top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

10 Agosti 2020 19:20:22

Dawa ya Fenticonazole

Dawa ya Fenticonazole

Fenticonazole ni dawa mojawapo ya kutibu magonjwa ya fangasi iliyoko kundi la imidazole. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Gynoxin,Lomexin.


Fomu ya dawa Fenticonazole


Fenticonazole hupatikana katika fomu kidonge chenye uzito wa

• 200mg • 600mg Fenticonazole hupatikana pia katika fomu ya krimu yenye asilimia 2% ya kiini cha dawa


Namna Fenticonazole inavyofanya kazi ili kutibu fangasi


Dawa ya Fenticonazole ni aina ya dawa kutoka kundi la antifangasi, Dawa hii hufanya kazi zake kwa kupinga kimeng’enya kinachoitwa saitokromu P-450 ambacho ni muhimu kwa ubadilishaji wa lanosteroli kwenda ergosteroli.Hii inasababisha kupunguza utengenezaji wa ergosteroli na kuongeza upenyezaji wa vitu vigeni kuingia kwenye seli ya fangasi na hivyo hufa.


Dawa zilizo kundi moja na Fenticonazole


Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo:

• Clotrimazole • Econazole • Miconazole • Ketoconazole • Tioconazole


Kazi ya Fenticonazole


Hutumika kwenye matibabu ya maradhi ya fangasi.


Wagonjwa wasiopaswa kutumia Fenticonazole


Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi


Utofauti wa Fenticonazole na dawa zingine kundi la imidazole


Mbali na uwezo wake wa kuua fangasi, dawa hii huwa na uwezo wa kuzuia uzalianaji wa bakteria na parasaiti. Hivyo huwa ni mbadala wa kutumia dawa za antibiotiki katika kutibu maambukizi ya fangasi pamoja na parasaiti jamii ya Trichomonas vaginalis.


Matumizi ya Fenticonazole kipinid cha ujauzito


• Dawa hii ipo kwenye kundi C la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito • Dawa hii hushauriwa kutumika kwa hali ya hatari ambapo hamna dawa nyingne mbadala wakati wa kipindi cha ujauzito.Tafiti kwa wanyama zinaonyesha kuwa dawa hii inayo madhara madogo kulinganisha na tafiti za kwa binadamu zinazoonyesha kuwa hakuna madhara yeyote


Matumizi ya Fenticonazole kwa mama anayenyonyesha


Takwimu Zinaonyesha kuwa kuna uwezekano wa hii dawa kuingia kwenye maziwa ya mtoto hivyo inashauriwa isitumike kwa wamama wanaonyonyesha.


Maudhi ya matumizi ya Fenticonazole


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni pamoja na : • Kuhisi kuungua mwilini • Kuwashwa mwilini


Je endapo utasahau dozi ya Fenticonazole ufanyaje?


Endapo ukisahau kutumia dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine, acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako inayofuata kama ulivyopangiwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 16:55:27

Rejea za mada hii:-

1.Drugs.Fenticonazole.https://www.drugs.com/international/fenticonazole.html. Imechukuliwa 8/8/2020

2.Patient.Fenticonazole.https://patient.info/medicine/fenticonazole-for-vaginal-thrush-gynoxin. Imechukuliwa 8/8/2020

3.Drugbank.Fenticonazole.https://www.drugbank.ca/drugs/DB13434.Imechukuliwa 8/8/2020

4.fenticonazole. NCBI.https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/18840006/. Imechukuliwa 10/09/2020

5, Fenticonazole.Patient.https://patient.info/medicine/fenticonazole-for-vaginal-thrush-gynoxin. Imechukuliwa 10/09/2020
bottom of page