top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

18 Aprili 2020 19:35:06

Saxagliptin

Saxagliptin

Saxagliptin ni dawa jamii ya dipeptidyl peptidase-4 (DPP-4) inayotumika katika matibabu ya kisukari aina ya pili.


Majina ya kibiashara ya Saxagliptin


Saxagliptinhufahamika kwa jina la kibiashara la Onglyza.


Fomu ya Saxagliptin


Dawa hii ni ya kumeza, hutuka baada ya kula chakula au kunywa wakati unakula chakula.


Dawa zilizo kundi moja na Saxagliptin


  • Sitagliptin

  • Alogliptin

  • Linagliptin

  • Vildagliptin


Jinsi Saxagliptin inavyofanya kazi


Hufanya kazi kwa kuongeza kiasi cha homoni za kimetaboli zinazoitwa inkretin ambazo huthibiti kiwango cha glukosi kwenye damu kwa kuchochea kuzalishwa zaidi kwa homoni ya Insulin, hasa baada ya kula

Hupunguza kiasi cha sukari kinazalishwa na ini kisha kuingia kwenye damu.


Saxagliptin hutibu nini?


Hutumika kwa wagonjwa wa kisukari aina ya pili.


Mwingiliano wa Saxagliptin na dawa zingine


Dawa usizopaswa kutumia pamoja na Saxagliptin


  • Apalutamide

  • Erdafitinib

  • Ethanol

  • Idelalisib

  • Ivosidenib

  • Lasmiditan

  • Voxelotor


Wagonjwa wasiopaswa kutumia Saxagliptin


Dawa ya Saxagliptin haipaswi kutumika kwa wagonjwa wenye mzio na dawa hii


Tahadhari ya Saxagliptin


  • Hupelekea maumivu ya jointi

  • Itumike kwa tahadhari kwa mgonjwa wa figo

  • Huweza pankreataitizi


Matumizi ya Saxagliptin Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha


  • Inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa mama mjamzito

  • Hakuna athari zozote kwa mtoto ikitumika kwa mama anayenyonyesha.


Maudhi ya Saxagliptin


  • Maambukizi ya mfumo wa upumuaji ya juu

  • Maumivu ya kichwa

  • Kuvimba uso na kutokwa na vipele

  • Kuvimba miguu

  • Kutapika

  • Kuhara

  • Kichefuchefu

  • Haipoglaisemia


Je endapo umesahau dozi ya Saxagliptin ufanyeje?


Endapo ukisahau tumia dozi yako, tumia dawa mara utakapokumbuka isipokuwa endapo muda wa dozi ingine umefika. Kama muda wa dozi ingine umefika ruka dozi hii uliyosahau na endelea kama ulivyopangiwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

3 Novemba 2021 11:23:52

Rejea za mada hii:-

1.Goodman and Gilman’s The pharmacological Basis of therapeutic ISBN 978-0-07-1624428 ukurasa wa 1264

2.MedScape.Saxagliptin.https://reference.medscape.com/drug/onglyza-saxagliptin-999211. Imechukuliwa 18/4/2020

3.WebMd.Saxagliptin.https://www.webmd.com/drugs/2/drug-152751/saxagliptin-oral/details. Imechukuliwa 18/4/2020

4.DrugBank.Saxagliptin.https://www.drugbank.ca/drugs/DB06335. Imechukuliwa 18/4/2020
bottom of page