top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

9 Mei 2020 18:32:07

Pioglitazone

Pioglitazone

Pioglitazone ni dawa ya kutibu kisukari aina ya pili iliyo kwenye kundi la thiazolidinedione.


Majina ya kibiashara


Pioglitazone hufahamika kwa jina la kibiashara kama Actos.


Hakikisha unakunywa dawa hii kama ulivyoshauriwa na daktari wako kila siku na kwa kiwango cha dozi uliyopewa.


Fomu na uzito wa Pioglitazone


Pioglitazone hupatikana katika fomu ya kidonge chenye uzito wa milligram zifuatazo;


  • 15 mg

  • 30 mg

  • 45 mg


Namna dawa Pioglitazone inavyofanya kazi


Dawa jamii ya thiazolidinedione ikiwa pamoja na Pioglitazone hufanya kazi zifuatazo ili kushusha kiwango chasukari kwenye damu.


Huchochea tezi ya kongosho kuzalisha homon insulin kwa wingi. Homoni hiihupunguza kiwango cha sukari kwenye damu kwa kuongeza seli kutumi na kuhifadhi sukari iliyo kwenye damu.


Dawa kundi moja na Pioglitazone


Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja (Kundi la thiazolidinedione) na dawa hii ni;


  • Rosiglitazone

  • Troglitazone


Pioglitazone hutibu nini?


Hutumika kushusha kiwango cha sukari kwawagonjwa wenye kisukari aina ya pili.


Dawa zenye mwingiliano na Pioglitazone


Pioglitazone haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo kutokana na kuw ana mwingilino mkali.

  • Baricitinib

  • Eluxadoline

  • Gemfibrozil

  • Ethanol


Angalizo


Pioglitazone haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao;


Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au dawa zingine jamii ya thiazolidinedione

Wagonjwa wenye moyo ulioferi


Tahadhari ya Pioglitazone


  • Huweza kupelekea kuongezeka kwa uzito inapotumika pamoja na dawa zingine za kisukari

  • Husababisha mwanamke ambaye anaingi komahedhi kuzalisha yai na hivyo humwongezea hatari ya kupata mimba endapo hatumii uzazi wa mpango.

  • Huweza kupelekea uvimbe wa miguu


Pioglitazone kwa mjamzito


Tafiti zilizofanyikwa kwa wanyama zinaonyesha hakuna madhara katika ukuaji wa mtoto (zilifanyika kwa panya na sungura) hivyo inaweza kutumika kwa tahadhari kwa mama mjamzito.


Pioglitazone kwa mama anayenyonyesha


Hakuna taarifa juu ya upatikanaji wa dawa hii kwenye maziwa hivyo inapaswa kutumika kwa tahadhari endapo faida ni nyingi kuliko hatari kwa mtoto.


Maudhi ya Pioglitazone


Baadhi ya maudhi madogo ya Pioglitazone ni;


  • Kuongezeka kwa shinikizo la juu la damu

  • Moyo kuferi

  • Kuharisha

  • Kupungua kwa kiwango cha damu

  • Maambukizi ya juu ya mfumo wa upumuaji

  • Kichwa kuuma

  • Sukari kushuka

  • Maumivu ya misuli


Nusu maisha ya Pioglitazone


Dawa hii baada ya kumezwa huanza kufanya kazi kwa masaa 3 hadi 4 na hufikia kilele kati ya masaa 2 hadi 4 na Matokeo ya dawa hudumu kwa masaa 24 baada ya dozi kuisha.


Utoaji Pioglitazone mwilini


Mabaki yake hutolewa kwa njia ya Mkojo kwa asilimia 53 na Kinyesi kw asilimia 16.


Je kama umesahau dozi ya Pioglitazone ufanyaje?


Kama umesahau kutumia dozi yako ya Pioglitazone, tumia mara pale utakapokumbuka isipokuwa kama muda wa dozi nyingine umekaribia sana ambao utapaswa kusubiria muda ufike ndipo unywe dozi hiyo tu na kuendelea kama ulivyopangiwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 16:55:55

Rejea za mada hii:-

1.FDA. Pioglitazone. https://www.accessdata.fda.gov/drugsatfda_docs/label/1999/21073lbl.pdf. Imechukuliwa 4/5/2020

2.Modern pharmacology with Clinical applications written by Charles R. Craig and Robert E. Stitizel ISBN 978-0316159340 ukurasawa 775

3.WebMd.Pioglitazone.https://www.webmd.com/drugs/2/drug-17406/rosiglitazone-oral/details. Imechukuliwa 4/5/2020

4.Medlineplus.Pioglitazone.https://medlineplus.gov/druginfo/meds/a699016.html .Imechukuliwa 4/5/2020

5.MedScape.Pioglitazone.https://reference.medscape.com/drug/actos-pioglitazone-342726.Imechukuliwa 4/5/2020
bottom of page