Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
26 Aprili 2020, 09:30:00

Penbutolol
Penbutolol ni dawa ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyo kwenye kundi la beta bloka isiyo na mwingiliano kwenye mfumo wa ki autonomiki.
Majina ya kibiashara
Penbutolol hufahamika kwa majina ya kibiashara kama Levatol.
Fomu na uzito wa Penbutolol
Penbutolol hupatikana katika mfumo wa kidonge chenye uzito wa miligramu 20.
Ufyonzwaji wa Penbutolol
Propranolol hufyonzwa vyema kwenye mfumo wa chakula kisha huingia kwenye mzunguko wa damu, kiwango cha juu kabisa kwenye damu hufikiwa ndani ya masaa 2-3 baada ya kunywa dozi ya kidonge.
Nusu maisha ya Penbutolol
Nusu ya Maisha ya dawa kwenye mwili ni masaa 5 kwa watu wasio na magonjwa ya figo na Ini.
Penbutolol na chakula
Tumia dawa hii pamoja na vyakula vyenye protini ili kuongeza ufyonzaji wake.
Umetaboli wa Penbutolol
Dawa hii hufanyiwa umetaboliu kwenye ini na asilimia 25 tu ya dawa mama huweza kupita kama ilivyo kwenda kwenye mzunguko wa damu mara baada ya kupita kwenye ini.
Utolewaji wa Penbutolol mwilini
Mwili hutoa dawa hii kwenye mzunguko wa damu kwa njia kuu ya mkojo kwa asilimia 90.
Namna Penbutolol inavyofanya kazi
Dawa ya penbutolol pamoja na kuwa kundi la dawa la Beta bloka, ufanyaji kazi wake wa kushusha shinikizo la juu la damu bado haufahamiki. Hata hivyo vitu vinavyochangia dawa hii kushusha shinikizo la damu la juu ni;
Kupunguza mzigo wa moyo kufanya kazi
Kuzuia figo kuzalisha homoni renini
Kupunguza mfumo toniki wa simpathetiki kwenye kituo cha vasomota kilicho ndani ya ubongo .
Dawa kundi moja na Penbutolol
Penbutolol ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo;
Acebutolol (Sectral)
Betaxolol (Kerlone)
Bisoprolol (Zebeta, Ziac)
Carteolol (Cartrol)
Carvedilol (Coreg)
Labetalol (Normodyne, Trandate)
Metoprolol (Lopressor)
Nebivolol (Bystolic)
Pindolol (Visken)
Propanolol (Inderal)
Sotalol (Betapace)
Timolol (Blocadren)
Penbutolol hutibu nini;
Hutumika kwenye matibabu ya wagonjwa wenye shinikizo la damu la juu
Kwa sasa shirika la dawa la U.S.A limeitoa dawa hii sokoni na hivyo haitumiki Bara la amerika. Baadhi ya nchi za afrika kuna baadhi yake zinaituia dawa hii.
Dawa zenye mwingiliano na Penbutolol
Penbutolol haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;
Verapamil
Timolol
Sotalol
Saquinavir
Rivastigmine
Propranolol
Pindolol
Penbutolol
Nebivolol
Nadolol
Metoprolol
Lofexidine
Labetalol
Esmolol
Diltiazem
Digoxin
Clonidine
Celiprolol
Carvedilol
Bisoprolol
Betaxolol
Acebutolol
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Penbutolol
Penbutolol haipaswi kutumika kwa wagonjwa wenye mzio na dawa hii au dawa zingine jamii ya Beta bloka.
Angalizo la Penbutolol
Penbutolol inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wafuatao;
Wagonjwa wenye haipathairodizim
Wagonjwa wenye shida ya figo
Wagonjwa wenye shida ya Ini
Wagonjwa wenye shida ya Moyo kuferi
Penbutolol kwa mjamzito
Dawa hii itumike wakati wa tahadhari tu endapo ambapo dawa nyingine mbadala ya kummpa mama mjamzito.
Penbutolol wakati wa kunyonyesha
Hamna takwimu zinazoonyesha kuwa maziwa ya mama anayenyonyesha yanaweza kuwa na kiasi gani chadawa hii hivyo inatakiwa kutumika kwa uangalifu endapo mamaatakuwa ananyonyesha.
Maudhi ya Penbutolol
Baadhi ya maudhi madogo ya Penbutolol ni;
Kizunguzungu
Msongo wa mawazo
Kuharisha
Kichefuchefu
Kikohozi kikavu
Mwili kuchoka
Je, kama umesahau dozi yako ya Penbutolol ufanyaje?
Kama umesahau dozi yako ya Penbutolol, tumia mara pale utakapokumbuka. Ikiwa muda wa dozi inayofuata umekaribia sana, subiria ufike kisha kunywa dozi moja tu na kuendelea kama ulivyoshauriwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021, 11:25:56
Rejea za mada hii:-