Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
27 Mei 2020 05:54:18
Carvedilol
Carvedilol ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyoko katika kundi la dawa linaloitwa beta bloka. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Coreg.
Rangi ya Carvedilol
Rangi yake huwa nyeupe au maziwa, hata hivyo rangi ya dawa mara nyingi hutegemea aina ya kiwanda
Carvedilol hupatikana katika mfumo wa kidonge chenye uzito wa miligramu,
3.125mg
6.25mg
12.5mg
25mg
Carvedilol hupatikana katika mfumo wa tembe chenye uzito wa,
10mg
20mg
40mg
80mg
Namna dawa inavyofanya kazi kupunguza shinikizo la damu.
Dawa jamii ya beta bloka ikiwa pamoja na Carvedilol hufanya kazi zifuatvyo ili kupunguza shinikizo la damu;
Hufanya kazi kwa kuzuia matendo yanayosababisha mapigo ya moyo kwenda kasi kwa kupinga utendji kazi wa seli za beta adrenorisepta.
Matendo ya carvedilol kwenye seli za alfa 1 adrenejik risepta hufanya misuli ya damu kulainika, hivyo hupelekea kupungua kwa upinzani wa mzunguko wa damu ndani ya mishipa ya damu. Matendo haya hupelekea kupungua kwa shinikizo la damu na hivyo kuruhusu mzunguko wa damu kuwa mzuri mwilini.
Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo;
Acebutolol (Sectral)
Betaxolol (Kerlone)
Bisoprolol (Zebeta, Ziac)
Carteolol (Cartrol)
Labetalol (Normodyne, Trandate)
Metoprolol (Lopressor, Toprol-XL)
Nadolol (Corgard)
Nebivolol (Bystolic)
Penbutolol (Levatol)
Pindolol (Visken)
Propanolol (Inderal)
Sotalol (Betapace)
Timolol (Blocadren)
Kazi za hii dawa ni kama ifuatavyo:
Hutumika kwenye matibabu ya wagonjwa wenye shinikizo la damu la juu
Hutumika kwenye matibabu ya wagonjwa wenye Anjaina pektorisi
Hutumika kwenye matibabu ya wagonjwa waliopata mayokadio infaksheni
Hutumika kwa matibabu ya Moyo kuferi
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo:
Acebutolol
Betaxolol
Bisoprolol
Carvedilol
Celiprolol
Clonidine
Digoxin
Diltiazem
Esmolol
Labetalol
Lofexidine
Metoprolol
Nadolol
Nebivolol
Penbutolol
Pindolol
Propranolol
Rivastigmine
Saquinavir
Sotalol
Timolol
Verapamil
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao:
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Beta bloka
Dawa hii inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wafuatao;
Wagonjwa wenye kisukari
Wagonjwa wenye haipathairodizim
Wagonjwa wenye shida ya Ini
Wagonjwa wenye shida ya Moyo kuferi
Wagonjwa wenye umri mkubwa
Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi hili la (beta bloka):
Nusu ya maisha ya dawa hii huchukua masaa saba mpaka kumi baada ya kutumiwa
Asilimia 16 ya dawa hii hutolewa mwilini kwa njia ya mkojo
Kundi la dawa kipindi cha ujauzito
Dawa hii ipo kwenye kundi C la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito
Matumizi kwa mama mjamzito
Dawa hii itumike wakati wa tahadhari ambapo hamna dawa nyingine ya mbadala ya kumpa mama mjamzito. Takwimu zinaonyesha kuwa kuna madhara ya kutumia hii dawa
Matumizi wakati wa kunyonyesha
Hakuna takwimu zinazoonesha kuwa dawa hii inaweza kuathiri maziwa ya mama anayenyonyesha, hata hivyo itumike kwa uangalifu.
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni pamoja na;
Kizunguzungu
Mwili kuchoka
Kuongezeka uzito
Kuharisha
Haipaglaisemia
Maumivu ya kichwa
Anjaina
Kutapika
Kutokwa na vipele
Kuwashwa mwilini
Kukosa usingizi
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Endapo ukisahau kunywa dozi yako, kunywa mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:55:55
Rejea za mada hii:-