top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

27 Oktoba 2020 06:20:22

Dawa ya Doxycycline

Dawa ya Doxycycline

Doxycycline ni antibayotiki jamii ya tetracycline ambayo hutumika kutibu magonjwa yanayotokana na maambukizi ya bakteria.


Majina mengine


Doxycycline huwa maarufu kwa majina ya Vibramycin na monodox.


Muda wa kuanza kazi


Doxycycline hufanya kazi pale inaponyewa Saa 1 au masaa 2 baada ya kula

Fomu ya dawa


Doxycycline hupatikana katika mfumo wa tembe wenye uzito wa;


  • 50 mg

  • 75 mg

  • 100 mg

  • 150 mg


Ufanyaji kazi wa doxycycline


Doxycycline hufanya kazi kwa kushikamana na Ribosome ya bakteria inayohusika kuzalisha protini muhimu zinazojenga mwili wa bakteria. Bila kuwa na hizi protini bakteria hukosa uwezo wa kufanya kazi zake kuleta madhara kwenye mwili. Hivyo Doxycycline hufanya kazi ya kusimamisha uzalishaji wa bakteria badala ya kuua bakteria.


Dawa zilizo kwenye kundi moja na Doxycycline


Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja na Doxycycline ( yaani kundi la tetracyclline) ni;


  • Choltetracycline

  • Oxytetracycline

  • Tetracycline

  • Minocycline

  • Demecycline

  • Methacyxline

  • Rolitetracyxline


Doxycycline hutibu nini?


  • Hutumika kwenye matibabu ya magonjwa ya zinaa kama kaswende na kisonono

  • Hutumika kwenye matibabu ya Maambukizi kwenye mfumo wa juu wa hewa yanayosababishwa na bakteria aina ya mycoplasma pneumoniae


Matumizi ya Doxycycline nje ya kazi yake


Doxycyline hutumika pamoja na dawa Ivermectin na madini zinck katika matibabu ya Ugonjwa wa COVID-19. Hii ni kutokana na tafiti zilizofanyika bara la Amerika na kuonyesha kuwa dawa hii ikitumika pamoja na dawa zilizotajwa, zinauwezo wa kupunguza kwa kasi dalili za COVID-19 pamoja na kuharakisha kupona ugonjwa kwa wagonjwa wenye dalili kali na dalili za kawaida Hata hivyo tafiti zinaonyesha kuwa, hakuna ushahidi wa kutosha kuhusu dawa Ivermectin kutumika kwenye matibabu ya COVID-19 na zinaita kufanyika tafiti nyingi kufanyika zaidi ili kutoa majibu mazuri yenye uhakika.


Upekee wa Doxycycline


  • Dawa hii nusu ya maisha ya dawa hii ni masaa 15 hadi 20 tangu itumike mwilini

  • Dawa hii hutolewa kwa njia ya kinyesi zaidi ukilinganisha na mkojo


Mwingiliano na dawa zingine


Doxycycline haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;


  • Acitretin

  • Flibanserin

  • Lomitapide

  • Tretinoin

  • flibanserin

  • lomitapide

  • tretinoin

  • Aluminum hydroxide

  • Aminolevulinic acid

  • Amoxicillin

  • Ampicillin

  • Apalutamide

  • Atracurium

  • Avapritinib

  • Axitinib

  • Bismuth subsalicylate

  • Bosutinib

  • Calcium acetate

  • Calcium carbonate

  • Calcium chloride

  • Calcium citrate

  • Calcium gluconate

  • Carbonyl iron

  • Cisatracurium

  • Cobimetinib

  • Dicloxacillin

  • Eliglustat


Wagonjwa wasiopaswa kutumia Doxycycline


Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao


  • Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za tetracycline

  • Wagonjwa wa ini

  • Na mama mjamzito kwenye miezi 6 ya mwishoni


Tahadhari ya Doxycycline


  • Dozi yake inapaswa kupunguzwa kwa mgonjwa mwenye shida ya figo

  • Huweza kuharibu rangi ya meno kwa mtoto kuanzia kwenye miezi 6 ya mwisho ya mimba hadi miaka 8


Doxycycline na ujauzito


Dawa hii inaweza kutumika kwenye miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito na baada ya hapo hairuhusiwi kutumika. Soma zaidi kwenye usalama wa dawa wakati wa ujauzito kwa maelezo zaidi.


Doxycycline kipindi cha kunyonyesha


Inaweza kutumika kwa mama anayenyonyesha sababu hakuna madhara yeyote yaliyoripotiwa


Maudhi ya doxycycline


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni;


  • Kizunguzungu

  • Kichefuchefu

  • Kutapika

  • Kuvimba mdomo

  • Maumivu kwenye sehemu ya juu ya tumbo

Je endapo utasahau dozi yako ya doxycycline ufanyaje?


Endapo ukisahau kutumia dozi yako ya doxycycline, tumia mara pale utakapokumbuka. Ikiwa muda wa dozi nyingine umekaribia sana, subiri ufike ili utumie dozi hiyo kama ulivyopangiwa na daktari.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 16:54:56

Rejea za mada hii:-

1.British National Formula Written by British Medical Association and pharmaceutical Society ISBN: 978 0 85711 340 5 ukurasa wa 555

2.Drugs.Doxycline.https://www.drugs.com/doxycycline.html. ImechuDrugs.Doxycline. Imechukuliwa 23/10/2020

3.WebMd.Doxycline.https://www.webmd.com/drugs/2/drug-14449/doxycycline-oral/details. Imechukuliwa 23/10/2020

4.Medscape.https://reference.medscape.com/drug/vibramycin-doryx-doxycycline-342548. Imechukuliwa 23/10/2020

5. LeonCalyet al. The FDA-approved drug ivermectin inhibits the replication of SARS-CoV-2 in vitro
Author links open overlay panel. https://www.sciencedirect.com/science/article/pii/S0166354220302011. Imechukuliwa 05.03.2021

6.CDC. Ivermectin. https://www.covid19treatmentguidelines.nih.gov/antiviral-therapy/ivermectin/. Imechukuliwa 05.03.2021
bottom of page