kwa Creatinine

 • Kifua kuuma

 • Angioedema


Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?


Endapo ukisahau kunywa dozi yako kunywa mara pale utakapokumbuka na endapo muda wa dozi nyingine umekaribia acha dozi uliyoisahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

3 Novemba 2021 11:50:10

Rejea za mada hii:-

1.Modern pharmacology with Clinical applications written by Charles R. Craig and Robert E. Stitizel ISBN 978-0316159340 ukurasawa 213

2.WebMd.Benazepril.https://www.webmd.com/drugs/2/drug-4682/benazepril-oral/details. Imechukuliwa 23/4/2020

3.Medicinenet.Benazepril.https://www.medicinenet.com/benazepril/article.htm .Imechukuliwa 23/4/2020

4.MedScape.Benazepril.https://reference.medscape.com/drug/lotensin-benazepril-342327.Imechukuliwa 23/4/2020
bottom of page