top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

27 Oktoba 2020 06:14:43

Dawa ya Demeclocycline

Dawa ya Demeclocycline

Demeclocycline ni aina ya dawa mojawapo ya antibayotiki jamii ya tetracycline ambayo hutumika kupambana na Maambukizi mbalimbali kwenye mwili. Dawa hii huwa maarufu kwa jina la declomycin.


Muda wa dawa kuanza kufanya kazi


Dawa hii hufanya kazi pale inaponyewa Saa 1 au masaa 2 baada ya kula Hakikisha unakunywa dawa hii kama ulivyoshauriwa na daktari wako kila siku na kwa kiwango cha dozi uliyopewa


Fomu ya dawa


Demeclocycline hupatikana katika mfumo wa kidonge wenye uzito wa milligramu zifuatazo:


  • 150 mg

  • 300 mg


Namna dawa inavyofanya kazi


Dawa hii hufanya kazi kwa kuzuia ukuaji wa bakteria kwa kuzuia utengenezaji wa protini kwenye bakteria


Dawa zilizo kwenye kundi moja na Demeclocycline


Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja (Tetracycline) na dawa hii ni ;

  • Choltetracycline

  • Oxytetracycline

  • Tetracycline

  • Doxycycline

  • Minocycline

  • Methacyxline

  • Rolitetracyxline


Demeclocycline hutibu nini


  • Hutumika kwenye matibabu ya wagonjwa wa Bronchitis ya muda mrefu

  • Hutumika kwenye matibabu ya ugonjwa wa brucellosis

  • Hutumika kwenye matibabu ya ugonjwa wa Trakoma

  • Hutumika kwenye matibabu ya ugonjwa wa conjunctivitis

  • Hutumika kwenye matibabu ya ugonjwa wa kipindupindu


Utofauti wa Demeclocycline na dawa zingine za Tetracycline)


  • Dawa hii hutolewa mwilini kwa njia ya mkojo kwa asilimia kubwa zaidi kuliko njia zingine.

  • Dawa hii nusu ya maisha ya dawa hii ni masaa 11 hadi 17 tangu itumike mwilini


Usitumie Demeclocycline pamoja na


Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;


  • Acitretin

  • Flibanserin

  • Lomitapide

  • Tretinoin

  • flibanserin

  • lomitapide

  • tretinoin

  • Aluminum hydroxide

  • Aminolevulinic acid

  • Amoxicillin

  • Ampicillin

  • Apalutamide

  • Atracurium

  • Avapritinib

  • Axitinib

  • Bismuth subsalicylate

  • Bosutinib

  • Calcium acetate

  • Calcium carbonate

  • Calcium chloride

  • Calcium citrate

  • Calcium gluconate

  • Carbonyl iron

  • Cisatracurium

  • Cobimetinib

  • Dicloxacillin

  • Eliglustat


Demeclocycline isitumike kwa watu wafuatao


  • Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za tetracycline

  • Wagonjwa wa ini

  • Na mama mjamzito kwenye miezi 6 ya mwishoni


Tahadhari ya Demeclocycline


  • Dozi ya Demeclocycline inapaswa kupunguzwa kwa mgonjwa mwenye shida ya figo

  • Huweza kuharibu rangi ya meno kwa mtoto kuanzia kwenye miezi 6 ya mwisho ya mimba hadi miaka 8


Demeclocycline na ujauzito


Demeclocycline inaweza kutumika kwenye miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito na baada ya hapo hairuhusiwi kutumika.


Demeclocycline kipindi cha kunyonyonyesha


Demeclocycline inaweza kutumika kwa mama anayenyonyesha sababu hakuna madhara yeyote yaliyoripotiwa


Maudhi ya Demeclocycline


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni;


  • Kizunguzungu

  • Kichefuchefu

  • Kutapika

  • Kuvimba mdomo

  • Maumivu kwenye sehemu ya juu ya tumbo


Je, kama umesahau dozi ya demeclocycline ufanyaje?


Kama umesahau kutumia dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka. Kama muda wa dozi nyingine umekaribia sana, subiria ufike kisha endelea na dozi kama ulivyoshauriwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 16:54:56

Rejea za mada hii:-

1.British National Formula Written by British Medical Association and pharmaceutical Society ISBN: 978 0 85711 340 5 ukurasa wa 506

2.Medlineplus.Demeclocycline.https://medlineplus.gov/druginfo/meds/a682103.html. Imechukuliwa 23/10/2020

3.WebMd.Demeclecycline.https://www.webmd.com/drugs/2/drug-8769/demeclocycline-oral/details. Imechukuliwa 23/10/2020

4.Medscape.Demeclecycline.https://reference.medscape.com/drug/declomycin-demeclocycline-342551. Imechukuliwa 23/10/2020
bottom of page