Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
26 Oktoba 2020, 11:23:28
Dawa ya Efinaconazole
Efinaconazole ni dawa mojawapo ya kutibu magonjwa ya fangasi iliyoko katika kundi la dawa linaloitwa antifangasi aina ya Triazole. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Jublia
Fomu ya dawa Efinaconazole
Efinaconazole hupatikana katika fomu ya mafuta •10%
Namna Efinaconazole inavyofanya kazi kutibu fangasi
Dawa ya Efinaconazole ni aina ya dawa kutoka kundi la antifangasi aina ya Triazole, Dawa hii hufanya kazi zake kwa kuingilia enzaimu inayoitwa saitokromu P-450 ambayo ni muhimu kwa ubadilishaji wa lanosteroli kwenda ergosteroli.Hii inasababisha kupunguza utengenezaji wa ergosteroli na kuongeza upenyezaji wa seli ya fangasi kwasababu ya upunguaji wa kiasi cha ergosteroli ambayo huwa kwenye seli ya fangasi.
Dawa zilizo kundi moja na Efinaconazole
• Fluconazole, • Itraconazole,
• Posaconazole • Posaconazole • Isavuconazole • Voriconazole
Kazi ya Efinaconazole
Hutumika kwenye matibabu ya maradhi ya fangasi.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Efinaconazole
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi
Matumizi ya Efinazonazole wakati wa ujauzito
• Dawa hii ipo kwenye kundi C ya usalama wa dawa kipindi cha ujauzito • Dawa hii hushauriwa kutumika kwa uangalifu wakati wa kipindi cha ujauzito
Matumizi ya Efinazonazole wakati wa kunyonyesha
Takwimu hazijaonyesha kuwa kuna uwezekano wa hii dawa kuingia au kuwa kwenye maziwa ya mtoto ila aishauriwi itumike kwa wamama wajawazito
Maudhi ya Efinazonazole
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni pamoja na : • Maumivu ya sindano • Kupata vipele
Ukisahau dozi ya Efinazonazole
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Endapo ukisahau kutumia dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:54:56
Rejea za mada hii:-