top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

26 Oktoba 2020 06:15:49

Dawa ya Butenafine

Dawa ya Butenafine

Butenafine ni dawa mojawapo ya kutibu magonjwa ya fangasi iliyopo katika kundi la dawa linaloitwa antifangasi aina ya allylamine. Dawa hii huwa maarufu kwa majina ya lotrimin na mentax


Fomu ya dawa Butenafine


Butenafine hupatikana katika fomu ya krimu yenye uzito mbalimbali, kiini cha dawa huwa kwa katika asilimia 1


Namna Butenafine inavyofanya kazi ili kutibu fangasi


Dawa ya Butenafine ni aina ya dawa ambayo hufanya kazi kwa kufungamana na steroli (ergosteroli) kwenye ukuta wa nje wa seli ya fangasi. Kwa kufanya hivi hutengeneza matundu na kufanya ukuta wa seli kuwa na uzaifu ambapo hupelekea kuruhusu kuvuja kwa sehemu za ndani na kufa. Ergosteroli ni aina ya steroli ambayo ni kuu katika ukuta wa seli ya fangasi na ni sehemu ambayo dawa hii hufanya kazi yake na dawa nyingine za antifangasi aina ya allylamine.


Dawa zilizo kundi moja na Butenafine

Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo:

Amorolfin Naftifine Terbinafine


Kazi ya dawa Butenafine


Hutumika katika kutibu maradhi ya fangasi kama yale ya Tinea pedis , Versicolour ,corporis na crusis Fangasi wanaoweza kudhuriwa na dawa hii ni • Epidermophyton floccosum • Malassezia furfur • Trichophyton mentagrophytes • Trichophyton rubrum • Trichophyton tonsurans


Wagonjwa wasiopaswa kutumia Butenafine


Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi


Utofauti wa Butenafine na dawa zingine katika kundi la allylamine


Dawa hii hutolewa mwilini kwa njia ya mkojo kwa asilimia kubwa zaidi kuliko njia zingine. Dawa hii nusu ya maisha ya dawa hii ni masaa 8 hadi 15 tangu itumike mwilini


Matumizi ya Butenafine wakati wa ujauzito na kunyonyesha


Dawa hii ipo kwenye kundi B la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito Dawa hii hushauriwa kutumika kwa hali ya hatari ambapo hamna dawa nyingne mbadala wakati wa kipindi cha ujauzito.Tafiti kwa wanyama zinaonyesha kuwa dawa hii inayo madhara madogo kulinganisha na tafiti za kwa binadamu zinazoonyesha kuwa hakuna madhara yeyote


Matumizi ya Butenafine wakati wa kunyonyesha


Hakuna takwimu zinazoonyesha kuwa dawa hii hutolewa kwenye maziwa ,Inaweza kutolewa kwa tahadhari


Maudhi ya dawa kwa mtumiaji wa Butenafine


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni pamoja na • Ngozi kuungua • Maumivu kwenye ngozi • Ukavu kwenye ngozi • Ngozi kuwasha • Kutokwa na vipele


Je endapo utasahau kutumia dozi ya Butenafine ufanyaje ?


Endapo umesahau kutumia dozi yako ya Butenafine, tumia mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine, acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 16:55:27

Rejea za mada hii:-

bottom of page