Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
22 Aprili 2020, 05:46:36
Lisinopril
Utangulizi
Lisinopril ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyo kwenye kundi la dawa linaloitwa angiotensini konventing enzaimu inhibita- ACEIs. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Zestril, Prinivil, Qbrelis
Rangi ya Lisinopril
Rangi yake huwa inatofautiana, mara nyingi utegemea aina ya kiwanda kinachotenegenza
Uzito na fomu ya Lisinopril
Lisinopril hupatikana katika mfumo wa kidonge chenye uzito wa miligramu,
2.5mg
5mg
10mg
20mg na
30mg
40mg
Ufanyaji kazi wa Lisinopril
Namna dawa inavyofanya kazi kupunguza shinikizo la damu.
Dawa jamii ya ACEIs ikiwa pamoja na lisinopril hufanya kazi zifuatazo ili kupunguza shinikizo la damu
Kutanua kipenyo cha mishipa ya damu ya vena na ateri kwa kupinga utengenezaji wa homoni ya angiotensin II na uvunjwaji wa bradykinin. Kutanuka kwa mishipa husababisha mishipa kuwa na kipenyo kikubwa hivyo kushuka kwa shinikizo ndani ya mishipa na matokeo yake ni kupunguza mzigo wa damu unaoingia na kutoka kwenye moyo na kupunguza utendaji kazi wa moyo kupita kiasi.
Kundi la dawa za Lisinopril
Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo;
Benazepril (Lotensin, Lotensin Hct)
Captopril (Capoten)
Enalaprili (Vasotec)
Fosinopril (monopril)
Moexipril (Univasc)
Perindopril (Aceon)
Quinapril (Accupril)
Kazi ya Lisinopril
Kazi za hii dawa ni kama ifuatavyo;
Hutumika kwenye matibabu ya wagonjwa wenye shinikizo la damu la juu
Hutumika kwenye matibabu ya moyo ulioferi
Hutumika kwa watu kwenye shida ya akyuti myokardio infarksheni ndani ya masaa 24 toka wamepata tatizo hili
Dawa zisizopaswa kutumika na Lisinopril
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;
Valsartan
Tolmetin
Telmisartan
Sulindac
Salsalate
Sacubitril/valsartan
Sacubitril/valsartan
Pregabalin
Piroxicam
Oxaprozin
Olmesartan
Naproxen
Nabumetone
Meloxicam
Mefenamic acid
Meclofenamate
Losartan
Lofexidine
Ketorolac
Ketoprofen
Irbesartan
Indomethacin
Ibuprofen
Flurbiprofen
Fenoprofen
Etodolac
Eprosartan
Diflunisal
Diclofenac
Celecoxib
Candesartan
Azilsartan
Aspirin
Aliskiren
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Lisinopril
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao:
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za ACEIs
Matumizi ya tahadhariya Lisinopril kwa makundi
Dawa hii inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wafuatao;
Wagonjwa wenye matatizo ya damu
Wagonjwa wenye riski ya kupata haipakalemia
Lisinopril Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Dawa hii ipo kwenye kundi C(miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito) na kundi D( miezimitatu ya mwisho wa ujauzito) la dawa salama kipindi cha ujauzito.
Haipaswi kutumika kwa mama mjamzito kwa sababu husababisha athari kwa mtoto tumboni. Madhara hayo kwa mtoto ni haipotension, haipoplezia ya fuvu, anyuria, kuferi wa figo na kifo.
Takwimu hazijaonyesha kuwa kuna uwezekano wa hii dawa kuingia au kuwa kwenye maziwa ya mtoto ila hapendekezwi kutumika
Maudhi ya Lisinopril
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa ni;
Maumivu ya kichwa
Kutapika
Kizunguzungu
Haipakalemia
Kuharisha
Maumivu ya kifua
Kikohozi kikavu
Vipele kwenye ngozi
Anyuria
Mwili kuchoka
Je endapo utasahau dozi ya Lisinopril ufanyaje?
Endapo ukisahau kunywa dozi yako, kunywa mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:38:14
Rejea za mada hii:-