Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dkt. Sospeter M, MD
Dkt. Lugonda B, MD
27 Agosti 2026, 05:28:28

Dawa Plozasiran
Plozasiran (Redemplo) ni dawa ya kisasa inayotokana na teknolojia ya RNA interference (RNAi), ambayo hupunguza kwa kiasi kikubwa kiwango cha mafuta aina ya triglycerides kwenye damu. Hutumika zaidi kwa wagonjwa wenye viwango vya juu hatarishi vya triglycerides, hususan Sindromu ya kizazi cha kailomaikronemia(SKK) na tatizo sugu la kiwango cha juu cha triglyceraide kwenye dmau.
Majina mengine ya Plozasiran
Majina mengine ya dawa ya Plozasiran ni;
Redemplo
Plozasiran Injection
Dozi na fomu ya Plozasiran
Plozasiran hupatikana katika fomu ya sindano (subcutaneous injection) yenye ujazo na nguvu maalum ya dozi.Dawa hutolewa kama:
Suluhisho tayari kwa sindano
Kawaida hutolewa kila baada ya wiki 12 kulingana na mwongozo wa daktari
Haitolewi kwa fomu ya vidonge.
Namna Plozasiran inavyofanya kazi yake
Plozasiran hufanya kazi yake kupitia kuingilia kazi za RNA, teknolojia inayozuia mwili kutengeneza protini inayoitwa apoC-III.
ApoC-III ni protini inayozuia kuvunjwa kwa triglycerides. Kwa kuipunguza, mwili hutengeneza uwezo mkubwa wa:
Kuondoa triglycerides kutoka kwenye damu
Kupunguza hatari ya uvimbekinga wa tezi kongosho inayotokana na mafuta mengi
Kuboresha uchakataji wa mafuta mwilini
Kwa ujumla, Plozasiran hulenga sababu ya msingi ya mafuta kupanda badala ya kupambana na dalili pekee.
Dawa zilizo kundi moja na Plozasiran
Dawa zilizo kwenye kundi moja na Plozasiran, yaani dawa za kushusha triglycerides, ni:
Volanesorsen
Olezarsen
Fenofibrate
Gemfibrozil
Icosapent Ethyl (Omega-3)
Niacin
Hizi zote hulenga kupunguza triglycerides lakini kwa njia tofauti na Plozasiran.
Kazi ya dawa Plozasiran
Kupunguza viwango vya triglycerides vilivyopanda kupita kiasi
Kuzuia hatari ya uvimbekinga wa tezi kongosho kutokana na mafuta kupanda
Kuboresha uchakataji wa mafuta mwilini
Kusaidia wagonjwa wenye matatizo ya kijenetiki ya mafuta (kama FCS)
Usitumie Plozasiran wakati gani?
Plozasiran haipaswi kutumika kwa wagonjwa wenye:
Mzio uliothibitishwa kwa dawa hii
Mzio kwa viambato vya dawa
Maambukizi makali sehemu ya sindano
Ugonjwa wa ini uliokithiri (hutathminiwa na daktari)
Tahadhari kwa watumiaji wa Plozasiran
Tumia kwa uangalifu kama una ugonjwa wa ini
Dawa hii haijathibitishwa kutibu viwango vya kawaida vya mafuta, inalenga viwango vya juu hatarishi
Wagonjwa wanaopata maumivu au wekundu sehemu ya sindano wanapaswa kumjulisha daktari
Usijidunge sindano bila maelekezo sahihi ya mtaalamu
Huweza kuhitaji ufuatiliaji wa vipimo vya damu mara kwa mara
Dawa ambazo ni mwiko kutumika pamoja na Plozasiran
Dawa zifuatazo zinaweza kuingiliana vibaya na Plozasiran na hazishauriwi kutumiwa pamoja:
Warfarin
Cyclosporine
Gemfibrozil (inaongeza hatari ya madhara)
Clopidogrel
Dawa za kupunguza ini kufanya kazi (hepatotoxic drugs)
Dawa za kupunguza kinga mwilini (immunosuppressants)
(Orodha kamili hutegemea maelekezo ya daktari na vipimo.)
Dawa ambazo zinaweza kuleta madhara yakitumika na Plozasiran
Statini (Simvastatin, Lovastatin, Rosuvastatin) – zinaweza kuongeza hatari ya maumivu ya misuli
Fenofibrate – huongeza hatari ya athari za ini
Mafuta Asidi za Omega-3 – zinaweza kuongeza athari za kuganda kwa damu
Methotrexate – huongeza hatari ya sumu ya ini
Amiodarone – huongeza hatari ya usumbufu wa umeme wa moyo
Daktari lazima ajue dawa zote unazotumia kabla ya kutumia Plozasiran.
Matumizi ya Plozasiran na chakula
Hakuna ulazima wa kuchukua pamoja na chakula kwa kuwa ni sindano
Hata hivyo, ulaji bora wa lishe yenye mafuta kidogo huongeza ufanisi wa dawa
Wagonjwa wenye SKK hutakiwa kuepuka mafuta kwa kiwango cha juu
Endapo utatapika baada ya Plozasiran ufanyaje?
Kwa kuwa ni sindano, kutapika hakubadilishi ufanisi wa dawa.Hivyo:
Hakuna haja ya kurudia dozi
Endelea na ratiba iliyopangwa na daktari
Ikiwa kutapika kunaambatana na dalili za mzio au maumivu makali, wasiliana na daktari.
Maudhi ya Plozasiran
Madhara ya kawaida
Maumivu au wekundu sehemu ya sindano
Uchovu wa muda mfupi
Maumivu ya kichwa
Kichefuchefu
Hisia za kuishiwa nguvu
Maumivu ya misuli
Madhara yanayotokea mara chache
Muwasho sehemu ya sindano
Kuvimba kidogo kwa ini (huchunguzwa kwa vipimo)
Dalili za mzio (mara chache)
Matumizi ya Plozasiran kwenye ujauzito
Tafiti bado ni chache kuhusu usalama kwa wajawazito
Haijulikani kama inaongeza hatari yoyote kubwa kwa mtoto
Hutolewa tu pale faida kwa mama zinapokuwa kubwa kuliko hatari
Wanawake wanaopanga ujauzito wanapaswa kushauriana na daktari kabla ya matumizi
Matumizi ya Plozasiran kwa mama anayenyonyesha
Haijathibitishwa kama dawa inaingia kwenye maziwa ya mama
Kuna ushahidi wa wanyama unaonyesha uwezekano wa kuingia kwenye maziwa
Daktari hupima faida dhidi ya hatari kabla ya kuamua
Ikiwa lazima kutumia dawa, mtoto afuatiliwe kiafya
Endapo umesahau dozi ya Plozasiran ufanyaje?
Kwa kuwa dozi hutolewa kila baada ya wiki 12:
Wasiliana na kliniki au daktari mara moja
Usijidunge bila ushauri
Punguza ucheleweshaji ili kudumisha ufanisi wa dawa
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeandikwa:
2 Machi 2026, 08:00:39
Rejea za mada hii:-

