top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

4 Mei 2020 21:54:30

Rabeprazole

Rabeprazole

Rabeprazole ni dawa ya kupunguza uzalishaji wa tindikali tumboni iliyo kwenye kundi la dawa za Protoni pampu inhibita. Dawa hii hutumika katika matibabu ya vidonda vya tumbo na magonjwa kadhaa ya njia ya mfumo wa chakula ikiwemo kucheua tindikali


Majina ya kibiashara


Majina ya kibiashara ya Rabeprazole ni;


  • Aciphex

  • Habeprazole

  • Pariets


Fomula ya kikemikali


Jina la kikemikali la Rabeprazole ni C18H21N3O3S


Jina la kisayansi (IUPAC)


Jina la kisayansi la Rabeprazole ni 2-[[4-(3-methoxypropoxy)-3-methylpyridin-2-yl]methylsulfinyl]-1H-benzimidazole.


Rabeprazole hutib nini?


  • Kutibu vidaonda vya tumbo ( hutumika pamoja na dawa zingine)

  • Kutibu kucheua tindikali- ugonjwa wa gastroesofajio refluksi

  • Kutibu vidonda vya tumbo vinavyo sababishwa na dawa zilizopo kwenye kundi la NSAID.

  • Kutibu hali ambayo sababisha michubuko kwenye koo la chakula kutokana na tindikali ya tumboni.

  • Hutumika Pamoja na dawa za antibakteria kutibu na kutokomeza maambukizi ya bakteria wa Helicobacter pylori ambao husababisha vidonda vya tumbo.

  • Kutibu sindromu ya Zollinger-Ellison


Dozi na fomu ya Rabeprazole


  • Vidonge vya miligramu 20.

  • Tembe za miligramu 5 na 10 kwa Watoto.


Namna ya kutumia Rabeprazole


  • Tumia kama ulivyo elekezwa na daktari wako.

  • Dozi yake hutegemea ugonjwa au hali inayotibiwa.


Namna Rabeprazole inavyofanya kazi


Rabeprazole huzuia hatua za mwisho za utoaji wa tindikali kutoka kwenye seli za tumbo zenye jina la gastrin na hivyo kuruhusu vidonda vya tumbo kupona na kusaidia hali nyingine kutokana na tindikali ya tumboni.


Ufyonzwaji wa Rabeprazole


Dawa hii hufonzwa kwaasilimia 52 baada ya kumeza.Huanza kufanya kazi baada ya saa 1 baada ya kumeza.


Nusu maisha ya Rabeprazole


Hufanya kazi mwilini hadi kwa saa 24.


Umetaboliwa wa Rabeprazole


Huchakatwa na mwili kwenye ini ili iweze kufanya kazi na kuondoa sumu.


Utoaji Rabeprazole mwilini


Taka mwili za mabaki ya rabeprazole hutolewa kwa njia ya mkojo (asilimia 90) na kinyesi (asilimia 10).


Wagonjwa wasiopaswa kutumia Rabeprazole


Rabeprazole ni marufuku kwa wagonjwa wafuatao;


  • Wagonjwa wenye aleji na pantoprazole.

  • Mgonjwa anaetumia dawa zenye rilpivirine.


Tahadhari wakati wa kutumia pantoprazole.


  • Kuhara wakati wakutumia dawa ya pantoprazole kunaweza kusababishwa na bakteria clostridium difficile.

  • Kutumia dawa hii kila siku zaidi ya mara moja kwa muda mrefu kunaongeza uwezekano wa mifupa kuvunjika kwa urahisi.

  • Matumizi ya kila siku kwa muda mrefu kama zaidi ya miaka mitatu yaweza kusbabisha upungufu wa vitamini B-12 kwa kupunguza ufyonzwaji wa vitamini hii

  • Matumizi ya muda mrefu yanaweza kusababisha kiwango cha magneziamu kwenye damu kushuka chini ya kiwango cha kawaida.

  • Matumizi ya zaidi ya mwaka yanaongeza atari ya polipsi kwenye tezi zilizo kwenye fandazi.

  • Inaweza leta ugonjwa wa kusambaa wa lupazi erithromatosasi


Muingiliano na dawa nyingine


Rabeprazole hupunguza ufyonzwaji wa dawa kama vile;

  • Sodium bicarbonate

  • Calcium carbonate

  • Magnesium dihydroxide

  • Magnesium carbonate

  • Magnesium trisilicate

  • Aluminium hydroxide

  • Ketoconazole

  • Atazanavir

  • erlotinib

  • mycophenolate mofetil (MMF).


Kutumia kwa pamoja na dawa ya warfarin inaweza kusababisha kuvuja damu nyingi na kuhatarisha maisha. Inabidi kufuatilia muda wa prothrombini(prothrombin time monitoring).


Dawa ya rabeprazole ikitolewa pamoja na amoxicillin, clarithromycin huongeza kiwango cha rabeprazole na clarithromycin kwenye damu.


Usitumie Rabeprazole pamoja na dawa zifuatazo, kwani husababisha madhara mwilini;


  • Erlotinib

  • Nelfinavir

  • Rilpivirine


Rabeprazole na chakula


Unaweza kutumia rabeprazole pamona na au bila chakula


Rabeprazole kwa mjamuzito


Dawa itumike kwa tahadhari kama faida ya kutumia ni kubwa kuliko madhara; Majaribio kwa wanyama yanaonesha madhara na majaribio kwa binadamu hayajafanyika. Au majaribio kwa wanyama na kwa binadamu hayajafanyika.


Rabeprazole kwa anayenyonyesha


Ni vyema kujitahidi kuepuka matumizi ya dawa hii wakati wa kunyonyesha kwani kwani haifahamaki kama dawa hii hufika kwenye maziwa ya mama, japo kua majaribio yanaonesha kuwa dawa hii inafika kwenye maziwa ya wanyama kama vile panya waliofanyiwa majaribio.


Maudhi madogo ya Rabeprazole


  • Maumivu ya kichwa

  • Kuaharisha

  • Kichefuchefu

  • Maumivu ya tumbo

  • Kutapika

  • Kujamba

  • Kizunguzungu

  • Maumivu ya viungo

  • Homa kwa watoto.

  • Maambukizi kwenye mfumo wa upumuaji kwa watoto.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 16:55:55

Rejea za mada hii:-

1.A Textbook of Clinical Pharmacology and TherapeuticS Fifth ISBN 978-0-340-90046-8 ukurasa wa 251.

2.U.S. Food and Drug Administration:
https://www.accessdata.fda.gov/drugsatfda_docs/label/2014/020973s035204736s005lbl.pdf. Imechukuliwa 01/05/2020 .

3.Medscape: https://reference.medscape.com/drug/aciphex-rabeprazole-342002#6. Imechukuliwa 01/05/2020 .
bottom of page