top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

10 Aprili 2020 19:20:38

Raltegravir

Raltegravir

Ramipril ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyo katika kundi la dawa linaloitwa angiotensini konventing enzaimu inhibita- ACEIs. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Altace.


Fomu na uzito wa Raltegravir


Ramipril hupatikana katika fomu ya kidonge chenye uzito wa;


  • 1.25mg

  • 2.5mg

  • 5mg na

  • 10mg


Namna Raltegravir inavyofanya kazi


Dawa jamii ya ACEIs ikiwa pamoja na ramipril hufanya kazi zifuatazo ili kupunguza shinikizo la damu.


Kutanua kipenyo cha mishipa ya damu ya vena na ateri kwa kupinga utengenezaji wa homoni ya angiotensin II na uvunjwaji wa bradykinin.


Kutanuka kwa mishipa ya damu husababisha mishipa kuwa na kipenyo kikubwa hivyo kushuka kwa shinikizo ndani ya mishipa na matokeo yake ni kupunguza mzigo wa damu unaoingia na kutoka kwenye moyo na kupunguza utendaji kazi wa moyo kupita kiasi.


Dawa kundi moja na Raltegravir


Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo;


  • Benazepril (Lotensin, Lotensin Hct)

  • Captopril (Capoten)

  • Enalaprili (Vasotec)

  • Fosinopril (monopril)

  • Lisinopril (Zestril, Prinivil, Qbrelis)

  • Moexipril (Univasc)

  • Perindopril (Aceon)


Raltegravir hutibu nini?


  • Hutumika kushusha shinikizo la juu la damu kwa wagonjwa wenye shinikizo la damu la juu

  • Hutumika kwa kuzuia riski ya kiarusi na mayocardio infaksheni


Dawa zenye mwingiliano na Raltegravir


Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;


  • Aliskiren

  • Sacubitril/valsartan

  • Aspirin

  • Azilsartan

  • Candesartan

  • Celecoxib

  • Diclofenac

  • Diflunisal

  • Eprosartan

  • Etodolac

  • Fenoprofen

  • Flurbiprofen

  • Ibuprofen

  • Indomethacin

  • Irbesartan

  • ketoprofen

  • Ketorolac

  • Lofexidine

  • Losartan

  • Meclofenamate

  • Mefenamic acid

  • Meloxicam

  • Nabumetone

  • Naproxen

  • Olmesartan

  • Oxaprozin

  • Piroxicam

  • Pregabalin

  • Sacubitril/valsartan

  • Salsalate

  • Sulindac

  • Telmisartan

  • Tolmetin

  • Valsartan


Wagonjwa wasiopaswa kutumia Raltegravir


Raltegravir haipaswi kutumika kwa wagonjwa wenye mzio na dawa hii au zingine jamii ya ACEIs


Angalizo la Raltegravir


Dawa hii inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wafuatao;


  • Wagonjwa walioferi ini

  • Wagonjwa wenye shinikizo la chini la damu


Upekee wa Raltegravir kwenye kundi lake


  • Dawa nusu ya maisha yake kwenye mwili ni kati ya masaaa 2 mpaka 4

  • Dawa hii hutolewa asilimia 60 kwa njia ya mkojo na asilimia 40 kwa njia ya kinyesi


Raltegravir na ujauzito


Haipaswi kutumika kwa mama mjamzito kwa sababu husababisha athari kwa mtoto tumboni. Madhara hayo kwa mtoto ni haipotension, haipoplezia ya fuvu, anyuria, kuferi wa figo na kifo.


Raltegravir kwa mama anayenyonyesha


Takwimu hazijaonyesha kuwa kuna uwezekano wa hii dawa kuingia au kuwa kwenye maziwa ya mtoto ila hapendekezwi kutumika kwa mama anayenyonyesha.


Maudhi ya Raltegravir


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hi ni pamoja na;


  • Maumivu ya kichwa

  • Kukohoa

  • Kizunguzungu

  • Kichefuchefu

  • Kuharisha

  • Shikizo la chini la damu

  • Kutapika


Je endapo utasahau dozi ya Raltegravir ufanyaje?


Kama umesahau kutumia Raltegravir, tumia mara pale utakapokumbuka. Kama muda wa dozi hiyo umekaribia sana, subiria ufike ili utumie dozi hiyo tu kama ulivyopangiwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

3 Novemba 2021 11:25:14

Rejea za mada hii:-

bottom of page