Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
27 Oktoba 2020 06:09:52
Dawa ya Chlortetracycline
Chlortetracycline ni aina ya dawa mojawapo ya antibayotiki ambayo hutumika kupambana na Maambukizi mbalimbali kwenye mwili. Dawa hii huwa maarufu kwa jina aureomycin.
Fomu ya dawa
Chlortetracycline hupatikana katika mfumo wa kidonge na mafuta kwa ajili ya kupaka
Namna dawa inavyofanya kazi
Dawa hii hufanya kazi kwa kuzuia ukuaji wa bakteria kwa kuzuia utengenezaji wa protini kwenye bakteria
Dawa zilizo kundi moja na Chlortetracycline
• Tetracycline • Oxytetracycline • Demexlocycline • Doxycycline • Minocycline • Methacyxline • Rolitetracyxline
Kazi ya dawa Chlortetracycline
Hutumika kwenye matibabu ya maradhi madogo ya ngozi
Utofauti wa pekee wa Chlortetracycline na dawa zingine za kwenye kundi hili la (Tetracycline)
• Dawa hii hutolewa mwilini kwa njia ya kinyesi kwa asilimia kubwa zaidi kuliko njia zingine. • Dawa hii nusu ya maisha ya dawa hii ni masaa 5 hadi 6 tangu itumike mwilini
Usitumie Chlortetracycline na dawa zifuatazo
• Acitretin • Flibanserin • Lomitapide • Tretinoin • flibanserin • lomitapide • tretinoin • Aluminum hydroxide • Aminolevulinic acid • Amoxicillin • Ampicillin • Apalutamide • Atracurium • Avapritinib • Axitinib • Bismuth subsalicylate • Bosutinib • Calcium acetate • Calcium carbonate • Calcium chloride • Calcium citrate • Calcium gluconate • Carbonyl iron • Cisatracurium • Cobimetinib • Dicloxacillin • Eliglustat
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Chlortetracycline
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao • Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za tetracycline • Wagonjwa wa ini
Tahadhari ya dawa hii
Dozi yake inapaswa kupunguzwa kwa mgonjwa mwenye shida ya figo
Matumizi ya Chlortetracycline kwa mama mjamzito
Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
• Dawa hii ipo kwenye kundi B la usalama kwa mama mjamzito • Dawa hii inaweza kutumika kwa mama mjamzito. Tafiti za wanyama hazionyeshi hatari yeyote kwa mjamzito
Matumizi ya Chlortetracycline kwa mama anayenyonyesha
Inaweza kutumika kwa mama anayenyonyesha sababu hakuna madhara yeyote yaliyoripotiwa
Maudhi ya Chlortetracycline
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni; • Kizunguzungu • Kichefuchefu • Kutapika • Kuvimba mdomo • Maumivu kwenye sehemu ya juu ya tumbo
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Endapo ukisahau kunywa dozi yako kunywa mara pale utakapokumbuka na endapo muda wa dozi nyingine umekaribia acha dozi uliyoisahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:54:56
Rejea za mada hii:-