top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

9 Agosti 2020 16:36:36

Dawa ya Undecylenic acid

Dawa ya Undecylenic acid

Undecylenic acid ni dawa mojawapo ya kutibu magonjwa ya fangasi iliyopo katika kundi la dawa linaloitwa antifangasi. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la cruex.


Fomu ya Undecylenic acid


Undecylenic acid hupatikana kwenye fomu ya unga na Maji au krimu katika asilimia zifuatazo :


 • Unga :10 %, 12% na 19 %

 • Maji : 25%


Namna Undecylenic acid inavyofanya kazi


Dawa ya undecylenic acid ni aina ya dawa ilni aina ya fati acid isiyo na maji, hufanya kazi ya kuzuia utengenezaji wa ukuta wa seli ya fangasi.


Dawa zinazofanya kazi kama Undecylenic acid


Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo:


 • Amphotericin B

 • Butoconazole

 • Capsofungin

 • Ciclopiro

 • Econazole

 • Flucytosine

 • Griseofulvin

 • Itraconazole

 • Miconazole

 • Naftifine hydrochloride

 • Oxiconazole nitrate

 • Sulconazole nitrate

 • Terbinifine

 • Terconazole

 • Tioconazole

 • Tolnaftate

 • Voriconazole


Kazi za Undecylenic acid


Hutumika kwenye matibabu ya maradhi ya fangasi mwilini kutokana na maradhi ya ngozi yanayosababishwa na fangasi aitwaye Tinea Corporis na pedis.


Wagonjwa wasiopaswa kutumia Undecylenic acid


Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi pamoja na wagonjwa watakaoonyesha dalili za kkuwashwa kwa ngozi

Tahadhari kwa watumiaji wa Undecylenic acid


 • Dawa hii ni kwa matumizi ya nje tu

 • Haipaswi kupakwa kwenye macho


Matumizi ya Undecylenic acid kwa mama mjamzito


Dawa hii inaweza kutumika endapo faida ni kubwa kuliko madhara yanayoweza kujitokeza kwa mama mjamzito.


Matumizi ya Undecylenic acid kwa mama anayenyonyesha


Hakuna takwimu zinazoonyesha kuwa dawa hii hutolewa kwenye maziwa ,Inaweza kutolewa kwa tahadhari.


Maudhi ya Undecylenic acid


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni pamoja na:

 • Kuwashwa ngozi


Je endapo utasahau dozi yako ya Undecylenic acid ufanyaje ?


Endapo ukisahau kutumia dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 16:55:27

Rejea za mada hii:-

1. Medscape.undecyclinicacid.https://reference.medscape.com/drug/cruex-caldesene-undecylenic-acid-derivatives-999563 . Imechukuliwa 8/8/2020

2. WebMd.Undecylenicacid.https://www.webmd.com/drugs/2/drug-5999/undecylenic-acid-topical/details. Imechukuliwa 8/8/2020

3. MayoClinic.Undecylenicacid.https://www.mayoclinic.org/drugs-supplements/undecylenic-acid-topical-route/description/drg-20066601. Imechukuliwa 8/8/2020

4. Drugbank.Undecyclenicacid.https://www.drugbank.ca/drugs/DB11117. Imechukuliwa 8/8/2020
bottom of page