Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
22 Aprili 2020 05:55:58
Moexipril
Utangulizi
Moexipril ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyo katika kundi la dawa linaloitwa angiotensini konventing enzaimu inhibita- ACEIs. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Univasc
Rangi ya moexipril
Rangi yake huwa pinki mpauko au nyekundu, hata hivyo mara nyingi hutegemea rangi ya kiwandailiyopendekezwa.
Fomu na uzito wa moexipril
Moexipril hupatikana katika mfumo wa kidonge chenye uzito wa miligramu,
7.5mg na
15mg
Namna moexipril inavyofanya kazi kupunguza shinikizo la damu.
Dawa jamii ya ACEIs ikiwa pamoja na moexipril hufanya kazi zifuatazo ili kupunguza shinikizo la damu
Kutanua kipenyo cha mishipa ya damu ya vena na ateri kwa kupinga utengenezaji wa homoni ya angiotensin II na uvunjwaji wa bradykinin. Kutanuka kwa mishipa husababisha mishipa kuwa na kipenyo kikubwa hivyo kushuka kwa shinikizo ndani ya mishipa na matokeo yake ni kupunguza mzigo wa damu unaoingia na kutoka kwenye moyo na kupunguza utendaji kazi wa moyo kupita kiasi.
Dawa zingine kwenye kundi la moexipril
Moexipril hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo;
Benazepril (Lotensin, Lotensin Hct)
Captopril (Capoten)
Enalaprili (Vasotec)
Fosinopril (monopril)
Lisinopril (Zestril, Prinivil, Qbrelis)
Perindopril (Aceon)
Quinapril (Accupril)
Kazi ya moexipril
Kazi moexipril ni kama ifuatavyo;
Hutumika kwenye matibabu ya wagonjwa wenye shinikizo la damu la juu
Hutumika kwenye matibabu ya figo ulioferi
Dawa zenye mwingiliano na moexipril
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo
Aliskiren
Sacubitril/valsartan
Aspirin
Azilsartan
Candesartan
Celecoxib
Diclofenac
Diflunisal
Eprosartan
Etodolac
Fenoprofen
Flurbiprofen
Ibuprofen
Indomethacin
Irbesartan
Ketoprofen
Ketorolac
Lofexidine
Losartan
Meclofenamate
Mefenamic acid
Meloxicam
Nabumetone
Naproxen
Olmesartan
Oxaprozin
Piroxicam
Pregabalin
Sacubitril/valsartan
Salsalate
Sulindac
Telmisartan
Tolmetin
Valsartan
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao:
Wagonjwa wenye mzio na dawa hii au jamii ya dawa za ACEIs
Tahadhari ya matumizi ya moexipril kwa wagonjwa
Dawa hii inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wafuatao;
Wagonjwa wenye shida ya figo
Wagonjwa wenye riski ya kupata haipakalemia
Moexipril kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Dawa hii ipo kwenye kundi C la usalama wad aw akipindi cha ujauzito
Haipaswi kutumika kwa mama mjamzito kwa sababu husababisha athari kwa mtoto tumboni. Madhara hayo kwa mtoto ni haipotension, haipoplezia ya fuvu, anyuria, kuferi wa figo na kifo.
Takwimu hazijaonyesha kuwa kuna uwezekano wa hii dawa kuingia au kuwa kwenye maziwa ya mtoto ila hapendekezwi kutumika
Maudhi ya moexipril
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa ni;
Kikohozi kikavu
Figo kuferi
Kukojoa protini
Kukojoa sana
Kutokwa na vipele
Maumivu ya kifua
Kichefuchefu
Kuwashwa
Kutapika
Haiponatremia
Kizunguzungu
Ini kuferi
Haipotesheni
Je endapo utasahau dozi ya moexipril ufanyaje?
Endapo ukisahau kunywa dozi yako, kunywa mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:20:49
Rejea za mada hii:-