Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
30 Juni 2020, 17:39:57
Dawa ya Phentolamine
Phentolamine ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu Iliyopo kwenye kundi la dawa linaloitwa Alpha Risepta Antagonisti.
Dawa hii iliyo maarufu kwa majina ya Regitine na Ora Verse huwa na rangi nyeupe lakini mara nyingi hutegemea rangi ya kiwanda kilichotengeneza dawa
Dawa hii inaweza kutumika pamoja na chakula?
Ndio, phentolamine inapaswa kutumiwa pamoja na chakula mara mbili kwa siku kama utakavyoelekezwa na kushauriwa na daktari wako.
Mfumo wa dawa ni upi?
Phentolamine hupatikana katika mfumo wa unga kwa ajili ya sindano katika milligram 5
Namna dawa inavyofanya kazi;
Dawa jamii ya Apha Risepta Antagonisti ikiwa pamoja na phentolamine hufanya kazi zifuatazo;
Hufunga milango ya seli yenye jina la Alpha adrenorisepta hivyo kupelekea kulegea na kutanuka kwa kipenyo cha mishipa ya damu. Kulegea na kutanuka kwa misuli ya mishipa ya damu hufanya damu ipite kirahisi na matokeo ni kushuka kwa shinikizo la damu.
Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja na dawa hii ni;
Alfuzosin
Bunazosin
Doxazosin
Indoramin
Phenoxybenzamine
Prazosin
Tamsulosin
Terazosin
Urapidil
Kazi ya dawa:
Hutumika kushusha shinikizo la damula juu(presha) kwa wagonjwa wa saratani ya kwenye matibabu ya wagonjwa wa saratani ya pheochromocytoma
Hutumika kushusha shinikizo la juu la damu wakati wa upasuaji kwa mgonjwa mwenye pheochromocytoma
Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi hili la (Alpha Risepta Antagonisti)
Dawa hii huongeza kiasi cha pyruvate kwenye damu tofauti na dawa zingine kwenye kundi hili
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;
Lofexidine
Sildenafil
Tamsulosin
Vardenafil
Yohimbe
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao:
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii dawa zingine jamii ya Alpha Risepta Antagonisti
Tahadhari ya dawa hii
Dozi ya kwanza ya dawa hii huweza kupelekea kushuka ghafla kwa shinikizo la damu na kuleta haipotensheni
Kundi la dawa kipindi cha ujauzito
Dawa hii ipo kwenye kundi C la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito
Matumizi kwa mama mjamzito
Dawa hii inaweza kutumika kwa tahadhari kwa mama mjamzito endapo faida ni nyingi kuzidi hatari
Matumizi kwa mama anayenyonyesha
Haipaswi kutumika kwa mama anayenyonyesha sababu haijulikani kama hutolewa kwenye maziwa baada ya kutumia dawa hii
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa ni;
Pua kubana
Maumivu sehemu ya sindano
Kuharisha
Maumivu ya kifua
Haipotension
Mengine yanayofanyika Mwilini
Kiwango cha juu cha dawa kwenye damu hufikiwa ndani ya dakika 10 hadi 20 na nusu maisha ya dawa mwilini ni dakika 19
Mabaki yake hutolewa kwa njia ya Mkojo kwa asilimia 13
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Endapo ukisahau dozi yako ya sindano unapaswa kuchomwa mara pale utakapokumbuka na endapo muda wa dozi nyingine umekaribia acha dozi uliyoisahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:55:27
Rejea za mada hii:-