top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

27 Oktoba 2020 06:26:33

Dawa ya Meclocycline

Dawa ya Meclocycline

Meclocycline ni aina ya dawa mojawapo ya antibayotiki jamii ya tetracycline ambayo hutumika kupambana na Maambukizi mbalimbali kwenye mwili.


Majina mengine ya dawa hii


Dawa hii huwa maarufu kwa jina la Meclocycline Sulfosalicylate.


Namna dawa inavyofanya kazi


Dawa hii hufanya kazi kwa kuzuia ukuaji wa bakteria kwa kuzuia utengenezaji wa protini muhimu kwa bakteria


Dawa zilizo kwenye kundi moja na Meclocycline


Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja (Meclocycline) na dawa hii ni;


  • Choltetracycline

  • Oxytetracycline

  • Tetracycline

  • Minocycline

  • Demecycline

  • Methacyxline

  • Rolitetracyxline


Kazi ya dawa


Hutumika kwenye matibabu ya vidonda vya mdomoni


Utofauti wa pekee wa dawa hii kwenye kundi la Tetracycline


Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi hili la (Tetracycline)


  • Dawa hii nusu ya maisha ya dawa hii ni masaa27 tangu itumike mwilini

  • Dawa hii hutolewa kwa njia ya kinyesi zaidi ukilinganisha na mkojo


Dawa zisizopaswa kutumika na Meclocycline


Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo


  • Acitretin

  • Flibanserin

  • Lomitapide

  • Tretinoin

  • flibanserin

  • lomitapide

  • tretinoin

  • Aluminum hydroxide

  • Aminolevulinic acid

  • Amoxicillin

  • Ampicillin

  • Apalutamide

  • Atracurium

  • Avapritinib

  • Axitinib

  • Bismuth subsalicylate

  • Bosutinib

  • Calcium acetate

  • Calcium carbonate

  • Calcium chloride

  • Calcium citrate

  • Calcium gluconate

  • Carbonyl iron

  • Cisatracurium

  • Cobimetinib

  • Dicloxacillin

  • Eliglustat


Wagonjwa wasiopaswa kutumia dawa hii


Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao


  • Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za tetracycline

  • Wagonjwa wa ini

  • Na mama mjamzito kwenye miezi 6 ya mwishoni


Tahadhari kwa watumiaji wa dawa hii


Dozi yake inapaswa kupunguzwa kwa mgonjwa mwenye shida ya figo

Huweza kuharibu rangi ya meno kwa mtoto kuanzia kwenye miezi 6 ya mwisho ya mimba hadi miaka 8


Matumizi kwa mama mjamzito


Dawa hii ipo kwenye kundi D la usalama kwa mama mjamzito

Dawa hii inaweza kutumika kwenye miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito na baada ya hapohairuhusiwi kutumika


Matumizi wakati wa kunyonyesha


Inaweza kutumika kwa mama anayenyonyesha sababu hakuna madhara yeyote yaliyoripotiwa


Maudhi ya dawa


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni;


  • Kizunguzungu

  • Kichefuchefu

  • Kutapika

  • Homa

  • Kichwa Kuuma


Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?


Endapo ukisahau kutumia dozi yako tumia mara pale utakapokumbuka na endapo muda wa dozi nyingine umekaribia acha dozi uliyoisahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 16:54:56

Rejea za mada hii:-

1.DrugBank.Meclocycline.https://www.drugbank.ca/drugs/DB13092. Imechukuliwa 25/10/2020

2.PubChem.Meclocycline.https://pubchem.ncbi.nlm.nih.gov/compound/Meclocycline. Imechukuliwa 25/10/2020

3.Drugs.Meclocycline.https://www.drugs.com/mtm/meclocycline-sulfosalicylate-topical.html. Imechukuliwa 25/10/2020

4.DrugCentral.Meclocycline.http://drugcentral.org/drugcard/3333. Imechukuliwa 25/10/2020
bottom of page