top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

26 Oktoba 2020 07:23:29

Dawa ya Albaconazole

Dawa ya Albaconazole

Albaconazole ni dawa mojawapo ya kutibu magonjwa ya fangasi iliyopo katika kundi la dawa linaloitwa antifangasi linaloitwa Triazole. Rangi yake huwa ni ya nyeupe, hata hivyo rangi hutegemea aina ya kiwanda kinachotengeneza

Fomu na uzito wa dawa Albaconazole


Dawa hii hupatikana katika mfumo wa kidonge katika milligramu zifuatazo : ⦁ 100 Mg ⦁ 200 Mg ⦁ 300 Mg ⦁ 400 Mg

Dawa zilizo kundi moja na Albaconazole


Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo: ⦁ Efinaconazole ⦁ Epoxiconazole ⦁ Isavuconazole ⦁ Itraconazole ⦁ Posaconazole ⦁ Propiconazole ⦁ Ravuconazole ⦁ Terconazole ⦁ Voriconazole


Namna Albaconazole inavyoanya kazi


Dawa ya Albaconazole ni aina ya dawa ambayo hufanya kazi kwa kufungamana na steroli (ergosteroli) kwenye ukuta wa seli ya fangasi. Kwa kufanya hivi hutengeneza matundu na kufanya ukuta wa seli kuwa na uzaifu ambapo hupelekea kuruhusu kuvuja kwa sehemu za ndani na kufa. Ergosteroli ni aina ya steroli ambayo ni kuu katika ukuta wa seli ya fangasi na ni sehemu ambayo dawa hii hufanya kazi yake na dawa nyingine ya antifangasi linaloitwa Triazole.

Kazi za ya Albaconazole


Hutumika kwenye matibabu ya maradhi ya fangasi ya mwili mzima


Dawa ambazo hazipaswi kutumika pamoja na Albaconazole


Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo: ⦁ Alfuzosin ⦁ Alprazolam ⦁ Cobimetinib ⦁ Conivaptan ⦁ Dihydroergotamine ⦁ Dihydroergotamine intranasal ⦁ Disopyramide ⦁ Dronedarone ⦁ Eliglustat ⦁ Flibanserin ⦁ Ibutilide


Wagonjwa wasiopaswa kutumia Albaconazole


Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi


Matumizi ya Albaconazole kwa mama anayenyonyesha


Dawa hii inaweza kutumika endapo itahitajika sana kwa mama mjamzito bila kuwepo kwa dawa nyingine mbadala


Matumizi ya Albaconazole kwa mama anayenyonyesha


Hakuna takwimu zinazoonyesha kuwa dawa hii hutolewa kwenye maziwa ,Inaweza kutolewa kwa tahadhari


Maudhi ya Albaconazole kwa mtumiaji


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni pamoja na : ⦁ Kutapika ⦁ Maumivu ya tumbo na kichwa ⦁ Kizunguzungu ⦁ Kuharisha ⦁ Mwili kuwa wa njano


Je endapo utasahau dozi yako Albaconazole ufanyaje ?


Endapo ukisahau kutumia dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 16:54:56

Rejea za mada hii:-

1.Drugs.Albaconazole.https://drugs.ncats.io/drug/YDW24Y8IAB. Imechukuliwa 13/10/2020

2.PubChem.Albaconazole.https://pubchem.ncbi.nlm.nih.gov/compound/Albaconazole. Imechukuliwa 13/10/2020

3.DrugBank.Albaconazole.https://www.drugbank.ca/drugs/DB12073. Imechukuliwa 13/10/2020

4.Aspergillus.Albaconazole.https://www.aspergillus.org.uk/IsavuconazoleAlbaconazoleRavuconazole. Imechukuliwa 13/10/2020
bottom of page