top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

22 Aprili 2020 16:45:58

Metolazone

Metolazone

Utangulizi


Metolazone ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu Pamoja na kupunguza uvimbe wa mwili kutokana magonjwa mbalimbali kama kuferi kufanya kazi kwa moyo na figo na pia inaweza kuzuia shida ya kupumua kutokana na maji kujaa kwenye mapafu.


Dawa hii iliyo kwenye kundi la dawa zinazoitwa Diuretiks , hupatikana katika mfumo wa kidonge kinachotumiwa mara moja kwa siku na hufaamika kwa jina jingine la Zaroxololy.


Rangi ya dawa huweza kuwa nyeupe ,lakini mara nyingi hutegemea aina ya kiwanda kinachotengeneza


Dawa hii haina madhara inapotumika pamoja na chakula


Metolazone hupatikana katika mfumo wa kidonge wenye uzito wa Milligram;

• 2.5mg

• 5mg

• 10mg


Namna dawa inavyofanya kazi


Hufanya kazi kwa kuongeza fugo kupotezaji madini ya kloraidi na sodiamu kwenye mkojo. Madini haya yanapopotea kwenye mkojo huambatana na maji, shinikizo la damu hupungua kutokana nakupungua kwa maji kwenye mishipa ya damu.


Madini haya pia yanapopotea kwenye mkojo Pamoja na maji hurusu maji yaliyotuwama kwenye mwili kupungua pia, ndo maana dawa hii ikitumiwa na watu waliovimba kutokana na kutuwama kwa maji kwenye miguu na sehemu zingine, uvimbe huo hupotea.


Madini ya sodiamu yanapopungua kwenye mishipa ya damu, husababisha kutanuka kwa mishipa ya dam una kushuka kwa shinikizo la damu.


Kazi ya dawa ;

Hutumika kutibu uvimbe wa mwili unaotokana na magonjwa ya moyo kuferi, magonjwa ya ini na figo.


Hutumika kutibu shinikizo la juu la damu.


Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;


• Aminolevulinic acid oral

• Isocarboxazid

• Lofexidine

• Methyl aminolevulinate

• Squill

• Tretinoin


Tahadhari ya dawa;


•Itumike kwa tahadhari kwa wagonjwa wa kisukari, wenye upungufu wa elekrolaiti, wenye madini ya kalisimau kwa wingi kwenye damu na shinikizo la chini la damu.

•Hupaswa kutumika kwa Tahadhari kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo na ini


Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao;


• Wagonjwa wenye mzio na dawa hii

• Wagonjwa Wenye shida ya kukojoa


Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha


Dawa hii ipo kwenye kundi B la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito


Dawa hii imeonekana kutokuwa na madhara kwenye tafiti za Wanyama endapo itatumika kipindi cha ujauzito

Kwa mama anayenyonyesha itumike kwa tahadhari endapo kuna umuhimu kwa sababu kiwango kidogo cha dawa hupita na kuingia kwenye maziwa ya mama na pia dawa hii imeonekana kupunguza kiwango cha maziwa kwa mama anayenyonyesha.


Baadhi ya maudhi maogo ya dawa ni;


• Kushuka kwa shinikizo la damu

• Arizimia

• Kizunguzungu

• Maumivu ya kichwa

• Kuchoka

• Kukosa hamu ya kula

• Kichefuchefu

• Kutapika

• Kukojoa sana

• Kutokuona vizuri

• Elektrolaiti kupungua

• Vipele

• Konstipesheni


Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?


Endapo ukisahau kunywa dozi yako, kunywa mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

3 Novemba 2021 11:30:08

Rejea za mada hii:-

1.MedScape.Metolazone.https://reference.medscape.com/drug/zaroxolyn-metolazone-342416. Imechukuliwa 21/4/2020

2.WebMd.Metolazone.https://www.webmd.com/drugs/2/drug-8431/metolazone-oral/details. Imechukuliwa 21/4/2020

3.MedLinePlus.Metolazone.https://medlineplus.gov/druginfo/meds/a682345.html. Imechukuliwa 21/4/2020

4.Rxlist.Metolazone.https://www.rxlist.com/consumer_metolazone_zaroxolyn/drugs-condition.htm. Imechukuliwa 21/4/2020

5.British National Formula Written by British Medical Association and pharmaceutical Society ISBN: 978 0 85711 340 5 ukurasa wa 229

6.Drugs.com. Metolazone. https://www.drugs.com/breastfeeding/metolazone.html. Imechukuliwa 21.02.2020
bottom of page