top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

9 Agosti 2020 17:01:08

Dawa ya Naftifine

Dawa ya Naftifine

Naftifine ni dawa mojawapo ya kutibu magonjwa ya fangasi iliyopo katika kundi la dawa linaloitwa antifangasi aina ya allylamine. Dawa hii huwa maarufu kwa jina la Naftin


Naftifine hupatikana katika mfumo wa mafuta na kimiminika (jeli)


• Mafuta mazito : yenye asilimia 1 na 2 % ya kiini cha dawa

• Jeli : yenye asilimia 1 na 2 % ya kiini cha dawa


Namna dawa inavyofanya kazi ili kutibu fangasi


Dawa ya naftifine ni aina ya dawa ambayo hufanya kazi kwa kufungamana na steroli (ergosteroli) kwenye ukuta wa seli ya fangasi. Kwa kufanya hivyo hutengeneza matundu na kufanya ukuta wa seli kuwa na uzaifu ambapo hupelekea kuruhusu kuvuja kwa sehemu za ndani. Ergosteroli ni aina ya steroli ambayo ni kuu katika ukuta wa seli ya fangasi na ni sehemu ambayo dawa hii hufanya kazi yake na dawa nyingine ya antifangasi aina ya allylamine.Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo:

• Amorolfin

• Butenafine

• Terbinafine


Kazi za hii dawa ni kama ifuatavyo:

• Hutumika kwenye matibabu ya maradhi ya fangasi kwenye ngoziDawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao:


• Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi

• Dawa hii haipaswi kutumika kwenye macho ,pua na mdomo


Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha


Dawa hii bado haijapewa kundi la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito


• Dawa hii inaweza kutumika endapo itahitajika sana kwa mama mjamzito bila kuwepo kwa dawa nyingine mbadala

• Hakuna takwimu zinazoonyesha kuwa dawa hii hutolewa kwenye maziwa ,Inaweza kutolewa kwa tahadhari


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni pamoja na


• Ngozi kuungua

• Maumivu kwenye ngozi

• Ukavu kwenye ngozi

• Ngozi kuwasha

• Kutokwa na vipele


Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje ?


Endapo ukisahau kutumia dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 16:55:27

Rejea za mada hii:-

1. WebMd.Naftifine.https://www.webmd.com/drugs/2/drug-6055-4052/naftifine-topical/naftifine-topical/details. Imechukuliwa 8/8/2020

2. DrugBank.Naftifine.https://www.drugbank.ca/drugs/DB00735. Imechukuliwa 8/8/2020

3. MedlinePlus.Naftifine.https://medlineplus.gov/druginfo/meds/a688020.html. Imechukuliwa 8/8/2020

4. Medscape.Naftifine.https://reference.medscape.com/drug/naftin-naftifine-topical-343497. Imechukuliwa 8/8/2020
bottom of page