top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

9 Agosti 2020 17:14:42

Dawa ya Nystatin

Dawa ya Nystatin

Nystatin ni dawa mojawapo ya kutibu magonjwa ya fangasi iliyopo katika kundi la dawa linaloitwa antifangasi aina ya Polyene. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Mycostatin


Famu na uzito wa Nystatin


Nystatin hupatikana katika mfumo wa unga, Maji na kidonge chenye uzito wa miligramu zifuatazo :


Unga : 100,000uniti/g

Maji : 100,000unit/mL

Kidonge : 500,000 unit


Namna Nystatin inavyofanya kazi


Dawa ya Nystatin ni aina ya dawa ambayo hufanya kazi kwa kufungamana na homoni ergosteroli iliyo kwenye ukuta wa seli ya fangasi. Kwa kufanya hivi hutengeneza matundu yanayoruhusu kupitisha vitu kuingia ndani ya seli ya fangasi hivyo seli hii hufa.


Dawa zilizo kindi moja na Nystatin


Dawa hii ipo kundi moja la polyene sawa na dawa zifuatazo:


Amphotericin B


Kazi ya Nystatin


Hutumika kwenye matibabu ya maradhi ya fangasi ya koo na kinywa

Hutumika katika kutibu fangasi ya mfumo wa chakuka Na mrija wa esofagasi


Dawa usizopaswa kutumia pamoja na Nystatin


Bovine collagen


Wagonjwa wasiopaswa kutumia Nystatin


Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi

Wagonjwa wenye fangasi iliyosambaa mwili mzima


Utofauti wa Nystatin na dawa zilizo kundi la polyene


Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi hili la (Antifangasi):


Dawa hii hutolewa mwilini kwa njia ya kinyesi kwa asilimia kubwa zaidi kuliko njia zingine.

Dawa hii nusu ya maisha ya dawa hii ni masaa 5 hadi 6 tangu itumike mwilini


Matumizi ya Nystatin kwa mama mjamzito


Dawa hii ipo kwenye kundi C la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito

Dawa hii hushauriwa kutumika kwa hali ya hatari ambapo hamna dawa nyingne mbadala wakati wa kipindi cha ujauzito.Tafiti kwa wanyama zinaonyesha kuwa dawa hii inayo madhara madogo kulinganisha na tafiti za kwa binadamu zinazoonyesha kuwa hakuna madhara yeyote


Matumizi ya Nystatin kwa mama anayenyonyesha


• Hakuna takwimu zinazoonyesha kuwa dawa hii hutolewa kwenye maziwa ,Inaweza kutolewa kwa tahadhari


Maudhi ya Nystatin


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni pamoja na :


Kuharisha

Kichefuchefu

Maumivu ya tumbo

Kutapika

Ngozi kuwasha


Ukisahau dozi ya Nystatin


Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje ?


Endapo ukisahau kutumia dozi yako,tumia mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine, acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako inayofuata kama ulivyopangiwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 16:55:27

Rejea za mada hii:-

1.Medscape.Nystatin.https://reference.medscape.com/drug/mycostatin-nilstat-nystatin-342594. Imechukuliwa 7/8/2020

2. WebMd.Nystatin.https://www.webmd.com/drugs/2/drug-8893-8206/nystatin-oral/nystatin-suspension-oral/details. Imechukuliwa 7/8/2020

3.Medicinenet.Nystatin.https://www.medicinenet.com/nystatin_liquid-oral/article.htm. Imechukuliwa 7/8/2020

4.Drugs.Nystatin. https://www.drugs.com/pro/nystatin-oral-suspension.html. Imechukuliwa 7/8/2020

5.Modern pharmacology with Clinical applications written by Charles R. Craig and Robert E. Stitizel ISBN 978-0316159340 ukurasa wa 598-600
bottom of page