Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
26 Oktoba 2020, 13:23:52

Dawa ya Posaconazole
Posaconazole ni dawa mojawapo ya kutibu magonjwa ya fangasi iliyoko katika kundi la dawa linaloitwa antifangasi aina ya Triazole. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Noxafil
Rangi, fomu na uzito Posaconazole
Rangi yake huwa ni njano ila pia mara inatofautiana na mara nyingi utegemea aina ya kiwanda kinachotenegeneza.
Posaconazole hupatikana katika mfumo wa kidonge chenye uzito wa miligramu
100
Posaconazole hupatikana katika mfumo wa maji wenye ujazo wa
Miligramu 40 kwa mililita moja (105mg/ml)
Posaconazole hupatikana katika mfumo wa sindano wenye ujazo 18mg/ml (300mg/vial)
Namna Posaconazole inavyofanya kazi
Dawa hii hufanya kazi zake kwa kuingilia kimeng’enya kinachoitwa inayoitwa saitokromu P-450 ambayo ni muhimu kwa ubadilishaji wa lanosteroli kwenda ergosteroli. Hii inasababisha kupunguza utengenezaji wa ergosteroli ambayo ni muhimu katika utengenezaji wa ukuta wa seli ya fangasi. Kwa kufanya hivyo hufanya seli ya fangasi kufa.
Dawa zilizo kundi moja na Posaconazole
Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo;
Albaconazole
Efinaconazole
Epoxiconazole
Fluconazole
Isavuconazole
Itraconazole
Propiconazole
Ravuconazole
Terconazole
Voriconazole
Kazi ya Posaconazole
Hutumika kwenye matibabu ya maradhi ya fangasi.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Posaconazole
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi
Matumizi ya Posaconazole kwa mama mjamzito
Dawa hii ipo kwenye kundi C ya usalama wa dawa kipindi cha ujauzito
Dawa hii hushauriwa kutumika kwa uangalifu kipindi cha ujauzito
Matumizi ya Posaconazole kwa mama anayenyonyesha
Takwimu hazijaonyesha kuwa kuna uwezekano wa hii dawa kuingia au kuwa kwenye maziwa ya mtoto ila aishauriwi itumike kwa wamama wajawazito
Maudhi ya dawa Posaconazole
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni pamoja na :
Kichefuchefu
Kutapika
Maumivu ya tumbo na kichwa
Kizunguzungu
Kuharisha
Kukosa hamu ya tendo la ndoa
Mwili kuwa manjano
Kuogopa mwanga
Kuwashwa mwili
Endapo umesahau dozi ya Posaconazole
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje ?
Endapo ukisahau kutumia dozi yako, tumia au paka mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine, acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako inayofuata kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:54:56
Rejea za mada hii:-