top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

21 Aprili 2020 20:59:54

Enalapril

Enalapril

Enalapril ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyo katika kundi la dawa linaloitwa angiotensini konventing enzaimu inhibita- ACEIs. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la jina la Vasotec


Uzito na fomu ya Enalapril


Enalapril hupatikana katika mfumo wa kidonge chenye uzito wa miligramu;


 • 2.5mg

 • 5mg

 • 10mg

 • 20mg


Pia hupatikana kwenye mfumo wa kimiminika cha kunywa na maji ya kuchoma.


Ufanyaji kazi wa Enalapril


 • Dawa jamii ya ACEIs ikiwa pamoja na enalapril hufanya kazi zifuatazo ili kupunguza shinikizo la damu

 • Kutanua kipenyo cha mishipa ya damu ya vena na ateri kwa kupinga utengenezaji wa homoni ya angiotensin II na uvunjwaji wa bradykinin. Kutanuka kwa mishipa husababisha mishipa kuwa na kipenyo kikubwa hivyo kushuka kwa shinikizo ndani ya mishipa na matokeo yake ni kupunguza mzigo wa damu unaoingia na kutoka kwenye moyo na kupunguza utendaji kazi wa moyo kupita kiasi.


Dawa kundi moja na Enalapril


Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo:


 • Benazepril

 • Captopril

 • Fosinopril

 • Lisinopril

 • Moexipril

 • Perindopril

 • Quinapril


Enalapril hutibu nini?


Hutumika kwenye matibabu ya wagonjwa wenye shinikizo la damu la juu

Hutumika kwenye matibabu ya moyo ulioferi

•Hutumika kwa watu wenye madhara ya Mishipa ya moyo kushoto yaani ventricula kushindwa kufanya kazi.


Enalapril haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;

 • Aliskiren

 • Sacubitril/valsartan

 • Allopurinol

 • Aspirin

 • Aspirin rectal

 • Azilsartan

 • Candesartan

 • Celecoxib

 • Diclofenac

 • Diflunisal

 • Eprosartan

 • Etodolac

 • Fenoprofen

 • Flurbiprofen

 • Ibuprofen

 • Indomethacin

 • Irbesartan

 • Ketoprofen

 • Ketorolac

 • Lofexidine

 • Losartan

 • Meclofenamate

 • Mefenamic acid

 • Meloxicam

 • Nabumetone

 • Naproxen

 • Olmesartan

 • Oxaprozin

 • Piroxicam

 • Pregabalin

 • Sacubitril/valsartan

 • Salsalate

 • Sulindac

 • Telmisartan

 • Tolmetin

 • Valsartan


Enalapril haipaswi kutumika kwa wagonjwa gani?


Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za ACEIs


Dawa hii inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wafuatao;


 • Wagonjwa wenye shinikizo la damu

 • Wagonjwa wenye riski ya kupata haipakalemia


Matumizi ya Enalapril kwa mama mjamzito


Dawa hii ipo kwenye kundi D la dawa zawakati wa ujauzito


Kwa wamama wajawazito dawa hii haipaswi kutumika kwa sababu husababisha athari kwa mtoto maana upunguza ufanyaji kazi wa kibofu cha mkojo na hivo hupelekea vifo vya watoto hivo isitumike wakati mama ana ujauzito


Matumizi ya Enalapril kwa mama anayenyonyesha


Dawa hii huingia kwenye maziwa ya mama na hivyo mtoto anaweza kuipata kwa kunyonya maziwa hivyo isitishwe kupewa kwa mama anayenyonyeshaBaadhi ya maudhi madogo ya dawa ni;


 • Maumivu ya kichwa

 • Kutapika

 • Kizunguzungu

 • Kichefuchefu

 • Haipakalemia

 • Shinikizo la chini la damu

 • Maumivu ya kifua

 • Kukohoa

 • Vipele kwenye ngozi

 • Kupata vipele kwenye Ngozi


Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?


Endapo ukisahau kunywa dozi yako, kunywa mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

3 Novemba 2021 11:34:13

Rejea za mada hii:-

1.Drugs.enalapril.https://www.drugs.com/enalapril.html. Imechukuliwa 21/4/2020

2.Medscape.enalapril.https://reference.medscape.com/drug/vasotec-enalaprilat-enalapril-342317. Imechukuliwa 21/4/2020

3.WebMd.enalapril.https://www.webmd.com/drugs/2/drug-6301-1560/enalapril-maleate-oral/enalapril-solution-oral/details. Imechukuliwa 21/4/2020

4.MedicinePlus.enalapril.https://medlineplus.gov/druginfo/meds/a686022.html. Imechukuliwa 21/4/2020

5. A Textbook of Clinical Pharmacology and Therapeutics FIFTH EDITION JAMES M RITTER ,LIONEL D LEWIS ,TIMOTHY GK MANT ,ALBERT FERRO. ISBN 978-0-340-90046-8. Ukurasa wa 187-188
bottom of page