top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

26 Oktoba 2020 06:23:28

Dawa ya Tioconazole

Dawa ya Tioconazole

Tioconazole ni dawa mojawapo ya kutibu magonjwa ya fangasi iliyoko katika kundi la antifangasi aina ya imidazole. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Vagistat 1.


Fomu ya dawa Tioconazole


Tioconazole hupatikana katika fomu ya krimu yenye ujazo mbalimbali na kiini cha dawa kwa asilimia 6.5%


Namna Tiozonazole inavyofaya kazi


Dawa ya Tioconazole ni aina ya dawa kutoka kundi la antifangasi aina ya imidazole.Dawa hii ya Tioconazole hufanya kazi zake kwa kuharibu ukuta wa seli ya fangasi. Tioconazole na aina nyingine za dawa ya fangasi hufanya kazi kwa kuzuia utengenezaji wa homoni ergosteroli ambayo huhitajika kwa ajili ya kutengeneza ukuta wa seli ya fangasi.


Dawa zilizo kundi moja na Tioconazole


Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo:


  • Bifonazole

  • Butoconazole

  • Clotrimazole

  • Econazole

  • Fenticonazole

  • Isoconazole

  • Ketoconazole

  • Luliconazole

  • Miconazole

  • Omoconazole

  • Oxiconazole

  • Sertaconazole

  • Sulconazole


Kazi ya Tioconazole


Hutumika kwenye matibabu ya fangasi aina ya Kandidiasisi.


Wagonjwa wasiopaswa kutumia Tioconazole


Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi


Matumizi ya Tioconazole kwa mama mjamzito


Dawa hii hushauriwa kutumika kwa uangalifu wakati wa kipindi cha ujauzito


Matumizi ya Tioconazole kwa mama anayenyonyesha


Takwimu hazijaonyesha kuwa kuna uwezekano wa hii dawa kuingia au kuwa kwenye maziwa ya mtoto ila aishauriwi itumike kwa wamama wanaonyonyesha.


Maudhi ya dawa Tioconazole


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni pamoja na;


  • Maumivu ya tumbo

  • Maumivu ya kichwa

  • Kuwashwa kwenye uke


Je endapo utasahau dozi yako ya Tioconazole ufanyaje ?


Endapo ukisahau kutumia dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine, ruka dozi uliyosahau na endelea na dozi yako inayofuata kama ulivyopangiwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 16:55:07

Rejea za mada hii:-

1.Drugs.Tioconazole.https://www.drugs.com/mtm/tioconazole-vaginal.htmll. Imechukuliwa 24/9/2020

2.Medscape.Tioconazole.https://reference.medscape.com/drug/vagistat-1-tioconazole-topical-343494. Imechukuliwa 24/9/2020

3.WebMd.Tioconazole.https://www.webmd.com/drugs/2/drug-63478/tioconazole-1-vaginal/details. Imechukuliwa 24/9/2020

4.Modern pharmacology with Clinical applications written by Charles R. Craig and Robert E. Stitizel ISBN 978-0316159340 ukurasa wa 601

5.Drugbank.Tioconazole.https://www.drugbank.ca/drugs/DB01007.Imechukuliwa 24/9/2020
bottom of page