top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

29 Aprili 2020 09:12:23

Lixisenatide

Lixisenatide

Utangulizi


Lixisenatide ni dawa mojawapo ya kutibu ugonjwa wa kisukari aina ya pili iliyopo kwenye kundi la dawa linaloitwa Glucagon like peptide 1 Agonisti. Dawa hii huwa maarafu kwa jina la Adlyxin na hutumika kwa kuchoma sindano mara moja kwa siku kabla ya kifungua asubuhi.


Dawa hii hupatikana katika dozi zifuatazo;


• 50mcg/mL katika 3mL

• 100mcg/mL katika 3 mL


Namna dawa inavyofanya kazi ;


Hufanya kazi kwa kuchochea kongosho kuzalisha homoni ya Insulin mara kiwango cha sukari kinapoongezeka kwenye damu.


Homoni ya Insulini husaidia seli za mwili kutumia na kuhifadhi sukari na hivyo kuiondoa kwenye dmau. Kufanya hivi kiwango cha sukari hupungua sana kwenye damu.


Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja ni;


• Exenatide

• Taspoglutide

• Semaglutide

• Dulaglutide


Kazi za dawa hii ni;


• Hutumika kudhibiti kiasi cha sukari kwa Wagonjwa wa kisukari aina ya pili


Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi hili la (GlP1 Inhibitor) ni;


• Ukilinganisha na dawa zingine za kundi lake, lixisenatide huweza kupunguza ufyozwaji wa dawa zingine za antibayotiki na parasetamo, hivyo mgonjwa anapaswa kutumia dawa zingine saa 1 kabla ya kutumia dawa hii.

• Utendaji kazi wake ni mzuri zaidi katika kuthibiti kiwango cha sukari kwenye damu ukilinganisha na dawa za kundi lake.

• Hufanya kazi vyema kwa wazee na watu wenye uhafifu wa kuona kutokana na kisukari.


Dawa hii inapaswa kufuatiliwa kwa ukaribu inapotumika na dawa zifuatazo;


• Acetaminophen

• Chlorpropamide

• Dienogest

• Ethinylestradiol

• Glimepiride

• Glipizide

• Glyburide

• Insulin degludec

• Insulin detemir

• Insulin glargine

• Mestranol

• Tolazamide

• Tolbutamide


Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao:


• Wagonjwa wenye aleji na dawa hii


Tahadhari ya dawa hii ni;


• Sio mbadala wa Insulin

• Haipaswi kutumika kwa mtu mwenye kisukari aina ya kwanza

• Huweza kupelekea pankreataitizi

• Huweza kupelekea figo kushindwa kufanya kazi

Kundi la dawa kwenye ujauzito


Shirika la dawa ulimwengu bado halijaweka dawa hii kwenye makundi ya dawa salama kipindi cha ujauzito


Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha


Tafiti zilizofanywa kwa wanyama zinaonyesha kuwa, dawa hii ilipotolewa kwa panya na sungura wakati wa ujauzito kipindi cha utengenezwaji wa ogani iliweza kusabababisha uharibifu kwenye mfumo wa mifupa na kupunguza ulaji wa chakula na kuongezeka uzito kwa mtoto. Hivyo, inapaswa kutumika kwa mama mjamzito endapo faida ni kubwa zaidi ya hatari kwa mtoto tumboni


Inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa mama anayenyonyesha kama faida ni kubwa kuliko hatari kwa mtoto


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa ni;


• Kushuka kwa kiasi cha sukari

• Kutapika

• Maumivu ya kichwa

• Kizunguzungu

• Uvimbe sehemu iliyochomwa sindano

• Choo kuwa kigumu

• Maumivu ya tumbo


Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?


Endapo ukisahau kuchoma dozi yako ya sindano choma mara pale utakapokumbuka na endapo muda wa dozi nyingine umekaribia acha dozi uliyoisahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

3 Novemba 2021 11:30:45

Rejea za mada hii:-

1.Drugs.Lixisenatide.https://www.drugs.com/mtm/lixisenatide.html. Imechukuliwa 21/4/2020

2.Diabetes.Lixisenatide.https://www.diabetes.co.uk/diabetes-medication/lyxumia.html. Imechukuliwa 21/4/2020

3.Medscape.Lixisenatide.https://reference.medscape.com/drug/adlyxin-lixisenatide-1000059. Imechukuliwa 21/4/2020

4.MedicineNet.Lixisenatide.https://www.medicinenet.com/adlyxin_lixisenatide/article.htm. Imechukuliwa 21/4/2020
bottom of page