top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

29 Aprili 2020 18:33:48

Doxazosin

Doxazosin

Utangulizi


Voriconazole ni dawa mojawapo ya kutibu magonjwa ya fangasi iliyoko katika kundi la dawa linaloitwa antifangasi. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Vfend.


Rangi yake huwa mara inatofautiana na mara nyingi utegemea aina ya kiwanda kinachotenegeneza.


Voriconazole hupatikana katika mfumo wa kidonge chenye uzito wa miligramu,


• 50

• 200


Voriconazole hupatikana katika mfumo wa maji wenye ujazo wa;


• Miligramu 200 kwa mililita 5 za maji (200mg/5ml)


Voriconazole hupatikana katika mfumo wa sindano wenye ujazo wa;

200mg/ml


Namna dawa inavyofanya kazi ili kutibu fangasi


• Dawa jamii ya Antifangasi ikiwa pamoja na Voriconazole hufanya kazi zifuatazo ili kutibu fangasi.Dawa ya Voriconazole ni aina ya dawa kutoka kundi la antifangasi, Dawa hii hufanya kazi zake kwa kuingilia kimeng;enya muhimu kwenye ini kinachoitwa saitokromu P-450.kimeng’enya hichi hubadili kiunda cha lanosteroli kwenda ergosteroli. Ergosteroli ni homoni muhimu sana inayotengeneza vijenzi vya ukuta wan je wa seli ya fangasi. Kukosekana kwa homoni hii hupelekeakuta za seli ya fangasi kuwa dhaifu na hivyo kupoteza maisha na kutozaliwa kwa seli mpya.


Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo:


• Amphotericin B

• Butoconazole

• Capsofungin

• Ciclopiro

• Econazole

• Flucytosine

• Griseofulvin

• Itraconazole

• Miconazole

• Naftifine hydrochloride

• Nystatin

• Oxiconazole nitrate

• Sulconazole nitrate

• Terbinifine

• Terconazole

• Tioconazole

• Tolnaftate


Kazi za hii dawa ni;


• Hutumika kwenye matibabu ya maradhi ya fangasi.

• Hutumika kwenye matibabu ya fangasi kwenye mfumo wa umeng'enyaji wa chakula uliyosababisha na Kandidiasi.


Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;


• Carbamazepine

• Chloroquine

• Cobimetinib

• Conivaptan

• Dihydroergotamine

• Dihydroergotamine intranasal

• Efavirenz

• Eliglustat

• Ergotamine

• Flibanserin

• Ivabradine

• Lefamulin

• Lomitapide

• Lovastatin

• Lurasidone

• Naloxegol

• Phenobarbital

• Pimozide

• Quinidine

• Regorafenib

• Rifabutin

• Rifampin

• Ritonavir

• Sirolimus

• Venetoclax


Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao:


• Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi

• Wagonjwa wenye Magonjwa ya figo


Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi hili ni;


• Dawa hii hutolewa mwili kwa njia ya Ini kwa asilimia kubwa na kwa njia ya mkojo.


Kundi la dawakipindi cha ujauzito


Dawa hii ipo kwenye kundi D ya usalama wa dawa kipindi cha ujauzito


Matumizi kwa mama mjamzito


• Dawa hii hushauriwa kutumika kwa hali ya hatari ambapo hamna dawa nyingne mbadala wakati wa kipindi cha ujauzito.Takwimu zinaonyesha kuwa dawa hii husababisha ujauzito kutoka.


Matumizi kwa mama anayenyonyesha


• Takwimu hazijaonyesha kuwa kuna uwezekano wa hii dawa kuingia au hapana kwenye maziwa ya mama ila itumike kwa wamama wajawazito kwa uangalifu.


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni;


• Kichefuchefu

• Kutapika

• Maumivu ya tumbo na kichwa

• Kizunguzungu

• Kuharisha

• Shinikizo la juu la damu

• Shinikizo la chini la damu

• Kupata homa

• Mapigo ya moyo kwenda haraka

• Kupata maruerue

• Kuogopa mwanga

• Kuwashwa mwili


Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?


Endapo ukisahau kutumia dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi inayofuata kama ulivyopangiwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

3 Novemba 2021 11:36:33

Rejea za mada hii:-

1.FDA. Doxazosin.https://www.accessdata.fda.gov/drugsatfda_docs/label/2009/019668s021lbl.pdf. Imechukuliwa 28.04.2020

2.Drugbank. Doxazosin. https://www.drugbank.ca/drugs/DB00590. Imechukuliwa 28.09.2020
3.Drugs.doxazosin.https://www.drugs.com/doxazosin.html. Imechukuliwa 28/4/2020

4.Medscape.doxazosin.https://reference.medscape.com/drug/cardura-xl-doxazosin-342343. Imechukuliwa 28/4/2020

5.WebMd.doxazosin.https://www.webmd.com/drugs/2/drug-3750-8060/doxazosin-oral/doxazosin-oral/details. Imechukuliwa 28/4/2020

6.MedicinePlus.doxazosin.https://medlineplus.gov/druginfo/meds/a693045.html. Imechukuliwa 28/4/2020

7.Modern pharmacology with Clinical applications written by Charles R. Craig and Robert E. Stitizel ISBN 978-0316159340 ukurasa wa 111-112

8.Clinical pharmacology and Therapeutics Written by James M Ritter ISBN 978-0-340-90046-8 ukurasa wa 193
bottom of page