Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
2 Mei 2020 19:39:47
Olmesartan
Olmesartan ni dawa ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyo kwenye kundi la dawa linaloitwa angiotensini II risepta bloka.
Majina ya kibiashara
Olmesartan hufahamika kwa majina mengine kama;
Benicar
Olmesartan na chakula
Unaweza kunywa olmesartan pamoja au pasipo chakula tumboni kama utakavyoelekezwa na daktari wako.
Fomu na uzito wa Olmesartan
Olmesartan hupatikana katika mfumo wa kidonge chenye uzito wa milligram zifuatazo;
5mg
20mg
40mg
Namna dawa ya Olmesartan inavyofanyakazi
Dawa jamii ya ARBs ikiwa pamoja na Olmesartan hufanya kazi zifuatazo ili kupunguza shinikizo la damu;
Olmesartan hufanya kazi kwa kufunga risepta za Angiotensin II zinazojulikana kwa jina la AT1 Risepta. Risepta hizi hupatikana kwenye moyo,mishipa ya damu na figo. Risepta hizi zinapofungwa hupelekea kutanuka kwa mishipa ya damu hivyo kuwa na kipenyo kikubwa na matokeo yake ni kushuka kwa shinikizo la damu.
Hupinga uzalishwaji wa homoni ya Aldosterone ambayo hutumika kuthibiti kiasi cha sodium na maji, Kiasi cha sodium kinapothibitiwa huweza kupunguza shinikizo la damu kwa hutanua kipenyo cha mishipa ya damu na kuruhusu damu kupita bila shinikizo la juu
Dawa kundi moja na Olmesartan
Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja (Kundi la ARBs) na Olmesartan ni;
Azilsartan
Candesartan
Eprosartan
Irbesartan
Losartan
Telmisartan
Olmesartan hutibu nini?
Olmesartan hutumika kwenye matibabu ya shinikizo la damu la juu
Upekee wa Olmesartan
Utofauti wa pekee wa Olmesartan na dawa zingine ni;
Olmesartan huvumilika kwa wagonjwa wa moyo ulioferi
Ni salama na thabiti kwa wagonjwa wa Portal haipatension wenye shida ya ini
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Olmesartan
Olmesartan haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;
Benazepril
Captopril
Enalapril
Fosinopril
Lisinopril
Lithium
Lofexidine
Moexipril
Perindopril
Potassium Phosphate IV
Quinapril
Ramipril
Trandolapril
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Olmesartan
Olmesartan haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao ;
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au dawa jamii ya ARBs pia haipaswi kutumika pamoja na dawa ya Aliskiren kwa wagonjwa wa kisukari
Wagonjwa wenye kiwango cha uchujaji mkojo (GFR) chini ya Millilitre 60 kwa dakika (GFR<60Ml/min/1.73m2)
Angalizo la Olmesartan
Olmesartan inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wafuatao;
Wagonjwa wenye moyo ulioferi
Wagonjwa wenye angioedema
Wagonjwa wenye Haipotension
Wagonjwa wenye shida ya figo
Olmesartan kwa mjamzito
Itumike kwenye hali ya dharura endapo hakuna dawa nyingine salama kipindi hiki sababu tafiti zinaonyesha yapo madhara kwa mtoto
Olmesartan wakati wa kunyonyesha
Inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa mama anayenyonyesha kwa sababu huingia kwenye maziwa ya mama
Maudhi ya Olmesartan
Baadhi ya maudhi madogo ya Olmesartan ni;
Kichwa kuuma
Kizunguzungu
Haipaglycemia
Maumivu ya mgongo
Dalili kama za mafua
Kuchoka
Kichefuchefu
Haipakalemia
Je, kama umeshau dozi yako ya Olmesartan ufanyaje?
Kama umesahau kutumia dozi yako ya Olmesartan, tumia mara pale utakapokumbuka isipokuwa kama muda wa dozi nyingine umekaribia sana ambapo utapaswa kusubiria muda huo ufike kisha uendelee na dozi kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021 11:27:55
Rejea za mada hii:-