Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
27 Oktoba 2020, 05:48:31
Dawa ya Cephalothin
Cephalothin ni aina ya dawa ambayo ipo kwenye kundi la kwanza la antibayotiki jamii ya Cephalosporin. Dawa hii huwa maarufu kwa jina la Cefalotin
Rangi na fomu ya Cephalothin
Rangi ya dawa ni nyeupe lakini mara nyingi hutegemea aina ya kiwanda kinachotengeneza Cephalothin hupatikana katika mfumo wa unga ambao hutumika kwa ajili ya sindano katika Milligramu zifuatazo; Tembe
• 250 mg • 500 mg • 750 mg
Namna Cephalothin inavyofanya kazi
Dawa hii hufanya kazi kwa kuzuia ukuaji wa bakteria kwa kuzuia utengenezaji wa peptidoglacan ambayo huunda ukuta wa seli kwenye bakteria ,Kwa kufanya hivyo hupelekea kufa kwa bakteria
Dawa zilizo kundi moja na cephalothin
Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja la Cephalosporin ya kwanza ni ;
• Cefazolin • Cefadroxil • Cephalexin • Cephapirin • Cephradine
Kazi ya cephalothin
Hutumika kama kinga ya kuzuia Maambukizi wakati wa upasuaji na pia hutumika kwa ajili ya kupambana na Maambukizi mbalimbali kwenye damu, mifupa na Ngozi
Utofauti wa cephalothin na dawa zingine kwenye kundi moja
Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi hili la cephalosporin daraja la kwanza ni
• Dawa hii hutolewa mwilini kwa njia ya mkojo kwa asilimia kubwa zaidi kuliko njia zingine. • Dawa hii nusu ya maisha ya dawa hii ni nusu saa mpaka saa 1 tangu itumike mwilini
Dawa usizopaswa kutumia pamoja na cephalothin
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo • Argatroban • Bivalirudin • Dalteparin • Enoxaparin • Fondaparinux • Heparin • Warfarin • Bazedoxifene • Dienogest • Estradiol • Ethinylestradiol • Probenecid
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Cephalothin
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za cephalosporin
Tahadhari Cephalothin
• Dozi yake inapaswa kupunguzwa kwa mgonjwa mwenye shida ya figo • Matumizi ya muda mrefu huweza kupelekea fangasi kwenye mwili
Matumizi ya cephalothin kwa mama mjamzito
• Dawa hii ipo kwenye kundi B la usalama kwa mama mjamzito • Dawa hii inaweza kutumika kwa mama mjamzito ,Tafiti za wanyama hazionyeshi hatari yeyote kwa mjamzito
Matumizi ya cephalothin kwa mama anayenyonyesha
Inaweza kutumika kwa mama anayenyonyesha sababu hakuna madhara yeyote yaliyoripotiwa
Maudhi ya cephalothin
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni; • Maumivu ya tumbo • Kichefuchefu • Kutapika • Kuharisha • Homa
Endapo umesahau dozi ya cephalothin
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje? Endapo ukisahau kutumia dozi yako tumia mara pale utakapokumbuka na endapo muda wa dozi nyingine umekaribia acha dozi uliyoisahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:54:56
Rejea za mada hii:-