top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

30 Juni 2020 17:25:58

Dawa ya Indoramin

Dawa ya Indoramin

Indoramin


Indoramin ni dawa mojawapo ya kupunguza dalili za tezi dume, dawa hii husinyaza misuli ya kibofu cha mkojo na tezi dume ili kumwezesha mtu kukojoa bila shida. Hujulikana kwa jina jingine la Flomax.


Kundi la dawa


• Alpha Risepta Antagonisti.


Rangi ya dawa


• Rangiya dawa ni nyeupe lakini mara nyingi hutegemea aina ya kiwanda kinachotengeneza.


Unaweza kutumia dawa hii pamoja na chakula?


Unaweza kutumia dawa ya Indoramin pamoja au pasipo na chakula mara moja kwa siku kama utakavyoelekezwa na kushauriwa na daktari wako.


Dawa ina uzito wa miligramu ngapi?


• Dawa hii hupatikana katika mfumo wa kidonge chenye milligram 20


Namna dawa inavyofanya kazi ;


Dawa jamii ya Apha Risepta Antagonisti ikiwemo Indoramin hufanya kazi zifuatazo;


• Hufunga milango ya seli yenye jina la Alpha adrenorisepta na hivyo kupelekea kulegea na kupanuka kwa mishipa ya damu na kuruhusu damu kupita bila shinikizo kubwa.


• Husinyaza misuli ya tezi dume na kibofu cha mkojo kwa mwanaume, kufanyika kwa hili hufanya mgonjwa apate nafuu kwenye dalili za tezi dume.


Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja (Alpha Risepta Antagonisti) na dawa hii ni:


• Alfuzosin

• Alfuzusin

• Bunazosin

• Doxazosin

• Phenoxybenzamine

• Phentolamine

• Prazosin

• Tamsulosin

• Urapidil


Kazi ya dawa


• Hutumika kwa ajili ya kushusha shinikizo la juu la damu kwa wagonjwa wenye presha

• Hutumika kupunguza dalili za tezi dume


Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo :


• Lofexidine

• Sildenafil

• Terazosin

• Vardenafil

• Yohimbe


Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao;


• Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Alpha Risepta Antagonisti


Tahadhari ya dawa hii


• Inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wenye shida ya moyo

• Inapaswa kusimamishwa endapo dalili za anjaina zitaonekana


Kundila dawa kipindi cha ujauzito


• Dawa hii ipo kwenye kundi B la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito


Matumizi kwa mama mjamzito


• Dawa hii inaweza kutumika kwa tahadhari kwa mama mjamzito ,Tafiti kutoka kwa wanyama zinaonyesha hakuna hatari yeyote endapo itatumika


Matumizi kwa mama anayenyonyesha


• Haipaswi kutumika kwa mama anayenyonyesha sababu haijulikani kama hutolewa kwenye maziwa baada ya kutumia dawa hii


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni;


• Maumivu ya kichwa

• Orthostatic hypotension

• Kushindwa kuwa imara katika kujamiana

• Kizunguzungu

• Maumivu ya misuli

• Maumivu ya Jointi


Mengine yanayofanyika Mwilini


• Kiwango cha juu cha dawa kwenye damu hufikiwa kwa saa 1na nusu maisha ya dawa mwilini ni masaa 5

• Mabaki yake hutolewa kwa njia ya Mkojo kwa asilimia 63 na kinyesi kwa asilimia 19


Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?


Endapo ukisahau dozi yako ya dawa unapaswa kunywa mara pale utakapokumbuka na endapo muda wa dozi nyingine umekaribia acha dozi uliyoisahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 16:55:27

Rejea za mada hii:-

1.DrugBank.Indoramin. https://www.drugbank.ca/drugs/DB08950.Imechukuliwa 30/6/2020.

2.Drug.Indoramin. https://www.drugs.com/uk/indoramin-20-mg-tablets-leaflet.html . Imechukuliwa 30/6/2020

3.ScienceDirect.Indoramin.https://www.sciencedirect.com/topics/medicine-and-dentistry/indoramin. Imechukuliwa 30/6/2020

4.PatientInfo.Indoramin.https://patient.info/medicine/indoramin-an-alpha-blocker-doralese. Imechukuliwa 30/6/2020
bottom of page