Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
30 Juni 2020 17:08:27
Phenoxybenzamine
Phenoxybenzamine ni dawa mojawapo ya kushusha shinikizo la juu la damu Iliyo kwenye kundi la Alpha Risepta Antagonisti.
Majina ya kibiashara
Phenoxybenzamine hufahamika kwa jina jingine la kibiashara kama Dibenzyline.
Phenoxybenzamine na chakula
Phenoxybenzamine inapaswa kutumiwa pamoja na chakula mara mbili kwa siku kama utakavyoelekezwa na kushauriwa na daktari.
Fomu na uzito wa Phenoxybenzamine
Dawa hii hupatikana katika mfumo wa tembe katika milligram 10
Namna Phenoxybenzamine inavyofanya kaz
Dawa jamii ya apha risepta antagonisti ikiwa pamoja na Phenoxybenzamine hufanya kazi zifuatazo;
Hufunga milango ya seli yenye jina la Alpha adrenorisepta na hivyo kupelekea kulegea na kupanua kipenyo cha mishipa ya damu na kuruhusu damu kupita bila shinikizo kubwa.
Dawa kundi moja na Phenoxybenzamine
Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja (Alpha Risepta Antagonisti) na dawa hii ni;
Phentolamine
Prazosin
Terazosin
Doxazosin
Alfuzosin
Tamsulosin
Indoramin
Urapidil
Bunazosin
Kazi ya Phenoxybenzamine
Hutumika kwenye matibabu ya wagonjwa wa pheochromocytoma kwa ajili ya kushusha shinikizo la juu la damu
Upekee wa Phenoxybenzamine
Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi hili la (Alpha Risepta Antagonisti) ni kwamba Phenoxybenzamine haifanyi vizuri kwenye risepta za alpha 1 na 2 kulinganisha na dawa zingine kwenye kundi hili
Mwingiliano wa Phenoxybenzamine na dawa zingine
Phenoxybenzamine haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo kutokan na kuw ana mwingiliano mkali;
Lofexidine
Sildenafil
Tamsulosin
Vardenafil
Yohimbe
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Phenoxybenzamine
Phenoxybenzamine haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao:
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Alpha Risepta Antagonisti pamoja na wagonjwa wenye tatizo la kushuka shinikizo la damu pale wanaposimama
Tahadhari ya Phenoxybenzamine
Dozi ya kwanza ya dawa hii huweza kupelekea kushuka kwa ghafla kwa shinikizo la damu
Inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wazee
Phenoxybenzamine kwa mjamzito
Dawa hii inaweza kutumika kwa tahadhari kwa mama mjamzito endapo faida ni nyingi kuzidi hatari
Phenoxybenzamine wakati wa kunyonyesha
Haipaswi kutumika kwa mama anayenyonyesha sababu haijulikani kama hutolewa kwenye maziwa baada ya kutumia dawa hii
Nusu maisha ya Phenoxybenzamine
Nusu maisha ya dawa mwilini ni masaa 19 hadi 24
Utolewaji Phenoxybenzamine mwilini
Mabaki yake hutolewa kwa njia ya Mkojo kwa asilimia 60 na Kinyesi kwa asilimia 13
Maudhi ya Phenoxybenzamine
Baadhi ya maudhi madogo ya Phenoxybenzamine;
Orthostatic haipotension
Mapigo ya moyo kwenda kasi
Kizunguzungu
Kuchoka
Mwili kuishiwa nguvu
Mdomo kuwa mkavu
Kichefuchefu
Kutapika
Pua kubana
Je kama umeshau dozi yako ya Phenoxybenzamine ufanyaje?
Kama umesahau dozi yako ya Phenoxybenzamine, unapaswa kutumia mara pale utakapokumbuka. Endapo muda wa dozi nyingine umefika, subiria muda utimie ndipo utumie dozi moja tu kasha kuendelea kama ulivyopangiw ana daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:55:27
Rejea za mada hii:-